tunamuombea rehema kwa Mungu na kumtakia pumziko la milele lenye amani, sote ni wamwenyezi Mungu kwa vile tulitoka kwake na tututarejea kwake wakati fulani.

shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa maisha ya All hasani mwinyi, huduma yake katika jamii na familia yake, haswa pia nafasi aliyo mjalilia ya urais wa Tanzania, kama taifa tumebakiwa na kumbukumbu nzuri za uongozi na utumishi wake katika serikali ambao kwao taifa limepata faida fulani kwa vizazi vilivyokuwepo na sisi tuliopo leo na hao wanaotuandama.
 
Tuliopitia miezi 18 ya kufunga mkanda tunamshukuru sana Rais Ali Hassan Mwinyi kwa kufungua uchumi na kuruhusu bidhaa kuingia nchini, tukaondoka katika dhiki ya mwendo wa kuruka, ulanguzi na habari za mikingamo.

Tukaondoka katika dhiki ya kukimbizana na magari ya ugawaji, dhiki ya kulazimishwa kununua unga wa muhogo ili kununua sukari, dhiki ya kuvaa nguo zilizochanika.

Dhiki ya kunua bidhaa duka la CCM kwa kuandikiwa kwenye kidaftari cha ration kama tuko vitani.

RIP Mzee Ali Hassan Mwinyi.
 
Nitamkumbuka kwa statement zake na kutokuwa mbaguzi wa kiimani

Alisimama jukwaani akasema, "anayetaka kula chura na ale asiwepo mtu wa kumpangia ale nini na akiwa wapi"
Alisimama jukwaani akasema "gonjwa hili limeingia pahala pale ambapo sote wakubwa na wadogo twapapenda"
Alikuwa ndiye mlezi wa Baraza la huduma za jamii la kikristo CSSC
 
💔
 
R.I.P Mzee Mwinyi, poleni Wafiwa

Mzee Mwinyi katika uongozi wake ana sura nyingi
1. Mema:
a. Aliivusha nchi kwa amani kutoka Ujamaa hadi mrengo tulio nao usio na jina.
b.Alifungua utandawazi na biashara huria, pamoja na mapungufu alituvusha kwa salama
c. Alituvusha kipindi cha mpito kutoka Chama kimoja hadi vyama Vingi
d. Alikuwa mvumulivu sana, hata alipokirihika hakukimbilia dola kuumiza wenzake
e. Ni Mwanamapinduzi huko visiwani.

2. Mapungufu
Kitendo cha kusimama na kutaka Katiba aliyoapa kuilinda na aliyoitumikia kwa miaka 10 ibadilishwe ili Magufuli aendelee bila ukomo ilikuwa doa kubwa sana. Alifanya hivyo ili mwanae ateuliwe na si kwa masilahi ya nchi.
Kwa hili alivuruga sana heshima yake aliyoijenga kwa miaka mingi

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Mwenyezi Mungu amrehehemu na kumpa pumzi la milele. Tukikumbuka sana alikuwa ni mtu sahihi kabisa kulipokea Taifa toka kwa Baba wa Taifa na kutuvusha salama kuelekea mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini baada ya kuanguka kwa Urusi na kuvunjwa kwa mfumo wa kikaburu Afrika ya Kusini. Taifa lilibarikiwa sana kuwa naye licha ya changamoto zilizomkuta kiuongozi. Mzee ruksa nwenye misemo mingi ya Kiswahili apumzike kwa Amani Amina. Inna illahi wa inna lillahi rajioun.
 
Kumbuka pia umri wake wakati huo hata mwalimu Nyerere mwisho mwisho alikua na kauli zenye utata
 
Tupate wadhamini kidogo [emoji95][emoji95][emoji95][emoji95][emoji95][emoji95]
 
Innaa milkullah yataswarrafu fiinaa kayfa yashaau
 
Huyu mpe, huyu mruke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…