Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Hapana, Mzee wetu tunamsitiri UNGUJA, ZANZIBAR.Mzee wetu azikwe mahali pachimbuko lake (Tanganyika)
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana, Mzee wetu tunamsitiri UNGUJA, ZANZIBAR.Mzee wetu azikwe mahali pachimbuko lake (Tanganyika)
Mzee wetu asili yake ni Tanganyika...Tanganyika ipewe ndugu yaoHapana, Mzee wetu tunamsitiri UNGUJA, ZANZIBAR.
💔Tuliopitia miezi 18 ya kufunga mkanda tunamshukuru sana Rais Ali Hassan Mwinyi kwa kufungua uchumi na kuruhusu bidhaa kuingia nchini, tukaondoka katika dhiki ya mwendo wa kuruka, ulanguzi na habari za mikingamo.
Tukaondoka katika dhiki ya kukimbizana na magari ya ugawaji, dhiki ya kulazimishwa kununua unga wa muhogo ili kununua sukari, dhiki ya kuvaa nguo zilizochanika.
Dhikibya kunua bidhaa duka la CCM kwa kuandikiwa kwenye kidaftari cha ration kama tuko vitani.
RIP Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Kwani Mpoto anayeimba ni Mkristo au Myunani??Nyimbo kwenye msiba wa kiislam?
Kama ulivyosikiaNataka kujua uhusiano wa kizimkazi na Mwinyi
Kumbuka pia umri wake wakati huo hata mwalimu Nyerere mwisho mwisho alikua na kauli zenye utataR.I.P Mzee Mwinyi, poleni Wafiwa
Mzee Mwinyi katika uongozi wake ana sura nyingi
1. Mema:
a. Aliivusha nchi kwa amani kutoka Ujamaa hadi mrengo tulio nao usio na jina.
b.Alifungua utandawazi na biashara huria, pamoja na mapungufu alituvusha kwa salama
c. Alituvusha kipindi cha mpito kutoka Chama kimoja hadi vyama Vingi
d. Alikuwa mvumulivu sana, hata alipokirihika hakukimbilia dola kuumiza wenzake
e. Ni Mwanamapinduzi huko visiwani.
2. Mapungufu
Kitendo cha kusimama na kutaka Katiba aliyoapa kuilinda na aliyoitumikia kwa miaka 10 ibadilishwe ili Mafufuli aendelee bila ukomo ilikuwa doa kubwa sana. Alifanya hivyo ili mwanae ateuliwe na si kwa masilahi ya nchi.
Kwa hili alivuruga sana heshima yake aliyoijenga kwa miaka mingi
JokaKuu Pascal Mayalla
Innaa milkullah yataswarrafu fiinaa kayfa yashaauRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan;
"Ndugu wananchi, kwa majonzi makubwa nasikitika kutangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, ambaye amefariki dunia leo Alhamisi tarehe 29 Februari mwaka 2024 saa 11:30 jioni, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.
Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu. Nchi yetu itakuwa katika kipindi cha siku saba za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia kesho Machi 1, 2024. Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi atazikwa tarehe 2 Machi 2024 huko Unguja, kisiwani Zanzibar."
Inna Lillahi wa inna ilayhi raaji’un.
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.
Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.
Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.
View attachment 2920484
Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua
Huyu mpe, huyu mruke.MSIBA MZITO Kwa Taifa.
Rais Mstaafu wa JMT.
Baba mzazi wa M.Kiti wa Baraza la Mapinduzi.
Mkuu wa chuo bora cha Afya Tanzania (Muhimbili).
Siku ya kukumbuka kifo chake itakuwa kila baada ya miaka minne ... (Miaka yenye mwezi wa pili wenye siku 29 tu)
View attachment 2920492
Hii picha ili trend kipindi cha msiba wa Rais John Pombe.