RC Mtaka ataka wanafunzi wanaofanya makosa wafukuzwe shule

Acha wivu wewe. Mtaka hakuna RC Tanzania nzima anamfikia kwa utendaji. Na amesema ukweli kabisa. Shule za serikali nidhamu ni Sifuri. Watoto ni singeli tu huku wakiambulia madudu kwenye mitihani hasa O level mpaka serikali inaona aibu kuweka rank maana ni mikiani zipo. Sasa shule binafsi nidhamu iko juu na ufaulu umaendana na nidhamu. Shule za umma bangi na pombe, simu na uovu kibao. Kwa hiyo unataka waendelee kulea wahuni na majizi shuleni wakati hata madarasa hayatoshi? Acha wafukuzwe.kabisa ili waache miundombinu kwa walio tayari kusoma.
Halafu unamuungaje Mtaka na Upinzani? Kuna Jambo umamzushia ili apoteze nafasi yake? Halafu hata akiipoteza wewe na roho mbaya yako hupati chochote Hata akiipoteza Mtaka ni MTU wa watu Sana na hatalala njaa hata kidogo. Huyo mwache kabisa. Magufuli mwenyewe alimvulia kofia tena akaweka wazi kuwa wapo watu washenzi kama wewe walimfanyia vetting mbaya ili tu asipate cheo. Tena walisema eti hatakiwi kuwa hata mkuu wa Wilaya. Shame on them. Mrudisheni Simiyu maana pamepyaya Sana. Jembe liko kazini na kila sekta yumo. Simiyu alikuwa kipaumbele Elimu na alifanikiwa mno. Njombe yuko katika kuvuta wawekezaji kwenye Kilimo. Wewe hizi akili unazo au umebakiza tu za kupiga majungu. Na wewe unajiita Great Thinker. To hell.
Mbona point ya jamaa iko vzr! Umem quote vibaya, ebu rudia kusoma point yake, yeye yuko pamoja na Mtaka kama ulivyo wewe na wachangiaji wengine nikiwemo mimi
 
Kuna wakati kabla ya kuleta mada inabidi mfanye kwanza japo utafiti kidogo jamani.
 
Bora afukuzwe maana unaweza piga mpaka ukaua mwisho ukaozee jera
 
Acha wivu wewe. Mtaka hakuna RC Tanzania nzima anamfikia kwa utendaji. Na amesema ukweli kabisa. Shule za serikali nidhamu ni Sifuri. Watoto ni singeli tu huku wakiambulia madudu kwenye mitihani hasa O level mpaka serikali inaona aibu kuweka rank maana ni mikiani zipo. Sasa shule binafsi nidhamu iko juu na ufaulu umaendana na nidhamu. Shule za umma bangi na pombe, simu na uovu kibao. Kwa hiyo unataka waendelee kulea wahuni na majizi shuleni wakati hata madarasa hayatoshi? Acha wafukuzwe.kabisa ili waache miundombinu kwa walio tayari kusoma.
Halafu unamuungaje Mtaka na Upinzani? Kuna Jambo umamzushia ili apoteze nafasi yake? Halafu hata akiipoteza wewe na roho mbaya yako hupati chochote Hata akiipoteza Mtaka ni MTU wa watu Sana na hatalala njaa hata kidogo. Huyo mwache kabisa. Magufuli mwenyewe alimvulia kofia tena akaweka wazi kuwa wapo watu washenzi kama wewe walimfanyia vetting mbaya ili tu asipate cheo. Tena walisema eti hatakiwi kuwa hata mkuu wa Wilaya. Shame on them. Mrudisheni Simiyu maana pamepyaya Sana. Jembe liko kazini na kila sekta yumo. Simiyu alikuwa kipaumbele Elimu na alifanikiwa mno. Njombe yuko katika kuvuta wawekezaji kwenye Kilimo. Wewe hizi akili unazo au umebakiza tu za kupiga majungu. Na wewe unajiita Great Thinker. To hell.
Naona umejichanganya mpaka basi. Ungesoma kwa utulivu nilichokiandika hapo juu, usingekuja na haya maelezo yako marefu. Inawezekana umekosea katika kum quote mtu mwingine, ukani quote mimi.

Pole! Hii ndiyo jamii forums. Inabeba watu wa kila aina.
 
Akiwa jambazi anakamatwa na vyombo vya dola anafungwa! Simle like that, asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
Kwanini tutengeneze kizazi cha majambazi kwa makusudi, huko kuwa gerezani ni kuliingizia taifa hasara kwani wanakula, wanalala na wanahudimiwa kwa fedha za walipa kodi.
Nchi zenye elimu bora zaidi yetu hazina adhabu za kipumbavu na wala hawana utaratibu wa kufukuza, kukimbilia adhabu na kufukuza ni ukosefu wa akili. Watu wasio na exposure, waodhani kukomoa kwa adhabu ndiyo malezi wakiwa kwenye nafasi za maamuzi ndiyo huisababisha TZ kuwa nyuma kielimu ukilinganisha na nchi nyingine.
 
Mtaka ni kama ana serikali yake ambayo haiendani na ya CCM na Samia, hivi mtoto unamfukuza shule ili iweje? Kwanza ni mtoto, anahitaji malezi na maangalizi.

Kwa aina ya waalimu tulio nao, hivi unawapa mamlaka yote hayo?

Mtaka ni moja ya members wazuri wa magrupu ya Chadema, na huwa mchangiaji mzuri wa fedha

Mtaka: Mwanafunzi mtukutu afukuzwe shule, asichapwe​

View attachment 2559219

Njombe. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewaagiza wakuu wa shule za Serikali kuwafukuza wanafunzi watukutu badala ya kuwachapa viboko au kuwarudisha nyumbani.

Mtaka alisema hayo alipozungumza na wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Manyunyu, iliyopo Matembwe wilayani Njombe.

Alisema shule si sehemu za watu kufanya mizaha na wazazi wengi wanaheshimu sana shule binafsi lakini za Serikali mambo huwa tofauti.

“Kuna shule za binafsi zikiagiza mwanafunzi aje na nguo mbili wanaenda nazo hizohizo, ukienda na ya tatu unarudishwa, wanakuambia shule hii ni marufuku mtoto kuja na simu ukienda nayo unarudishwa nyumbani, huku kwenye shule zetu za umma tuna mizaha mingi,” alisema.

Mizaha hiyo alisema inasababisha mwanafunzi akifanya vituko na mwalimu akamwadhibu basi mwalimu atajadiliwa hadi kwenye mitandao ya kijamii na polisi watamkamata kuandika maelezo, lakini ujinga huo haufanyiki shule binafsi.

Alisema jamii inapozungumzia maadili ni lazima yasimamiwe na namna ya kuyasimamia ni kuyajenga tangu vijana wakiwa shuleni.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Valentino Hongoli alisema “mwaka jana mheshimiwa Rais alitupatia Sh60 milioni ambazo tulijenga madarasa matatu na ofisi shuleni hapa, kama tusingepewa watoto wangeshindwa kusoma.”

Mkuu wa Sekondari ya Wasichana Manyunyu, Advera Bagoka alisema wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu walikuwa 202, ila walioripoti ni 120 na 51 wamebadilisha shule, huku 31 hawajulikani walipo.

“Shule yetu ina uhaba wa walimu wa sayansi na hisabati,” alisema.
Na wafukuzwe tu waje uraiani na wakiyarudia hayo makosa uraiani kama ni jinai wapelekwe jera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingine huyu hapa wa ajabu ajabu! Kweli nchi yetu Ina watu wanao umwa
Sasa wewe ndoo umeandika nini? Hii nchi ina balaaa

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
Kabla ya kumshambulia mjumbe, kwa mtazamo wangu nadhani mlitakiwa kwanza muwe mna ABC kuhusu hiyo Tume ya Jackson Makwetta iliyoundwa kwa lengo la kufanyia kazi changamoto mbalimbali kuhusu elimu yetu, lakini mwisho wa siku ikaishia kwenye makabati ya wenye dhamana na elimu yetu.

Elimu yetu ina matatizo mengi. Na ni ukweli ulio wazi, wanasiasa wamechangia pakubwa kuharibu mfumo wetu wa elimu.

Mfano mdogo tu, ni ule wa kuruhusu wanafunzi wote kwenda sekondari! Huku wakitambua fika hao wanafunzi wamegawanyika katika makundi matati ya uelewa (according to Plato).

Matokeo yake ndiyo hayo ya kukutana na watoto wasiopenda shule! Wavuta bangi, wahuni, malaya, wezi, vibaka, nk! Na mwalimu akijaribu kupambana na watoto wa aina hii (maana tayari na yeye ameshinikizwa na wakubwa zake kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayepata 0 katika shule yake), anarekodiwa; na baada ya hilo tukio kusambaa, jamii inamhukumu mwalimu.

By the way, ninaunga mkono ushauri wa RC Mtaka.
 
Je kama angefukuzwa shule asingekuwa jambazi? Yoyote anaye-support watoto watukutu wafukuzwe shule ni juha na hana akili timamu.
Jenga hoja ili watu wakuelewe. Siyo lazima mtazamo wako wewe, basi ufanane na wa kwangu. Jifunze pia kuheshimu mawazo ya wengine.

Siku zote matusi hutumiwa na watu wasioweza kujitetea kwa hoja.
 
Kwanini tutengeneze kizazi cha majambazi kwa makusudi, huko kuwa gerezani ni kuliingizia taifa hasara kwani wanakula, wanalala na wanahudimiwa kwa fedha za walipa kodi.
Nchi zenye elimu bora zaidi yetu hazina adhabu za kipumbavu na wala hawana utaratibu wa kufukuza, kukimbilia adhabu na kufukuza ni ukosefu wa akili. Watu wasio na exposure, waodhani kukomoa kwa adhabu ndiyo malezi wakiwa kwenye nafasi za maamuzi ndiyo huisababisha TZ kuwa nyuma kielimu ukilinganisha na nchi nyingine.
Anayetengeneza hicho kizazi cha majambazi ni mzazi mwenyewe, kwasababu anashindwa kumlea mtoto wake kwenye maadili yanayo takiwa, mfano mtoto amefanya makosa shuleni mwalimu amempa adhabu kwa lengo la kumsaidia mzazi kumuweka mtoto kwenye utaratibu, mzazi huyo huyo ndo mtoa matusi kwa mwalimu, sasa kwanini sheria na taratibu za shule zisifuatwe??
 
Njombe. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewaagiza wakuu wa shule za Serikali kuwafukuza wanafunzi watukutu badala ya kuwachapa viboko au kuwarudisha nyumbani.

Mtaka alisema hayo alipozungumza na wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Manyunyu, iliyopo Matembwe wilayani Njombe.
Sheria inasemaje
 
Watoto wanakaa masaa mengi zaidi na walimu ila ni kweli kwenye malezi kunahitajika ushirikiano wa wazazi pamoja na walimu.
 
Walimu wa ushauri na nasihi ni muda muafaka kuajiriwa kwa uwingi mashuleni hasa sekondari wenda wakasaidia kuleta ufanisi mzuri katika kubadili tabia mbaya kwa baadhi ya wanafunzi na walimu wao mana kesi za walimu kwa wanafunzi, walimu kwa wanajamii, walimu kwa walimu zinazidi kufukuta kwa kasi.
 
Mtaka ni kama ana serikali yake ambayo haiendani na ya CCM na Samia, hivi mtoto unamfukuza shule ili iweje? Kwanza ni mtoto, anahitaji malezi na maangalizi.

Kwa aina ya waalimu tulio nao, hivi unawapa mamlaka yote hayo?

Mtaka ni moja ya members wazuri wa magrupu ya Chadema, na huwa mchangiaji mzuri wa fedha

Mtaka: Mwanafunzi mtukutu afukuzwe shule, asichapwe​

View attachment 2559219

Njombe. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewaagiza wakuu wa shule za Serikali kuwafukuza wanafunzi watukutu badala ya kuwachapa viboko au kuwarudisha nyumbani.

Mtaka alisema hayo alipozungumza na wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Manyunyu, iliyopo Matembwe wilayani Njombe.

Alisema shule si sehemu za watu kufanya mizaha na wazazi wengi wanaheshimu sana shule binafsi lakini za Serikali mambo huwa tofauti.

“Kuna shule za binafsi zikiagiza mwanafunzi aje na nguo mbili wanaenda nazo hizohizo, ukienda na ya tatu unarudishwa, wanakuambia shule hii ni marufuku mtoto kuja na simu ukienda nayo unarudishwa nyumbani, huku kwenye shule zetu za umma tuna mizaha mingi,” alisema.

Mizaha hiyo alisema inasababisha mwanafunzi akifanya vituko na mwalimu akamwadhibu basi mwalimu atajadiliwa hadi kwenye mitandao ya kijamii na polisi watamkamata kuandika maelezo, lakini ujinga huo haufanyiki shule binafsi.

Alisema jamii inapozungumzia maadili ni lazima yasimamiwe na namna ya kuyasimamia ni kuyajenga tangu vijana wakiwa shuleni.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Valentino Hongoli alisema “mwaka jana mheshimiwa Rais alitupatia Sh60 milioni ambazo tulijenga madarasa matatu na ofisi shuleni hapa, kama tusingepewa watoto wangeshindwa kusoma.”

Mkuu wa Sekondari ya Wasichana Manyunyu, Advera Bagoka alisema wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu walikuwa 202, ila walioripoti ni 120 na 51 wamebadilisha shule, huku 31 hawajulikani walipo.

“Shule yetu ina uhaba wa walimu wa sayansi na hisabati,” alisema.
Enzi za waliosoma zamani ilikua hakuna mchezo, ukileta utukutu unaambiwa nenda nyumbani halafu mwambie mzazi wako aripoti shule ili afahamishwe matatizo yako, na ukirudia tena unaambiwa peleka utukutu wango nyumbani au nenda kachunge kuku ujue hapo ndio umeshafukuzwa
 
Sahihisha hapo kwa Single mother's. Huwezi kuniambia watoto wote watukutu wanalelewa na Single mothers. Wapo Single mothers strong Sana kuliko Sisi wanaume na wame produce vidume na wasichana imara mno kila sekta. Ziko nyumba zina wazazi wote lakini watoto wameishia kuwa hovyo. Ungefanya utafiti ndiyo ufanye hii painful attach hata kwa dada na mama zetu humu ambao wako imara mno kimalezi. Ninafahamu single mothers kadhaa ambao watoto wao ni mfano Bora mno. Tena form four wanatoka na single digits na nidhamu mtaani ni perfect mpaka na admire mkuu. Poleni Single mother.

Tena Bora single mothers. Wako single fathers wa hovyo mno na watoto wanaharibika na wengine wanalawiti watoto na kesi ni nyingi mno. Hebu wasemee na hawa. Hatujawahi kusikia single mother kabaka mwanaye wa kiume. Haya tuendelee na mada ya Mtaka maana mleta mara ameshajificha.
Akili gani umetumia wewe kusoma?.

Ndiyo maana huwa nasema wengi mnasoma mada mbalimbali na hamtafakari au kuelewa kilichoandikwa.

Hebu screenshot nilipoandika SINGLE MOTHER'S, alafu weka namba yako nikutumie 10,000/- sababu ulielewa nilichoandika.
 
Back
Top Bottom