RC Mtaka ataka wanafunzi wanaofanya makosa wafukuzwe shule

Mbona point ya jamaa iko vzr! Umem quote vibaya, ebu rudia kusoma point yake, yeye yuko pamoja na Mtaka kama ulivyo wewe na wachangiaji wengine nikiwemo mimi
 
Kuna wakati kabla ya kuleta mada inabidi mfanye kwanza japo utafiti kidogo jamani.
 
Bora afukuzwe maana unaweza piga mpaka ukaua mwisho ukaozee jera
 
Naona umejichanganya mpaka basi. Ungesoma kwa utulivu nilichokiandika hapo juu, usingekuja na haya maelezo yako marefu. Inawezekana umekosea katika kum quote mtu mwingine, ukani quote mimi.

Pole! Hii ndiyo jamii forums. Inabeba watu wa kila aina.
 
Akiwa jambazi anakamatwa na vyombo vya dola anafungwa! Simle like that, asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
Kwanini tutengeneze kizazi cha majambazi kwa makusudi, huko kuwa gerezani ni kuliingizia taifa hasara kwani wanakula, wanalala na wanahudimiwa kwa fedha za walipa kodi.
Nchi zenye elimu bora zaidi yetu hazina adhabu za kipumbavu na wala hawana utaratibu wa kufukuza, kukimbilia adhabu na kufukuza ni ukosefu wa akili. Watu wasio na exposure, waodhani kukomoa kwa adhabu ndiyo malezi wakiwa kwenye nafasi za maamuzi ndiyo huisababisha TZ kuwa nyuma kielimu ukilinganisha na nchi nyingine.
 
Na wafukuzwe tu waje uraiani na wakiyarudia hayo makosa uraiani kama ni jinai wapelekwe jera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingine huyu hapa wa ajabu ajabu! Kweli nchi yetu Ina watu wanao umwa
Sasa wewe ndoo umeandika nini? Hii nchi ina balaaa

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
Kabla ya kumshambulia mjumbe, kwa mtazamo wangu nadhani mlitakiwa kwanza muwe mna ABC kuhusu hiyo Tume ya Jackson Makwetta iliyoundwa kwa lengo la kufanyia kazi changamoto mbalimbali kuhusu elimu yetu, lakini mwisho wa siku ikaishia kwenye makabati ya wenye dhamana na elimu yetu.

Elimu yetu ina matatizo mengi. Na ni ukweli ulio wazi, wanasiasa wamechangia pakubwa kuharibu mfumo wetu wa elimu.

Mfano mdogo tu, ni ule wa kuruhusu wanafunzi wote kwenda sekondari! Huku wakitambua fika hao wanafunzi wamegawanyika katika makundi matati ya uelewa (according to Plato).

Matokeo yake ndiyo hayo ya kukutana na watoto wasiopenda shule! Wavuta bangi, wahuni, malaya, wezi, vibaka, nk! Na mwalimu akijaribu kupambana na watoto wa aina hii (maana tayari na yeye ameshinikizwa na wakubwa zake kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayepata 0 katika shule yake), anarekodiwa; na baada ya hilo tukio kusambaa, jamii inamhukumu mwalimu.

By the way, ninaunga mkono ushauri wa RC Mtaka.
 
Je kama angefukuzwa shule asingekuwa jambazi? Yoyote anaye-support watoto watukutu wafukuzwe shule ni juha na hana akili timamu.
Jenga hoja ili watu wakuelewe. Siyo lazima mtazamo wako wewe, basi ufanane na wa kwangu. Jifunze pia kuheshimu mawazo ya wengine.

Siku zote matusi hutumiwa na watu wasioweza kujitetea kwa hoja.
 
Anayetengeneza hicho kizazi cha majambazi ni mzazi mwenyewe, kwasababu anashindwa kumlea mtoto wake kwenye maadili yanayo takiwa, mfano mtoto amefanya makosa shuleni mwalimu amempa adhabu kwa lengo la kumsaidia mzazi kumuweka mtoto kwenye utaratibu, mzazi huyo huyo ndo mtoa matusi kwa mwalimu, sasa kwanini sheria na taratibu za shule zisifuatwe??
 
Sheria inasemaje
 
Watoto wanakaa masaa mengi zaidi na walimu ila ni kweli kwenye malezi kunahitajika ushirikiano wa wazazi pamoja na walimu.
 
Walimu wa ushauri na nasihi ni muda muafaka kuajiriwa kwa uwingi mashuleni hasa sekondari wenda wakasaidia kuleta ufanisi mzuri katika kubadili tabia mbaya kwa baadhi ya wanafunzi na walimu wao mana kesi za walimu kwa wanafunzi, walimu kwa wanajamii, walimu kwa walimu zinazidi kufukuta kwa kasi.
 
Enzi za waliosoma zamani ilikua hakuna mchezo, ukileta utukutu unaambiwa nenda nyumbani halafu mwambie mzazi wako aripoti shule ili afahamishwe matatizo yako, na ukirudia tena unaambiwa peleka utukutu wango nyumbani au nenda kachunge kuku ujue hapo ndio umeshafukuzwa
 
Akili gani umetumia wewe kusoma?.

Ndiyo maana huwa nasema wengi mnasoma mada mbalimbali na hamtafakari au kuelewa kilichoandikwa.

Hebu screenshot nilipoandika SINGLE MOTHER'S, alafu weka namba yako nikutumie 10,000/- sababu ulielewa nilichoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…