Rayvanny ampost mpenzi wake Paula wa Kajala wakila bata

Waandishi wa makala na maisha walohitimisha kwamba kuna vitu vitatu maishani hutakiwi kuviweka hadharani

1. Mahusiano/Mapenzi yako

2. Uchumi wako

3. Malengo yako (Next Movie)
 
Mama yake ni mlokole, alisema hawezi kukubali kupokea na kutumia hela ya mtoto wake sababu kazi na mazingira yanayompatia hiyo hela hakubaliani navyo na ni kinyume cha imani yake. Hivyo akasema ataendelea kujitafutia kipato kwa kuendelea kuuza mboga za mafungu, ingawa mtoto wake hapendi.
 
Mama anaitafta mbingu Kwa juhudi zote , kongole kwake
 
Umegusia 20%???
Basi tu.
 
Sina wivu, lakini Paula demu wa kawaida kinoma.
 
Hayo magari amepiga tu picha. Naishi nae jirani hana gari kama hizo.

Hata Davido ukute nae kapiga tu picha. Umaarufu ni upuuzi sana. Marehemu Ruge kafa akiwa anaishi apartment ya chumba na sebule na tuliaminishwa anawanyonya wasanii.
Tuweke ushabiki pembeni, Ruge alikuwa anashindwa kujenga nyumba....!!! Huwa mnawadharau Sana watu maarufu na hii ni Kwa Tanzania Tu...!! Ukiwa maarufu the rest waliobaki ni kukuchawia
 
Tuweke ushabiki pembeni, Ruge alikuwa anashindwa kujenga nyumba....!!! Huwa mnawadharau Sana watu maarufu na hii ni Kwa Tanzania Tu...!! Ukiwa maarufu the rest waliobaki ni kukuchawia
Uwezo alikuwa nao ila hakujenga mpaka anakufa. Wala sina dharau kwa mtu maarufu bali kwa nchi yetu uwa wanajisahau sana. Mwisho wa Ruge haukuwa mzuri hata kidogo nakumbuka mpaka tulipitishiwa bakuli la michango siku za mwisho.

Mimi binafsi sina wivu na mtu yoyote ila nachukia watu wanaopata nafasi lakini wanazichezea kwa kuendekeza anasa kama hawa wasanii wa sasa. Mbona kuna wanaofanya vizuri na kuwekeza kama kina Sugu, H. Baba, P. Funky, Master Jay, n.k

Ukweli usemwe ili wajifunze pia kupata hela umri mdogo ni tatizo inabidi uwe na adabu sana ya maisha ndio utoboe. Wasanii na watu maarufu upande wa burudani majority wana mwisho mbovu sana
 
Tuweke ushabiki pembeni, Ruge alikuwa anashindwa kujenga nyumba....!!! Huwa mnawadharau Sana watu maarufu na hii ni Kwa Tanzania Tu...!! Ukiwa maarufu the rest waliobaki ni kukuchawia
Pia hilo la kujenga nyumba ni tatizo sana kwa watu. Wanakuwa na uwezo ila wanajisahau mwisho wake uwezo ukiisha wanadharaulika. Ruge ni mfano mzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…