RC Mtaka ataja makabila 5 yanayokuza Uchumi wa Sekta Binafsi Tanzania

RC Mtaka ataja makabila 5 yanayokuza Uchumi wa Sekta Binafsi Tanzania

Mjinga kabisa huyu bwana, anazungumza habari za ukabira karne ya 21,!? Huyu bwana anapenda sifa sana , enzi hizo akiwa rc simiyu alitutesa sana walimu, alijaribu kuupeleka ujinga wake dodoma wakampinga.
Hajazungumza kuhusu ukabira amezungumza kuhusu ukabila!
 
angesema makabila yanayojihusisha na uuzaji bidhaa reja reja na jumla./ Kuuza maduka ya bidhaa.
Akishasema inasaidia nini kwenye uchumi wa Taifa hili?? Dhambi ya ukabila ni mbaya sana, tujifunze athari za ukabila kutoka kwa majirani zetu wa Kenya.
 
Ila mnatukosea sana Wanyantuzu ndo wasukuma haswa! Hapo wasukuma wa geita na maeneo mengine ni mchanganyiko sana! Ntuzu ndo sukuma Org! Wanyantuzu kwa wasukuma ni kama Warombo kwa wachaga!
Unaona athari ya ukabila?? Mtabaguana wenyewe kwa wenyewe tena. Achaneni na upumbavu wa kuwaza makabila
 
Kwa sasa wanaongoza WAKINGA kwa kuwa na pesa ndefu na biashara kubwa. Siyo wachaga. Wakinga wana nidhamu kubwa sana ya kutunza pesa. Kariakoo wanaitawala. Sasa wameanza kuwekeza kwa kasi kubwa sana DODOMA.
 
Mnyantuzu ni Msukuma fullstop! Aache ujinga! Anafikri uchumi unajengwa na biashara tu? Vipi kuhusu Kilimo kinachofanywa na Wasukuma?
 
Makabila ya Kiuchumi au ya kitajiri Kwa Mujibu wa Mtaka

Wachaga
Wakinga
Wapemba
Waha
Wanyantuzu.

My Take
Kama kabila lako halipo kwenye List jihesabu wewe ni Maskini tu.
---

MAKABILA 5 MUHIMU ZAIDI UKUAJI SEKTA BINAFSI TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesesma kuna jamii 5 muhimu zinazochangamsha ukuaji wa sekta binafsi, uchumi wa nchi na biashara kiujumla, huku akizitaja jamii hizo kuwa ni; Watu kutoka Kilimanjaro, Wakinga, Waha, Wapemba na Wanyantuzu.

RC Mtaka ameyazungumza hayo katika mahojiano maalum na Charles William kuhusu hali ya uwekezaji, biashara na kilimo katika mkoa wa Njombe.

Wasafi Media
Haya mambo ya makabila yanatoka wapi tena? Ni aibu kwa kiongozi wa kitaifa kuanza kuelezea jambo lo lote kwa kuunganisha na kabila la mhusika. Mfano mzuri ni wa jiji la Dar ambalo linachangia vikubwa kwenye mapato ya serekali. Kwa kuwa wenyeji wa lilipo jiji ni Wazaramo, basi tuseme Wazaramo wanachangia vikubwa kwenye serekali? Tuachane na ukabila kuendeleza umoja wa nchi.
 
Wewe huna kabila? Mbona mapovu sana? Tofautisha kuzungumzia makabila na kuzungumzia ukabila.
 
Mda mwingine kama kiongozi kukaa kimya husaidia kuficha upande wa pili wa ujinga wake
 
Makabila ya Kiuchumi au ya kitajiri Kwa Mujibu wa Mtaka

Wachaga
Wakinga
Wapemba
Waha
Wanyantuzu.

My Take
Kama kabila lako halipo kwenye List jihesabu wewe ni Maskini tu.
---

MAKABILA 5 MUHIMU ZAIDI UKUAJI SEKTA BINAFSI TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesesma kuna jamii 5 muhimu zinazochangamsha ukuaji wa sekta binafsi, uchumi wa nchi na biashara kiujumla, huku akizitaja jamii hizo kuwa ni; Watu kutoka Kilimanjaro, Wakinga, Waha, Wapemba na Wanyantuzu.

RC Mtaka ameyazungumza hayo katika mahojiano maalum na Charles William kuhusu hali ya uwekezaji, biashara na kilimo katika mkoa wa Njombe.

Wasafi Media
mbona kigoma iko katika top three ya mikoa maskini Tanzania?
 
Kigoma kama.mkoa ila.sio watu wake.

Kwani hujui ilikuwa imetengwa Kwa miundombinu ya Kiuchumi na Kijamii Kwa miaka na mikaka isipokuwa recently ndio imeanza kufunguliwa?
kwamba rukwa (ambayo haikuwa na barabara ya lami na haifikiki hata kwa reli) na haiko katika top 3 za umaskini yenyewe haikuwa imetengwa? Vipi kuhusu katavi? Tabora ambayo nayo ni hohe hahe nayo ilitengwa ilhali reli ilikatisha hapo na ni kituo kikuu cha treni nchi hii, hata waha madeal yote lazima wakatishe tabora kwa reli....

Hulka ya jamii za watu wanaoishi mkoa husika ndiyo husababisha. Waha ni wafanyabiashara-umachinga nk, lakini kwenye kilimo ni wavivu....kama wahaya ambao nao kagera iko top three, wasomi lakini wavivu wa kazi, wamekalia porojo na majigambo tu kwa kuwa wana mashamba ya urithi ya migomba
 
kwamba rukwa (ambayo haikuwa na barabara ya lami na haifikiki hata kwa reli) na haiko katika top 3 za umaskini yenyewe haikuwa imetengwa? Vipi kuhusu katavi? Tabora ambayo nayo ni hohe hahe nayo ilitengwa ilhali reli ilikatisha hapo na ni kituo kikuu cha treni nchi hii, hata waha madeal yote lazima wakatishe tabora kwa reli....

Hulka ya jamii za watu wanaoishi mkoa husika ndiyo husababisha. Waha ni wafanyabiashara-umachinga nk, lakini kwenye kilimo ni wavivu....kama wahaya ambao nao kagera iko top three, wasomi lakini wavivu wa kazi, wamekalia porojo na majigambo tu kwa kuwa na mashamba ya urithi ya migomba
Rukwa Barabara ya lami imefika Toka 2013 wakati Kigoma Hadi Leo hii hakuna Barabara ya lami hata Moja inayounganisha na Mkoa wa jirani achilia mbali umeme wa grid ya Taifa.

Narudia kukwambia Kigoma ilicheleweshwa tuu ila kufikia 2025 hutoikuta huko kwenye hiyo list maana Kasi ya kuifungua ni kubwa sana.
 
rukwa ipi ilipata lami 2013 wewe? mimi natoka rukwa, hatunaga porojo za kijinga. 2013 ndipo lami ilianza kujengwa. Kigoma mlikuwa na advantage ya reli kwa usafirishaji wa kila kitu, lakini kwa sababu ya uvivu hamkuwa na bidhaa yo yote ya kilimo ya kusafirisha ili iwaondolee umaskini zaidi ya vichupa vya mawese kwenye mabegi.

Kama ni umeme rukwa mpaka leo haiko kwenye gridi ya taifa, hata ukimuuliza waziri atakwambia bado hakuna mpango wa kuunganisha rukwa kwenye gridi ya taifa kwa sasa. Tofauti ya rukwa na mikoa mingi nchi hii, wakazi wa rukwa walitengwa kwa dhana ya kuwa ni wachawi nao wakajua wametengwa hivyo tangu uhuru hujitafutia maendeleo wao wenyewe kimya kimya. Ndiyo sababu rukwa hata hali ya hewa iwe mbaya vipi huwezi ukasikia watu wanaililia serikali iwasaidie. Ni nadra sana.

Na ni mahali pekee Tanzania huwezi ukaona ombaomba mitaani, kila mtu anawajibika kwa maisha yake binafsi na ya familia na ukoo wake. mwisho wa siku wakusanya takwimu wakifanya tafiti zao wanakuta hakuna umaskini wa kutupwa kama mikoa mingine.
 
Kigoma kama.mkoa ila.sio watu wake.

Kwani hujui ilikuwa imetengwa Kwa miundombinu ya Kiuchumi na Kijamii Kwa miaka na mikaka isipokuwa recently ndio imeanza kufunguliwa?

Kweli wanyonge wanyongeni haki yao muwape, waha ni wapambanaji na kwa sasa hata shule waha wamesoma sana na ujasiliamali wanajitahidi nadhani mazingira yao magumu yaliwafanya automatically kupambana
 
Back
Top Bottom