TANZIA Rais wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia
View attachment 2920520
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.

Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.

View attachment 2920484

Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua
Apumzike kwa amani mzee Mwinyi, niliwaza habari yake mchana huu!
 
hii dunia inatufunza nini?

halafu ukute kuna mtu anafanya uovu ili watoto wake waje waishi Maisha mazuri kupitia udhulumaji wake, yaani mpaka unamjengea na nyumba na gari kabisa kupitia dhulma, mwishowe unaondoka na hata huoni tena watoto wako wakiponda raha ambazo ww ndo umewatafutia kwa kudhulumu wengine. tunakumbushana tu. mimi siwezi kuhuzunika kwasababu huyo marehemu hakuwa na shida au dhiki yoyote hapa duniani,
Mzee Mwinyi alikuwa mwadilifu
 
Alale mahala pema peponi mzee Mwinyi hakua na ubaya na mtu , alikua mchamungu na mpenda Haki.
Ni kweli kabisa huyu mzeeataenda mbinguni. Hivi na yeye pia kwenye utawala wake alitia sahihi ya wahalifu kunyongwa?Kama alifanya hivyo alifanya vema sana. Nyerere naye nilimsifu alinyonga kwa kutia sahihi. Kikwete, mkapa na magufuli walituangusha. Mama inabidi anyonge wengi kwa kutia sahihi. Watu wamezidi kuwa makatili sana. Yani unakuta wanamteka dereva wa bodaboda na kumuua kumtoboa macho. Mama nyonga bila huruma usisikize human rights
 
Back
Top Bottom