PostGE2025 Rais Samia: Wanaochokolewa masikio kuvunja amani, Dar es Salaam nenda kaulize leo kama vijana wanataka kungia njiani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Jana analejelo kuwa kilichowapata kaka zao na dada zao hawawezi kuthubutu kuandamana. Na mijitu mitanganyika inapiga makofi.
Mnajenga visasi, mtafikiwa vizazi vyenu hata kama hampo! Watu watalipiza. Badala ya kufanya reconciliation, mnawadhihaki!
Muda ni mwalimu mzuri!
 
Hapa TZ ukiona watu wamevaa misitu na mishati wako mbele kule wakati Mheshimiwa anahutubia au wamekaa chini - ujue akili kichwani hamna, ni njaa na tumbo tu na unafiki.
 
Ila sisi Watanzania bana….yaani huyu nguchiro anawadhihaki watu wote waliouliwa na ma askari wake halafu na sisi tunamwacha tu atambe!

Kwa anavyotamba hivyo haieleweki hata ni kwa nini aliunda tume ya kumchunguza maana majibu yote anayo!
Jibu ni moja tu “anatumudu”
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Hoteli ya Jaz Elite Aurora iliyopo Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 09 Januari, 2026 amesema ametahadharisha akiwaita wanaochokonolewa kuharibu amani ya nchi kuacha mara moja akikumbusha yaliyojiri Dar es Salaam na kwamba vijana hawatamani hata kuingia njiani.

"Kwa wale wanaochokolewa masikio kuvunja amani ya nchi hii niwasihi acheni mara moja. Amani ikichafuka haichagui na tuulizeni sisi wa upande wa pili ilipochafuka amani Dar es Salaam tu pale nenda kaulize leo vijana kama wanataka kuingia njiani, hakuna anaetamani, amani ikivunjika haichagui."

Vilevile amekiri uwepo wa tofauti za mawazo akisisitiza zisitumike kuleta migawanyo ya kisiasa na kuharibu utulivu wa kisiasa nchini.

"Maendeleo yetu, kunawiri kwetu kupendeza kwetu, kulala na kuamka salama tutunze amani ya nchi yetu tofauti za mawazo zipo lakini zisitugawe wala zisiharibu utulivu wa kisiasa na amani ya nchi yetu"

Tume ya Chande hiache mara moja kupoteza fedha zetu za kodi kwa kuchunguza chanzo cha mauaji ya 29 October. Muuwaji huyu apa anajisifia
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Hoteli ya Jaz Elite Aurora iliyopo Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 09 Januari, 2026 amesema ametahadharisha akiwaita wanaochokonolewa kuharibu amani ya nchi kuacha mara moja akikumbusha yaliyojiri Dar es Salaam na kwamba vijana hawatamani hata kuingia njiani.

"Kwa wale wanaochokolewa masikio kuvunja amani ya nchi hii niwasihi acheni mara moja. Amani ikichafuka haichagui na tuulizeni sisi wa upande wa pili ilipochafuka amani Dar es Salaam tu pale nenda kaulize leo vijana kama wanataka kuingia njiani, hakuna anaetamani, amani ikivunjika haichagui."

Vilevile amekiri uwepo wa tofauti za mawazo akisisitiza zisitumike kuleta migawanyo ya kisiasa na kuharibu utulivu wa kisiasa nchini.

"Maendeleo yetu, kunawiri kwetu kupendeza kwetu, kulala na kuamka salama tutunze amani ya nchi yetu tofauti za mawazo zipo lakini zisitugawe wala zisiharibu utulivu wa kisiasa na amani ya nchi yetu"

Amani ya maandamano ya Wakatoliki ingefanywa kwa WAISLAMU ingekuwa Jihad, karibuni kufunga msikiti hata Mmoja tu uone shughuli yake
 
Ama washauri wake ndio tatizo?.
Hakupaswa kutoa kauli kama hizi wakati huu ambapo kesi ya jinai ICC inaelekea kuanza.
Nahisi washauri wake wana tatizo kubwa, ama wanataka aharibikiwe.

Ni makosa makubwa kuwalaumu washauri. Huyu ni kilaza, hasaidiki, hashauriki, hasikilizi yoyote. Tanzania yote anaiona kama geto lake anaweza kufanya chochote na Watanganyika wote kama watumwa wake.

Ukimpa ushauri mzuri asioupenda anakufukuza kazi, kukuteka ama kukuua kabisa.
 
Ama washauri wake ndio tatizo?.
Hakupaswa kutoa kauli kama hizi wakati huu ambapo kesi ya jinai ICC inaelekea kuanza.
Nahisi washauri wake wana tatizo kubwa, ama wanataka aharibikiwe.

..huenda hashauriki na hafundishiki.

..kwanini anatoa kauli za ajabuajabu wakati kumetokea mauaji makubwa nchini?
 
Makanisa yanatuangusha sana
Kama Makanisa yooooooote yakatoka na kauli moja ya Maandamano tutarudisha nchi kwa wananchi

Kanisa Katoliki na Kanisa la Gwajima tu!
Makanisa mengine yoooote ni laana tu!

Haya Makanisa mawili:
Wakiwaambia waumini wao nchi nzima neno moja tu watu waandamane, basi Asubuhi Njema yaja!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Hoteli ya Jaz Elite Aurora iliyopo Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 09 Januari, 2026 amesema ametahadharisha akiwaita wanaochokonolewa kuharibu amani ya nchi kuacha mara moja akikumbusha yaliyojiri Dar es Salaam na kwamba vijana hawatamani hata kuingia njiani.

"Kwa wale wanaochokolewa masikio kuvunja amani ya nchi hii niwasihi acheni mara moja. Amani ikichafuka haichagui na tuulizeni sisi wa upande wa pili ilipochafuka amani Dar es Salaam tu pale nenda kaulize leo vijana kama wanataka kuingia njiani, hakuna anaetamani, amani ikivunjika haichagui."

Vilevile amekiri uwepo wa tofauti za mawazo akisisitiza zisitumike kuleta migawanyo ya kisiasa na kuharibu utulivu wa kisiasa nchini.

"Maendeleo yetu, kunawiri kwetu kupendeza kwetu, kulala na kuamka salama tutunze amani ya nchi yetu tofauti za mawazo zipo lakini zisitugawe wala zisiharibu utulivu wa kisiasa na amani ya nchi yetu"

Hivi huyu mwanamke anachokonolewa kiasi kwamba anathubutu kuendelea na kauli zake hizo!?

Bado haguswi na vifo vya vijana wa Kitanganyika, ambao baadhi yao anajaribu kuficha miili yao isipatikane ili iweze kupumzishwa na wapendwa wao!?

Hivi anafikiri ya kwamba watu wanekwisha sahau kirahisi namna hiyo. Anaringia matumizi mabaya ya vyombo vya dola ili kuzidi kujengea hofu Watanganyika!?
 
Makanisa yanatuangusha sana
Kama Makanisa yooooooote yakatoka na kauli moja ya Maandamano tutarudisha nchi kwa wananchi

Kanisa Katoliki na Kanisa la Gwajima tu!
Makanisa mengine yoooote ni laana tu!

Haya Makanisa mawili:
Wakiwaambia waumini wao nchi nzima neno moja tu watu waandamane, basi Asubuhi Njema yaja!
Yaani nakwazika sana hata mimi, hivi kinawashinda nini kutoa kauli moja tu jumapili moja maandamano yaanzir hapo hapo kanisani!
 
Ujumbe wa SSH kueleweka inakuwa ngumu lakini lazima maneno magumu yasemwe vichwa vyetu vitafanya kazi ya kuuchambua ugumu ili uweze kueleweka vyema.

Tundu Lissu na Heche waliposema kwamba 'watakinukisha', yale hayawakuwa maneno mabaya kwa wote wanaowasikiliza?.

Wanasiasa hawa wametengeneza fitina kwa muda mrefu sasa matokeo ya dhambi yanapoirudia jamii wote kwa ujumla wetu tunaumia.

Kina Mange kila siku wanarusha video za kutengenezwa na AI lengo sisi tuzidi kumchukia Mheshimiwa SSH hawajui kwamba wanaitengeneza fitina ambayo siku inapoturudi basi atayepona inabidi akamshukuru Mungu.

Simuoni SSH akidhihaki vifo ule ni ujumbe mzito kwamba ukiipoteza amani unaumia mazima, hauwezi hata kuingia JF ukafungua uzi.

Tumetengeneza roho ya chuki na ubaguzi kwa muda mrefu sana, lakini kilichotokea October 29 kinapaswa kiwe fundisho kuhusu kuichezea amani.
 
Back
Top Bottom