Rais Samia: Watanzania tumezoea bure, hakuna hiyo sasa

Madaraka ya kulevya.
 
Kumbe ndio maana hashtuki bei za bidhaa zinavyopanda kila siku, kwa hii mentality tujifunge mikanda.
Katiba imetuletea rais asiyeweza kutawala., bora Bashiru alliance hili mapema akataka uchaguzi.
 
Kati yetu sisi wenye nchi na wao viongozi wa "sirikali" ni yupi hasa anae tegemea na kuzoea vya bure? Acheni mazereu na manyanyaso kiasi hicho vipi nyie
 
Wanzazibar wenzake wanapata umeme na maji bure sisi huku kila kitu tunalipa
Hivi wale mawaziri wazanzibar wanaoambana na mh.Rais kwenye ziara zake huku bara kazi yao huwa nini hasa, utasikia waziri wa bara anasema waziri pacha wangu kutoka Zanzibar simama usalimie kidogo, akisimama utasikia mpapinduzi, mapinduzi, najiuliza wanatoka huko kote kuja kutwambia Mapinduzi.
 
Kazi yao ni kusifia biashara imeisha
 
Hakuna mzanzibar anayepata umeme na maji bure, kila nyumba ina luku hakuna bure sijui nani anawadanganya.
Tumeisha wazoea tabia zenu ni kulialia utadhani hamna mikono ya kufanya kazi.Kwanini hamkuwasha vibatari kama hiyo jeuri mnayo??Sisi watanganyika tumeisha jitolea kuwatunza mpaka Mungu atakapo amua.
 
Wanalipwa posho za safari za watanganyika za bure kwasababu wanataka vya bure na kwasababu rais ni mzznzibar na rais wenyewe ameshindwa kutofautishi mipaka kati ya Tanganyika na zanzibar ndo maana unaona waziri wa Zanzibar anazungumzia maswala ya Tanganyika.
 
Rais Yuko sahihi, watanzania tumekuwa watu wa kulia lia na kulalamika Kama yatima, Ni wakati Sasa watanzania tutambue kuwa ulipaji Kodi niwajibu wetu na sio kulia lia.
 
Wanavunja kaitiba bila kujua au kwa makusudi ili kujipendekeza kwa Rais...
 
Rais Yuko sahihi, watanzania tumekuwa watu wa kulia lia na kulalamika Kama yatima, Ni wakati Sasa watanzania tutambue kuwa ulipaji Kodi niwajibu wetu na sio kulia lia.
Nani halipi kodi wewe? Hivi unakielewa ulichokiandika hapo? Watu wanacholalamikia ni huduma mbovu zinazotolewa na serikali kwa mfano umeme na maji vimekua kero, tena umeme ndio zaidi ni kero kubwa sana, sasa kuna ambae alipii umeme anatumia umeme bure? Ni nani ambae halipii umeme anaetumia umeme bure km sio serikali yenyewe kutegemea kulipia umeme wanaotumia kwa kutumia kodi zetu? Sasa kati ya sisi na wao nani anatumia bure?

Think twice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…