BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Alhamisi ya wiki hii, Oktoba 27, 2022, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki shughuli ya ufunguzi wa Daraja la Mto Wami ambalo liko ndani ya Jimbo lake la Chalinze.
Daraja la Mto Wami limekamilika kwa 96% na litakapokamilika litaweza kuishi kwa Miaka 120. Daraja la Mto Wami linalounganisha Mkoa wa Pwani na Tanga, wakati Rais Samia anaingia madarakani Utekelezaji wake kwa zaidi ya miaka mitatu ilikuwa kwa asilimia 47 tu lakini ndani ya miezi 18 ya kwanza ya Rais Samia, Ujenzi wa Daraja hili kubwa sana na la kisasa umefanyika kwa asilimia 49.
Akizungumza baada ya kutembelea na kufanya shughuli ya ufunguzi wa Daraja hili, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ukamilishaji wa Daraja hili ni alama nyengine ya Utendaji wa uhakika wa Rais Samia Suluhu Hassan.