TANZIA Rais wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia
View attachment 2920520
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.

Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.

View attachment 2920484

Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua
Eee Allaah, Mghufurie na Mrehemu, na Muafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Mpanulie kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Jannah na Mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya Moto)[1]
 
View attachment 2920520
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.

Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.

View attachment 2920484

Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua
Allah ampe kauli thabiti amuondolee adhabu za kabri nenda mzee mwinyi mwambie mjomba Magu kinu no 9 kimewashwa!
 
Nye
MSIBA MZITO Kwa Taifa.
Rais Mstaafu wa JMT.
Baba mzazi wa M.Kiti wa Baraza la Mapinduzi.
Mkuu wa chuo bora cha Afya Tanzania (Muhimbili).

Siku ya kukumbuka kifo chake itakuwa kila baada ya miaka minne ... (Miaka yenye mwezi wa pili wenye siku 29 tu)
View attachment 2920492

Hii picha ili trend kipindi cha msiba wa Rais John Pombe.
Nyerere alitariki 1999 ambayo sio leap year.
Magufuli alitariki 2021 ambao sio leap year.
 
Naomba unisamehe na wote mnisamehe sanaa .niliandika kabla yakutagazwa kwa kifo cha mzee wetu.ndio maana nimerudi kurekebisha haraka sana baada ya kupata taarifa za huzuni kwa Taifa letu juu ya msiba wa mzee wetu.naomba mnisamehe sana
How old are you?
 
Niungane na watanzania wenzangu kuomboleza msiba wa rais wetu mstaafu
 
Mkuu mbona unaandika mambo yasiohusiana na thread

Uzi unaongelea msiba wa Rais Mstaafu Mwinyi,Wewe unaongelea habari za Samia

Are u mentally ok?

Kuna wakati kama huna cha kuongea ni heri ukanywa maji na kulala
Njaa mbaya sana.
 
Back
Top Bottom