RC Makonda aandaa sherehe Arusha. Anatarajiwa kuchinja ng'ombe 200

RC Makonda aandaa sherehe Arusha. Anatarajiwa kuchinja ng'ombe 200

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ng’ombe takribani 200 watatolewa kwa ajili ya kuchoma nyama, tukio linalolenga kuimarisha uhusiano kati ya wafanyabiashara wa mkoa huo na viongozi wanaoshiriki kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.

“Ng’ombe kama 200 hivi watachinjwa, ni kuchoma nyama tu hakuna ugali wala wali, lakini tumewaita wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Arusha” amesema Makonda

Ametangaza kufanyika kwa sherehe ndogo Agosti 29, 2024 kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Arusha na Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.
Vipi Mbunge atakuwepo?
 
Nimeangalia comment sisi wa TZ bado sana. Juzi Arusha kulikua na maandamano watu hawana maji, wamasai bado wana maswali yao hawana majibu.. leo tunafanya sherehe. Aisee
 
Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.....

Arusha ina matajiri wengi....

Sadaka na zaka si tu huko misikitini na makanisani....

Kulitunza dola letu kunahitaji SADAKA NA ZAKA za MALI na UHAI WETU...

Mh.Makonda analifahamu hilo fika[emoji7][emoji7]

#Nchi Kwanza[emoji7]
Kwa hiyo 👆 hapo wanafanya kafara ya Amani, Daa poor brain kabisa
 
Kama hawatoi Kuponi getini nami nitaenda kula hizo nyama Choma

Ikiwezekana waweke na Muziki kabisa tukeshe tukifurahia Rc wetu kwenda kugombea Ubunge
Babu ulienda kuchungulia kwenye chungu, ukaona , maana 2025 chochote kinaweza kutokea,
 
ng'ombe mmoja analiwa watu 400.

ng'ombe 200 zitaliwa na watu elfu 80.

Hapo tunahitaji gunia karibu 30 za mkaa kwa ajili ya hili zoezi.
 
Kuna vitu viwekwe sawa kwa ajili ya hii sherehe kusije kufanyika janja janja watu wakadhurika
 
Babu ulienda kuchungulia kwenye chungu, ukaona , maana 2025 chochote kinaweza kutokea,
Hahaha...............huyo ndiye Mkuu, tujiandae kumpisha kwenye msafara wa kuongozwa na ving'ora Kila Mkoa
 
Nadhani itakuwa Choma festival, maana Kwa ng'ombe 200 nyama yake sio ya mchezo
Unashangaa 200, rizi1. Alichinga1,500 kwenye idi ya kuchinga mkwa huu, almost kila kaya kwenye Jimbo lake ilipata Kilo 5 AU 6.

Babu watu wako na pesa
 
Unashangaa 200, rizi1. Alichinga1,500 kwenye idi ya kuchinga mkwa huu, almost kila kaya kwenye Jimbo lake ilipata Kilo 5 AU 6.

Babu watu wako na pesa
Hahaha.............ndiyo maana Nchi ipo Uchumi wa Kati, Kila mtu analamba asali
 
Hii itasaidia kidogo kushutua tumbo, maana ugali ,makande, na mtindi ndio mtindo wa maisha chuga
 
Hela za kufanya ujinga zipo na mnazo zinatoka chap chap. Kutulipa wazabuni na kuwalipa wakandalasi hapo ni kazi sanaa.

Si ajabu ukakuta Mkurugezi hajalipa mafundi wanaojenga madarasa.😂😂
Hyo inaitwa resources mobilisation skill sio lazma pesa siwe zake amaweza akamobilize wafugaji na wafanya biashara ya nyama wakafanya kwa faida yao.
 
Back
Top Bottom