Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan;
"Ndugu wananchi, kwa majonzi makubwa nasikitika kutangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, ambaye amefariki dunia leo Alhamisi tarehe 29 Februari mwaka 2024 saa 11:30 jioni, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.
Kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu. Nchi yetu itakuwa katika kipindi cha siku saba za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia kesho Machi 1, 2024. Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi atazikwa tarehe 2 Machi 2024 huko Unguja, kisiwani Zanzibar."
Inna Lillahi wa inna ilayhi raaji’un.
Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki leo, Februari 29, 2024 saa 11:30 Jioni katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.
Tangu Novemba 2023, alikuwa anapatiwa matibabu huko London, Uingereza na baadaye kurejeshwa nchini kuendelea na Matibabu katika hospitali ya Mzena hadi leo ambapo amepatwa na mauti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo kuanzia Machi 1, 2024, bendera zitapepea nusu mlingoti.
Atazikwa Machi 2, 2024 Unguja, Zanzibar.
View attachment 2920484
Taarifa za kuugua kwake, soma: Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua