Ripoti ya CAG 2021-2022: Rais Samia ataka baadhi ya mashirika yasiyo na tija kufutwa

Kumbe kweliiii, aseeeh bas hatareee mnoo.
 
TTCL ni kampuni ya umma, naiona hatari simu nyeti kama za ikulu na Usalama zikipitia kampuni binafsi, ambazo wanahisa ni wale mabeberu.

TTCL wabaki na land line na miundombinu wezeshi ya mawasiliano
Mabeberu mnawaonea sana wakati Kazi yao ni kutafta tu faida, software nyingi za mawasiliano wao ndio wanakuuzia sema sisi watanzania hatuma mawazo ya pamoja kila mmoja na Lake hivyo kuleta ushabiki na ujinga kwenye vitu vya msingi.
 
Hayo mashirika anaposema yafutwe sio kama hayatokuwepo mbadala hapana .... kwa huku bongo tunakasumba kama shirika likishajijenge kwenye upigaji hata aje nan mwema kama hatojiunga nao basi atapigwa kitu kizito aondolewe, akimbie ama arogwe afe... so bora yafutwe tuu
 
Sijakuelewa, yaani shirika linafutwa alafu linaletwa mbadala? Hilo mbadala litakaloletwa litakua halina upigaji?
 
Kwanini Wakurugenzi, Bodi za Mashirika 14 yanayojiendesha kwa hasara waendelee na kazi zao?

Mashirika haya yamepata hasara kubwa sana
Mashirika haya yana Wakurugenzi na Bodi ambazo kazi yake ni kuweka malengo ili mashirika yafanikiwe, je kwanini waendelee kuwepo ofisini?

Rais Samia kama una uchungu wa nchi anza na hizo bodi, Wakurugenzi na Wasaidizi wao wote waondolewe kazini

Mashirika yafutwe

ATCL
NDC
TRC
TIB
 
ATCL, TRC na NDC ni mashirika muhimu kwa uchumi wa nchi.

Kuyavunja kutarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Pia kufanya hivyo kwamfanya raisi Samia nae aonekane ni sehemu ya tatizo kwa kukubali kushindwa kuwa ameshindwa kusimamia ukuaji wa mashirika hayo na uendeshaji wake.
 
Lina binafsishwa
Hayo mashirika ni mali ya taifa yaani assets hivyo huwezi kuyabinafsisha kwa watu binafsi.

Serikali yaweza tu kutafuta management ambayo ina utaalam wa uendeshaji na ikaingia nayo mkataba maalum.

India shirika lao la ndege Air India laongozwa na muingereza na ana ujuzi wa kusimamia mashirika mbalimbali ya ndege ya kimataifa.

Tukubali sisi baadhi ya waafrika akili zetu tumeziweka rehani.
 
Ukisema yafutwe unakuwa wajishusha sana kifikra.

Toa wazo la kuleta tija.
 
TTCL ni kampuni ya umma, naiona hatari simu nyeti kama za ikulu na Usalama zikipitia kampuni binafsi, ambazo wanahisa ni wale mabeberu.

TTCL wabaki na land line na miundombinu wezeshi ya mawasiliano
Mawazo ya kijima kutoka kwa wale wanaitwa BBC (Born Before Computers). Dunia hii kama hacker/Intruder anaweza kiingilia mawasiliano ya Vodacom kutaka kujua siri za Serikali basi hashindwi kuingia hata hizo za TTCL.

Nobody needs TTC, let them be euthanized right now
 
Wakurugenzi wa hayo makampuni yote wameteuliwa. Hakukua na interview Wala nini.
Tangaza kazi hizo watu wenye sifa wajitokeze.
Mfano mzuri, Maharage alifanyishwa na Nani interview? Sidhani Kama anajua kwamba Power =| squared R ama V=IR
 
Wakurugenzi wa hayo makampuni yote wameteuliwa. Hakukua na interview Wala nini.
Tangaza kazi hizo watu wenye sifa wajitokeze.
Mfano mzuri, Maharage alifanyishwa na Nani interview? Sidhani Kama anajua kwamba Power =| squared R ama V=IR
Kuna wakati wala huhitaji kujua hivyo vitu ili kuwa kiongozi mzuri, management skills, uzalendo na kuweka mbele maslahi ya nchi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…