TANZIA Rais wa awamu ya pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia
View attachment 2920756

Hii ndio Taarifa ya Serikali iliyosambazwa kwa vyombo vya habari usiku huu, Kwamba Mzee huyu ataagwa na Wananchi wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru tarehe 1/3/2024, kabla ya kusafirishwa kuelekea kwao Zanzibar kwa Mazishi yaliyopangwa kufanyika Tarehe 2 March.

Apumzike kwa Amani
Mpaka hapo sijaona ratiba naona taarifa
 
Ana siku nying ameondoka mzee wetu, nadhani ndo taratibu kutangaza baada ya muda kupita huku wakiweka mambo sawa.
Hakuna kitu kama hicho !
Kwani wafiche nini ?
Yeye hakuwa sitting President !
Huwa zinacheleweshwa habari za vifo vya Sitting Head of States kwa sababu za kiusalama !
Lakini kwa mstaafu huwa hakuna kuficha kitu. !!
Kwa sababu huwa hakuna sababu zozote za kiusalama !!
Na kwa Mwislamu hata hiyo protokali itafanyika kwa kuzingatia sheria za dini ambazo haziruhusu marehemu kuwekwa muda mrefu bila kuzikwa !

Ndio maana unaona imeshatangazwa kwamba mzee wetu atazikwa tarehe 2 march 2024 !!
 
View attachment 2920756

Hii ndio Taarifa ya Serikali iliyosambazwa kwa vyombo vya habari usiku huu, Kwamba Mzee huyu ataagwa na Wananchi wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru tarehe 1/3/2024, kabla ya kusafirishwa kuelekea kwao Zanzibar kwa Mazishi yaliyopangwa kufanyika Tarehe 2 March.

Apumzike kwa Amani
Kwa hiyo walichelewa kutangaza kifo chake mpaka muafaka uliopatikana juu ya kuzikwa jati ya chaguo lake Mkulanga ña la Hussein
 
Walisema mzee aliacha wosia wake kuwa azikwe kwao Mkuranga; imekuwaje watoto wamedharau matakwa ya marehemu?
Kuna athari gani kwa familia wanapokiuka matakwa ya marehemu kama yalivyoainishwa kwenye wasia wake?
Kwao ni zanzibar !
Huko Mkuranga labda ni kwa Babu na Mababu waliopita. !

Kama vile Obama huwezi ukasema kwao ni Kogelo Kisumu Kenya !

Kule Kogelo ni kwa Baba yake na Babu Zake !
Hata sisi hapa Tanganyika ni wahamiaji tu kutoka sehemu mbali mbali za Bara hili na Dunia hii. !
🙏🙏
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan;

"Ndugu wananchi, kwa majonzi makubwa nasikitika kutangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, ambaye amefariki dunia leo Alhamisi tarehe 29 Februari mwaka 2024 saa 11:30 jioni, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu. Nchi yetu itakuwa katika kipindi cha siku saba za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia kesho Machi 1, 2024. Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi atazikwa tarehe 2 Machi 2024 huko Unguja, kisiwani Zanzibar."

Inna Lillahi wa inna ilayhi raaji’un.
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.

Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.

View attachment 2920484

Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua
Enyi majizi, matapeli na mafisadi ya Mali za umma, maisha ya mwanadamu ni hadithi tu. Pumzika mwinyi.
 
MSIBA MZITO Kwa Taifa.
Rais Mstaafu wa JMT.
Baba mzazi wa M.Kiti wa Baraza la Mapinduzi.
Mkuu wa chuo bora cha Afya Tanzania (Muhimbili).

Siku ya kukumbuka kifo chake itakuwa kila baada ya miaka minne ... (Miaka yenye mwezi wa pili wenye siku 29 tu)
View attachment 2920492

Hii picha ili trend kipindi cha msiba wa Rais John Pombe.
MHSRIEP 🙏🏼
 
Hakuna kitu kama hicho !
Kwani wafiche nini ?
Yeye hakuwa sitting President !
Huwa zinacheleweshwa habari za vifo vya Sitting Head of States kwa sababu za kiusalama !
Lakini kwa mstaafu huwa hakuna kuficha kitu. !!
Kwa sababu huwa hakuna sababu zozote za kiusalama !!
Na kwa Mwislamu hata hiyo protokali itafanyika kwa kuzingatia sheria za dini ambazo haziruhusu marehemu kuwekwa muda mrefu bila kuzikwa !

Ndio maana unaona imeshatangazwa kwamba mzee wetu atazikwa tarehe 2 march 2024 !!
Katika vitu ambavyo dola ipo makini sana ni kuepusha taharuki

oamoja na maisha ya faragha ya Mzee Mwinyi lakini walipogundua safari inakaribia ilibidi watangaze Mzee anaumwa na tunaomba Mumuombee

hii ilikuwa ni kuliweka Taifa Mkuu sawa na ndio sababu taarifa hii tumepokea kwa masikitiko ila sio kwa Mstuko mkubwa

ilifanyika hivyo kwa Kambrage na kwa Magufuli japo kwa style tofauti

kwa Mzee Mkapa haikuwezekana kwa kuwa ilikuwa ghafla sana na Mwamba JPM hakuamini sana hizo protocol
 
Walisema mzee aliacha wosia wake kuwa azikwe kwao Mkuranga; imekuwaje watoto wamedharau matakwa ya marehemu?
Kuna athari gani kwa familia wanapokiuka matakwa ya marehemu kama yalivyoainishwa kwenye wasia wake?
MWINYI sio mzanzibar ni wa mkuranga kumzika zanzibar ni kumlazimisha aonekane ni mzanzibar na pia mwanae ambaye ni rais kule aonekane ni mzanzibar shida yote ni Magufuli kumpa hussein urais
 
Back
Top Bottom