Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 11,074
- 20,608
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Halafu eti huyu asifukuzwe shule wakati anauzaa madawa ya kulevya na kifungo chake ni miaka kadhaaDogo Rajabu wa kigogo sekondari yeye breaktime anauzia wenzake bangi
Halafu eti wasifukuzwe shule. Yaani. Shule ipoteze rasilimali na miundombinu kusomesha majizi ambayo yataishia kupata Zero. Di Bora waishie tu la Saba?Loooh Igogo,Mwanza napaelewa sana. Hapo ndo base kuu ya wezi,vibaka na majambazi wa jijini Mwanza. Watoto wa hapo wamepinda kinoma, we chiembe nenda huko ukajionee.
Bora akajifiche maana leo ni mwana kulitafuta ni mwana kulipata. Sijui amewazaje kumgusa Mtaka. Naona ana test zali la kidole kwenye uji wa volcano.Waungwana wamemfukuza mwenye uzi kwa uzi wake haha
Sahihisha hapo kwa Single mother's. Huwezi kuniambia watoto wote watukutu wanalelewa na Single mothers. Wapo Single mothers strong Sana kuliko Sisi wanaume na wame produce vidume na wasichana imara mno kila sekta. Ziko nyumba zina wazazi wote lakini watoto wameishia kuwa hovyo. Ungefanya utafiti ndiyo ufanye hii painful attach hata kwa dada na mama zetu humu ambao wako imara mno kimalezi. Ninafahamu single mothers kadhaa ambao watoto wao ni mfano Bora mno. Tena form four wanatoka na single digits na nidhamu mtaani ni perfect mpaka na admire mkuu. Poleni Single mother.We ndugu chiembe umesoma comments zilizofuatia andiko lako na umejifunza nini hapo?.
Usiweke au kuandika kwa usuda za kisiasa, kidini nk, kisa kiongozi fulani ni mtu fulani au katokana na mazingira fulani, hiyo ni mbaya sana ndg Mtanganyika.
Kwanza sheria za kufukuza shule mtoto nunda zipo na labda kama huna mtoto nakushauri nenda shule ya jirani kaongee na mwalimu mkuu umuulize je, mtoto anafukuzwa shule kwa kosa gani? -Alafu njoo hapa urekebishe mada yako.
Na watoto hawa wa kizazi kipya wanaolelewa na single parent unataka adekezwe wala asipewe onyo kali la kufukuzwa skuli unadhani kutakuwa na nidhamu hapo?.
Next time angalia logic yako na isimame na uhalisia wa maisha kulingana na matukio, siyo unamuingiza mfu kwenye scenerial isiyomuhusu, -Pole.
Nakuunga mkono mkuuNamuunga mkono Mtaka 100% kwa 100%.
P
Ndio hivyo mkuu. Asiefunzwa vizuri na ***** mwalimu hatomuwezaSasa wakipigwa wanakufa wawafanyeje. Tulishakubaliana enforcing discipline ni kazi ya mzazi. Mwalimu ni kufundisha. Mtoto asiye na nidhamu arudishwe kwa mzazi.
Wakifukuzwa wakija mtaani wauze ngadu mahakama itawaonesha chimbo linalowafaaHALAFU WAKIMKUFUKUZA ITAKUWAJE?
Ukiacha kuwa Mwanafunzi actual experience yako katika uemdeshaji au taratubu za Shule na upi? Tuanzie hapo kwanza ili tuende vyema katika huu mjadala kwa Nia njema tu ya kujengaJe kama angefukuzwa shule asingekuwa jambazi? Yoyote anaye-support watoto watukutu wafukuzwe shule ni juha na hana akili timamu.
Government Kuna watu wenye akili Kama za mtoa mada, ndiko watoto wao wanakosoma (community schools) kwamba Mambo yaende hobela hobela na ndio maana hata products za hizo Shule kwa Sasa haziaminiki tofauti na zamaniHivi mbona shule za private hazina mitoto ya ajabuajabu kama gov
Yupo sahihi 100% . Kuliko kupambana nao Kwa viboko mwishowe uwaue bure.Mtaka ni kama ana serikali yake ambayo haiendani na ya CCM na Samia, hivi mtoto unamfukuza shule ili iweje? Kwanza ni mtoto, anahitaji malezi na maangalizi.
Kwa aina ya waalimu tulio nao, hivi unawapa mamlaka yote hayo?
Mtaka ni moja ya members wazuri wa magrupu ya Chadema, na huwa mchangiaji mzuri wa fedha
Mtaka: Mwanafunzi mtukutu afukuzwe shule, asichapwe
View attachment 2559219
Njombe. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewaagiza wakuu wa shule za Serikali kuwafukuza wanafunzi watukutu badala ya kuwachapa viboko au kuwarudisha nyumbani.
Mtaka alisema hayo alipozungumza na wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Manyunyu, iliyopo Matembwe wilayani Njombe.
Alisema shule si sehemu za watu kufanya mizaha na wazazi wengi wanaheshimu sana shule binafsi lakini za Serikali mambo huwa tofauti.
“Kuna shule za binafsi zikiagiza mwanafunzi aje na nguo mbili wanaenda nazo hizohizo, ukienda na ya tatu unarudishwa, wanakuambia shule hii ni marufuku mtoto kuja na simu ukienda nayo unarudishwa nyumbani, huku kwenye shule zetu za umma tuna mizaha mingi,” alisema.
Mizaha hiyo alisema inasababisha mwanafunzi akifanya vituko na mwalimu akamwadhibu basi mwalimu atajadiliwa hadi kwenye mitandao ya kijamii na polisi watamkamata kuandika maelezo, lakini ujinga huo haufanyiki shule binafsi.
Alisema jamii inapozungumzia maadili ni lazima yasimamiwe na namna ya kuyasimamia ni kuyajenga tangu vijana wakiwa shuleni.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Valentino Hongoli alisema “mwaka jana mheshimiwa Rais alitupatia Sh60 milioni ambazo tulijenga madarasa matatu na ofisi shuleni hapa, kama tusingepewa watoto wangeshindwa kusoma.”
Mkuu wa Sekondari ya Wasichana Manyunyu, Advera Bagoka alisema wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu walikuwa 202, ila walioripoti ni 120 na 51 wamebadilisha shule, huku 31 hawajulikani walipo.
“Shule yetu ina uhaba wa walimu wa sayansi na hisabati,” alisema.
Akiwa jambazi anakamatwa na vyombo vya dola anafungwa! Simle like that, asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwenguJe kama angefukuzwa shule asingekuwa jambazi? Yoyote anaye-support watoto watukutu wafukuzwe shule ni juha na hana akili timamu.
Mbona suala la watoto watukutu kufukuzwa shule ni jambo la kawaida wala siyo jipya sema tu wewe umemuotea huyo Mtaka.Mtaka ni kama ana serikali yake ambayo haiendani na ya CCM na Samia, hivi mtoto unamfukuza shule ili iweje? Kwanza ni mtoto, anahitaji malezi na maangalizi.