RC Adam Malima ashauri Serikali kuwa makini kwenye Mkataba wa DP World, ili tusipigwe kama kwenye Mikataba ya Madini

Hapa kwenye suala la DPW hakuna cha collective responsibility bali kuna kuburuzana! Serikali haikutoa muda wa kutosha kujadili makubaliano hayo kama inavyoyaita ingawa sisi tunajua ni mkataba.
 
Wewe kilikuzuia nini kutoa maoni kama ya Malima hapo mwanzo?
 
Waandishi wa habari siku hizi wamekuwa ni mawakala wa matangazo, kwenye "bahasha" kubwa ndiko wanakoelemea.
 
He is old school
...katika suala la makubaliano ya bandari wengi tumejua mia zao mbovu, hasa wanao utetea. Hili lina mstari mwekundu wa wanaipenda Tanganyika bila vyeo, utajiri, nasaba na husuda na wale wenye nia hasi na Tanganyika. Je huyo old school yupo upande gani? Halafu wasio werevu huzeeka pia. You can be old school of fools.
 
..Adam amempiga kijembe Maza ambaye wajomba zake ni Waarabu wa Oman.
Tanganyika haikuhitaji kero 24 za muungano. Ilihitaji mikataba mibovu tu ijitenge. Huu ni mwanzo. Ngoja tuone mwisho wa haya utaleta matokeo gani.
 
Sikujua kama huko chama pendwa bado wako watu wenye akili. Hongera RC kwa kusema kweli. Mungu akulinde
 
Eti waarabu wajomba zake..si akaishi nao sasa..tuacheni rasilimali zetu hatavizazi vyetu vitatakuja kusahihisha pale mlipo shindwa
Wewe mpuuzi na mjinga na kumbe una chuki za kidini na sio kukosa.
Malima amesema waarabu SIO wajomba. Akimaanisha tusiwaamini kupita kiasi. Mpuuzi wewe unaamua kupotosha kwamba kasema wajomba zetu?
 
Mkataba bado jamani, muelezwe vipi? Labda hamuelewi kuwa kuna kampuni tatu mpaka sasa zinagombania bandari ya Dar. Sasa nyinyi kuona Mkubaliano ya serikali ya Dubai na Tanzania, mkachukulia, ooh tayri. Hapana, mkataba bado una michaakato yake.
Wewe ajuza hakika umechanganyikiwa, hujui kwamba hujui na ndio maana unatumika kama tambara la kudekia sakafu. Hebu msome huyu mbunge anasemaje...

(nanukuu) Wabunge wa CCM tuliopitisha Mkataba wa Uwekezaji Bandarini tuko vizuri kichwani, pale Bungeni kuna wabunge wa CCM wako vizuri kichwani.

Mimi mwenyewe nimemaliza chuo Mzumbe wakaning'ang'ania nibaki kufundisha pale kwa sababu nina akili nyingi, nilipata GPA ya juu sana.

Kwa hiyo hatukupitisha mkataba bila kuusoma, na tusingezeweza kupitisha mkataba usio na maslahi kwa nchi yetu.
(mwisho wa nukuu)

By Elibariki Kingu

Kabla mkataba huo wa siri haujavuja, neno lililotumika ni mkataba. Baada ya wananchi wazalendo kuupigia kelele, kama ilivyo kawaida ya CCM wakaja na maneno mara azimio, mara makubaliano, mara hatua za awali na mauupuzi upuzi yote

Mkataba uliingiwa zaidi ya mwaka nyuma Rais alipotia sahihi yake.
 
This guy is smart! Ngoja tuone kama SSH atamtumbua! Na wale mawaziri, MaRC, Ma DC, MARAS, MADAS etc wanajitia uchawa katika mamlaka yao nao waondoe funza vichwani! Ahsante Comrade Malima kuna kiroboto mmoja DAS wa Busega anawashwa kuhitaji damu ajifunze haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…