TANZIA Rais wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia
Nina mambo Matatu.

1. Mwinyi RIP
2. Naona Awamu ya Sita itakuwa ya mwisho Kuwa na wastaafu..
3. Naombea Mazishi Yafanyike Mkuranga Pwani. Wiki iliyopita niliona barabara inachongwa. Je Akizikwa Pwani Atakuwa ameua Muungano?
Hawajamtendea haki kwenda kumzika unguja wakati kwao ni hapo mkuranga.
 
Mzee Mwinyi alikuwa ni Rafiki wa Watu Wote hivyo Watu waachwe wakamzike pasiwepo CHAWA vimbelembele waliojaa Unafiki

Tunategemea Kaswida ziwepo na Siyo hawa Wasanii wetu wa Kampeni

RIP mzee Rukhsa
 
View attachment 2920520
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.

Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.

View attachment 2920484

Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua
Wasisahau kuzingatia wasia wake juu ya namna ya kumuhifadhi
 
Back
Top Bottom