Rais Samia: Wananitukana wakitaka niwajibu, sasa siwajibu..
Mama anaupiga mwingi sana ni wivu na chuki zao tu
Ndugu zangu Watanzania,

Leo imekuwa siku ya moto sana na ngumu sana kwa wanasiasa uchwara wa Nchi hii. Leo Rais wetu mpendwa ameshusha NONDO za hatari sana zilizowakosha watanzania na kuibua shangwe kwa watanzania mbalimbali waliokuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka ikulu.

Ambapo Rais Samia amesema ya kuwa amekuwa akitukanwa sana na watu ambao wanataka awajibu lakini amekataa kuwajibu.na badala yake kuendelea kuchapa kazi kwa kasi katika kujenga uchumi wetu.amesema wapo wengine mara wasema mama huyu hafai mara ooo kafanya hivi kafanya vile .lakini anasema yeye hasikilizi Makelele na badala yake anaangalia kazi iliyo mbele yake ya kuujenga uchumi ambao unaendelea kuimarika na kufanya vyema kila iitwayo leo.

Amesema ila yule atakayekwamisha juhudi zake za kuujenga uchumi wetu na mageuzi yake ya uchumi kwa hakika huyo atamkera sana.

Kwa hakika nipo sahihi kabisa naposema kuwa Rais Samia ni Jemedari hodari ,Ni Chuma cha Reli kwelikweli,Jasiri Muongoza Njia ,ni Mama wa shoka ,shujaa wa Afrika na Mwana mageuzi ya kiuchumi. Mungu atupe nini Zaidi ya zawadi hii ya kipekee kabisa ya kutupatia Rais SAMIA ? tunataka nini watanzania wenzangu? Kwanini tunataka tuje kuanza kujuta baadaye na kububujikwa machozi ya majuto ya kumlilia na kwenda kumpigia Magoti Rais Samia arejee tena madarakani?

Tutapata wapi Mwingine aina ya Rais SAMIA?mama mchapa kazi, mama mwenye huruma,upendo,ukarimu, unyenyekevu na mama mwenye kuwajali Watanzania? Kwanini tunataka kumkatisha tamaa mama huyu MZALENDO wakweli na dhati kwa Taifa letu? Kwanini tunataka kuchezea bahati hii tuliyonayo?Hamuoni hata DUNIA itatushangaa na kutuona hatujitambui? Embu tuendelee kumuunga mkono Rais wetu na kuhakikisha kuwa Tunampeleka na kumrejesha Ikulu kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima hapo Mwakani.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

 
Hapo akitoka anaenda kuandaa master plan ya kukopa na kuandaa safari nyingine nje ya nchi.

Hana hoja za kujibu kuhusu muungano uchwara huo ndio maana anasingizia anatukanwa.
Hajasingizia anatukanwa bali ni kweli anatukanwa.Hata yule Askofu Machumu alimwambia kuwa yeye ni zaidi ya Chizi. Quote ".........jina la kumpa maana kama ni uchizi ameshazidi hapo".....
 
Hajasingizia anatukanwa bali ni kweli anatukanwa.Hata yule Askofu Machumu alimwambia kuwa yeye ni zaidi ya Chizi. Quote ".........jina la kumpa maana kama ni uchizi ameshazidi hapo".....
Samia mwenyewe ni mtukanaji namba moja maana aliita katiba "kijitabu"
 
FFFF inaweza mjibu mtu kama LISU, kama kashindwa kinana

FFFF-fighting for food for four years
 
Makonda alishasema kuwa wanaomtukana Rais ni mawaziri wake mwenyewe sasa anawaogopa jumba bovu anawaangushia Chadema.
 
Inabidi Viongozi wetu watofautishe tuhuma/kashfa na matusi,kwani wazalendo wanapokuwa muuluzia Rais wa Nchi yuko wapi?Mbona haonekani ndani ya mipaka ya Nchi?Wana maana nzuri tu.Hawamtukani bali wanataka wajue kiongozi wao mkuu wa Nchi.
 
Kila mtanzania anajionea namna kazi kubwa za kimaendeleo zinavyofayika hapa Nchini. na namna miradi mbalimbali ya kimkakati ilivyokamilika kwa wakati na kuleta
IMG_20240611_163704.jpg
IMG_20240611_163734.jpg
matokeo chanya kwa watanzania
Pumbavu wewe..
 
Inabidi Viongozi wetu watofautishe tuhuma/kashfa na matusi,kwani wazalendo wanapokuwa muuluzia Rais wa Nchi yuko wapi?Mbona haonekani ndani ya mipaka ya Nchi?Wana maana nzuri tu.Hawamtukani bali wanataka wajue kiongozi wao mkuu wa Nchi.
Acha ujinga wako wewe. Kwa hiyo unafikiri kuwa Watanzania ni wajinga kuwa hawafahamu yapi ni matusi na yapi siyo matusi
 
Wananchi wako wanapokuwa kuulizia juwa wanakupenda.Mfano ukiwa Nyumbani kwako Usipoonekana kwa mda watoto wako lazima watauliza Mama yuko wapi? Mbona hatumuoni
 
Back
Top Bottom