TANZIA Rais wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia
Kiukweli Demokrasia ya Vyama Vingi ilijengwa na Mzee Mwinyi japo baadae waliomfatia waliichakachua

Hapa Iringa tulipata Mbunge wa NCCR mageuzi Mwalimu wangu Kibasa

Wewe utamkumbuka kwa lipi?

Mungu wa mbinguni mrehemu Mzee Mwinyi
Kumbe umesoma Mwembetogwa....Kuna toto moja la kiburushi mashallah lilikuwa linakaa wilolesi...miaka hiyo.
 
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.

Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.

View attachment 2920484

Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua
"Mwinyi was born on 8 May 1925 in the village of Kivure, Pwani Region, where he was also raised.[4] He then moved to Zanzibar and got his primary education at Mangapwani Primary School in Mangapwani, Zanzibar West Region. Mwinyi then attended Mikindani Dole Secondary School in Dole, Zanzibar West Region.[5] From 1945 to 1964 he worked successively as a tutor, teacher, and head teacher at various schools before deciding to enter national politics".
 
Mtu wa kwanza kuuza wanyama pori hai uarabuni
Rais wa kwanza kukuruhusu kupoza maji kwny fridge bila ya hofu ya kuonekana kabaila wala Mhujumu Uchumi

Huyu ndie binadamu wa kwanza kuamuru kuondoa marufuku ya Watanzania kutembelea Nchi kadhaa ambazo hapo awali zilipigwa marufuku kwny hati za kusafiria kwa sababu za kihafidhina
 
Mzee Mwinyi alikuwa ni Rafiki wa Watu Wote hivyo Watu waachwe wakamzike pasiwepo CHAWA vimbelembele waliojaa Unafiki

Tunategemea Kaswida ziwepo na Siyo hawa Wasanii wetu wa Kampeni

RIP mzee Rukhsa
Mzee wetu azikwe mahali pachimbuko lake (Tanganyika)
 
Wa
MSIBA MZITO Kwa Taifa.
Rais Mstaafu wa JMT.
Baba mzazi wa M.Kiti wa Baraza la Mapinduzi.
Mkuu wa chuo bora cha Afya Tanzania (Muhimbili).

Siku ya kukumbuka kifo chake itakuwa kila baada ya miaka minne ... (Miaka yenye mwezi wa pili wenye siku 29 tu)
View attachment 2920492

Hii picha ili trend kipindi cha msiba wa Rais John Pombe.
Wamejichanganya kuchelewesha kuutangaza, ndicho kitatokea hicho 😌
 
Daah R.I.P kwake kaula sana miaka 100 sio mchezo..

pumzika kwa amani rais mstaafu ali hassan mwinyi dunia itakukumbuka kwa kuibadilisha Tanzania kutoka kwenye mfumo wa ujamaa na kujitegemea hadi mfumo wa ubepari.

Ni wewe ndio uliye ifanya Tanzania ikakua kiuchumi mpaka sasa ilipo bila maono yako Tanzania isingekuwa hivi

Nb.rais mwinyi alizaliwa mkurang, pwani Tanganyika mwaka 1924 na amefariki leo tarehe 29/2/2024


R.i.p
 
Back
Top Bottom