Rais Samia wasikudanganye nikodishie Helicopter nikakuonyeshe Wakubwa Watano waliochepusha Maji ya Mto Ruvu

Serikali iwekeze kwenye ujenzi wa mabwawa ya kutunza maji ya mvua, angalua hata lita bilioni 50 haya yanatosha kwa miezi 3 kwa Jiji la Dar na Pwani.
Mradi wa kisarawe upelekwe haraka ili tupate maji yakutosha
 
Mmezidi umbea chukuwa chopa hiyo ukanionyeshe hao waandamizi
🚠🚠🚠
 
Tanzania ni nchi ya mabogus vilaza watu wasio jielewa viongozi hakuna wapo kwa ajili ya maslahi yao wenyewe kazi yao ni kuwaza kuiba hela za umma kwenda kuhonga dada zetu akuna wanachofikiria
Awawezi kutatua changamoto ndogondogo kama maji na umeme wapo wapo tuu kama mazombi bora hii nchi tumpe mkoloni atuongoze maaana atujitambui
Imagine kiongozi mkubwa msomi wa PHd anakaa jukwaani anasema tukae tumwombe mungu ndo atuletee maji na vyanzo vya maji vinapita milangoni mwetu hata huyo wanayesema tumwombe huko aliko anatucheka kweli kweli.
 
Ila huyu maza namuonea huruma yani watu wanaomzunguka kheeee
 
Na kila msimu wa mvua maji yanatiririka kwenda bahari ya hindi; hayo wangeyavuna na kuyatumia kwa mashamba na kuyahifadhi kwenye mabwawa.
 
Mzee kwanini usimwage ugali tu hapa kwa kuwataja wahusika ili wa wakati wa dar wajue shida na matatizo wanayoyapata ni kundi furani ebu wataje
 
Ni huko mbwawa?
 
Wanyonge tunateseka wenye vyao wanajilia na kujichukulia tu...kweli tupo dunia mbili tofauti
 
Lisemwalo lipo GENTAMYCIME asipuuzwe apewe chopa akaonyeshe, Awesu apite na huku, ya mwanafunzi darasa la 7 yalikua km hivi hivi fichua fichua, naomba GENTAMYCIME aongezewe ulinzi na chopa apewe akaonyeshe huo mchepuko wa maji ulipo
Nachoka kila Siku kuwafafanulieni kuwa Siitwi huyu Tapeli GENTAMYCIME aliyeiiga hii ID yangu Ili Kusafiria Nyota yangu Kali ya Kiumaarufu na Kiuwasilishaji wa Kipekee hapa JamiiForums.

Naitwa GENTAMYCINE ambaye nimejiunga hapa Jamiiforums mwaka 2013 Mwezi July na huyu Tapeli wa Kuiiga ID yangu GENTAMYCIME amajiunga hapa miezi.ya Karibuni tu na mwaka huu.

Kwanini msiwe mnazihakiki Kwanza hizi ID's kabla ya Kuzichanganya? Hivi kuna Member mzoefu na mkongwe hapa JamiiForums hajui kuwa ID yangu GENTAMYCINE pia ina Avatar ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin BIBI Netanyahu ambaye namkubali ( nampenda ) mno?

Mnanichosha Kuwafafanulieni 24/7.
 
kama unachokisema ni kweli. umefanya jambo la maana kulitaarifu. lakini umekosea kitu kimoja tu. hoja yako umeiwasilisha kitoto toto zyd.
 
Mkuu kwa hili Dini ulilompa hapa utashangaa hilo Juha ( Fool ) litakuja tena Kukubishia au kuendelea Kuuliza Swali lake la Kipuuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…