Ridhiwani: Daraja la Wami ni alama nyingine ya uhakika wa utendaji wa Rais Samia

Tunampongeza zaidi aliyemalizia kazi. Angetaka asingeendelea na mradi na msingemfanya chochote. Mbona JPM alistopisha mradi wa gesi na hamsemi. Mama anastahili pongezi nyingi sana.
Ipo mingine mingi tu inaendelea, Sgr, jpm Bridge, ikulu Dom, mjiwa wa mtumba, mahospitali kila kona ya nchi, etc, mwambie asitopishe asimalizie tuone itakuwaje!
 
Huyu dogo hawezi kusema lolote zuri kumhusu Magu maana alibinywa sana na Magu kwenye dili zake chafu. Wacha asifie aliempa ulaji lakini ajue Wami hiyo ni maelekezo ya Magu, akili (design) ni ya Marehemu Mfugale bingwa wa madaraja, waziri msimamizi akiwa Kamwelwe.
 
Screenshot_20221028-221740_Instagram.jpg
 
Alhamisi ya wiki hii, Oktoba 27, 2022, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki shughuli ya ufunguzi wa Daraja la Mto Wami ambalo liko ndani ya Jimbo lake la Chalinze.

Daraja la Mto Wami limekamilika kwa 96% na litakapokamilika litaweza kuishi kwa Miaka 120. Daraja la Mto Wami linalounganisha Mkoa wa Pwani na Tanga, wakati Rais Samia anaingia madarakani Utekelezaji wake kwa zaidi ya miaka mitatu ilikuwa kwa asilimia 47 tu lakini ndani ya miezi 18 ya kwanza ya Rais Samia, Ujenzi wa Daraja hili kubwa sana na la kisasa umefanyika kwa asilimia 49.

Akizungumza baada ya kutembelea na kufanya shughuli ya ufunguzi wa Daraja hili, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ukamilishaji wa Daraja hili ni alama nyengine ya Utendaji wa uhakika wa Rais Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2401186View attachment 2401187View attachment 2401188View attachment 2401189
Nyie waKijaninavheni kuwanga mchana kwenye Hilo faraja. Hizo vitambaa vya Nini hapo??
 
Bora hata ungemsifia Magufuli, walau ningekuelewa. Maana hilo daraja lilishakuwepo kwenye mpango wa ujenzi kitambo tu! Changamoto ilikuwa ni mtu wa kuanzisha ujenzi wake.

Huyo mama yako atakumbukwa kwa kuanzisha tozo za kukurupuka tu na Madelu wake.
Badala ya kusifia foundation mwenyewe JPM wanapindisha ionekane jiwe alikua na speed ndogo.
Nchi ina wanafki wengi sana
 
Bora hata ungemsifia Magufuli, walau ningekuelewa. Maana hilo daraja lilishakuwepo kwenye mpango wa ujenzi kitambo tu! Changamoto ilikuwa ni mtu wa kuanzisha ujenzi wake.

Huyo mama yako atakumbukwa kwa kuanzisha tozo za kukurupuka tu na Madelu wake.
Baba yake mbona hakulijenga wakati ndo chief wa jimbo enzi hizo.
 
Hafu huu upuuzi wenu nyie vijana fulani wawili ndani ya baraza ati kila mradi ulikuwa na asilimia za chini ila mama kapiga mwingi naona ka upuuzi mtupu
 
Alhamisi ya wiki hii, Oktoba 27, 2022, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete ameshiriki shughuli ya ufunguzi wa Daraja la Mto Wami ambalo liko ndani ya Jimbo lake la Chalinze.

Daraja la Mto Wami limekamilika kwa 96% na litakapokamilika litaweza kuishi kwa Miaka 120. Daraja la Mto Wami linalounganisha Mkoa wa Pwani na Tanga, wakati Rais Samia anaingia madarakani Utekelezaji wake kwa zaidi ya miaka mitatu ilikuwa kwa asilimia 47 tu lakini ndani ya miezi 18 ya kwanza ya Rais Samia, Ujenzi wa Daraja hili kubwa sana na la kisasa umefanyika kwa asilimia 49.

Akizungumza baada ya kutembelea na kufanya shughuli ya ufunguzi wa Daraja hili, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ukamilishaji wa Daraja hili ni alama nyengine ya Utendaji wa uhakika wa Rais Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2401186View attachment 2401187View attachment 2401188View attachment 2401189
Samia na madaraja wapi na wapi? Rizmoko aache mambo yake bana hata babake alishindwa kufikiria kujenga daraja jipya jimboni kwake. Sijawahi kumkubali Magufuli Ila haki na sofa yake apewe.
 
Hafu huu upuuzi wenu nyie vijana fulani wawili ndani ya baraza ati kila mradi ulikuwa na asilimia za chini ila mama kapiga mwingi naona ka upuuzi mtupu
Wanamjaza ujinga ili waendelee kubunya kiaina! Hizo ndiyo tabia za Watoto wa Mjini zilivyo, wenyewe wanakuambia wanaenda na upepo unako vuma!!
 
Mjomba Magufuli alianzisha ujenzi,Mama anamalizia ujenzi.Wote wanastahili pongezi.
Kama Magu asingeanzisha ujenzi,Mama asingemalizia ujenzi.
Lakini kama Mama asingeendelea kuweka pesa kwenye mradi huo ungesua sua kwa kipindi kirefu.
Mama amerithi miradi mikubwa ya Mjomba Magu lakini amejitahidi kuiendeleza kwa kuitengea pesa stahiki bila propaganda.
 
Back
Top Bottom