Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kitaeleweka tu!Hatareee sana
NyingineSehemu ya 21
Nilijaribu kuufungua mlango, ukakataa, lakini pembeni yake palikuwa na kitu kama mashine ndogo, nayo ikaniandikia maandishi ya kuchagua lugha kati ya Kihindi na Kiingereza...
Daaaah imeishia patamu sanaSehemu ya 21
Nilijaribu kuufungua mlango, ukakataa, lakini pembeni yake palikuwa na kitu kama mashine ndogo, nayo ikaniandikia maandishi ya kuchagua lugha kati ya Kihindi na Kiingereza, nikachagua Kiingereza. Kisha mashine ile ndogo iliyokuwa chini ya kitasa, ikaniomba nichague njia ya malipo, kama nita ‘scan QR code’ au kama nitalipa kwa kutumia kadi yangu ya benki. Ni bahati tu nilikumbuka kutembea na kadi yangu ya benki yenye rangi ya dhahabu. Nikaitoa na kuipachika katika mashine, nikaweka namba za siri na kiasi cha Shilingi elfu hamsini kikakatwa, halafu mashine ikasema, ‘door unlocked.’ Nikahakikisha kwa kukizungusha kitasa, mlango ukafunguka, na kadri nilivyokuwa nazidi kuingia ndani, mapazia yakawa yanashuka ili kufanya walio nje wasiweze kutuona. Nilishangazwa sana na teknolojia hii iliyowekezwa katika biashara ya ukahaba!
Sasa nilikuwa ndani, mapazia yalikuwa yameshuka kiasi cha kutokuonekana na watu waliokuwa nje, nikatazama chini ya kitasa cha mlango, palikuwa na kimashine kama kile cha nje, lakini hiki kilikuwa kikihesabu muda na nilipotazama niligundua zilibaki dakika hamsini na nane. Hapo nikabaini kuwa, ile pesa niliyolipa, natakiwa kuwa ndani humo kwa saa moja, sikufahamu kama endapo ningezidisha muda nini kingetokea.
Baada ya kumaliza kukitazama kifaa kile, niligeuka. Masikini, msichana Asi hakuwa katika sofa alilokaa mwanzo, alikaa kwenye kona kabisa pembeni akiwa hana utayari wa kufanya jambo lolote. Alitetemeka na machozi yalimtoka, alikuwa amejikunyata kama kitoto cha chura, macho katazama sakafuni. Ndipo sasa niliitoa ile barakoa. Halafu nikaita, “Asii.” Alishtuka, akanitazama kwa hamaki, alipogundua ni mimi, akanirukia kwa furaha.
“Mako ni wewe?” Aliuliza kwa sauti.
“Ni mimi Asi,” nilijibu nikitabasamu. Kwa kuwa alinirukia, nilikuwa bado nimembeba, basi nikambwaga katika godoro lile lililojazwa upepo, tukanesa tukilaliana.
“Sikudhani kama ningekuona tena, hata sasa siamini Mako!” alisema msichana, nilipomtazama nikagundua aliyapunguza mavazi, sasa alibaki na kikaptura kidogo sana chepesi tena cha kubana, nikashangaa, mavazi mengine aliyabwaga muda gani?
Asi alikuwa mweusi aliyevutia sana. Umri mdogo, sura iliyochongoka kama yai na ngozi laini yenye umoto wa baridi kiasi nayo sauti yake ya mahaba iliyobembeleza mithili ya magita yanayopigwa na magwiji Dally Kimoko na Santana vilinichanganya ukizingatia nililala naye kitanda kimoja kilichotengenezwa kwa ajili ya starehe, basi nikajikuta nisiyejitambua, nikampiga busu, halafu nikazichezea chuchu zake zilizokuwa wazi, halafu taratiibu nikaanza kuushusha mkono kuelekea chini.
“Mako…” Asi aliita, sikuitika, akaendelea. “Unafanya nini Mako, mimi na wewe siyo wapenzi.”
Nilishtushwa na kauli hii ndipo nikakumbuka mambo yote, mimi na Asi hatukuwahi kuwa wapenzi, tulionana tu huko uswahili, akapotea na nikaanza kumtafuta.
“Mako,” Asi aliita, hakujali kama nimeitika au la, akaendelea, “Kama unanitaka, nitongoze, tena nitongoze kwa heshima zote na jibu lako nitakupa baada ya wiki mbili.”
Nilimtazama usoni nikiwa nimelalia ubavu wa kulia, naye akanitazama, tukacheka sana.
“Kwa mara ya kwanza nimeyaweka rehani maisha yangu. Kutaka kulala na mwanamke anayejiuza, mwanamke wa kila mtu,” nilisema nikimtazama Asi.
“Ni ngumu kuamini Mako, leo ni siku yangu ya pili humu, nimeanza jana, sikupata mteja siku nzima kwa sababu mapazia hayakufunguliwa, niliwaomba waniache nizoee hali ya chumba changu kwanza,” alijibu msichana.
“Kwa hivyo leo upo tayari kwa kazi?” niliuliza.
“Sipo tayari, muda wote nimejiinamia, nilipanga akipatikana mteja, nipambane naye, nife mimi au afe yeye, lakini kazi hii hapana.”
“Ilikuwaje ukaja hapa?”
“Babuu alikuja kwetu Tanga akidai anatafuta wasichana watakaofanya kazi nje ya nchi. Kazi zenyewe za ofisi na mshahara mnono. Alinichukua mimi lakini kwenye gari nilikutana na wenzangu watatu. Tulipofika Dar es Salaam katika ile nyumba uliyoniona, tukakuta wengine wawili, halafu walikuja wawili wengine wakatukuta pale. Peke yangu nilichukuliwa kuletwa India. Muda wote nilidhani nakuja kufanya kazi ya ofisi. Baada ya Kufika India, wametumia siku kadhaa kunitengeneza, kunifundisha taratibu za kazi hii namna tutakavyogawana malipo na ofisi, na mambo mengine mengi. Baada ya kuamini nimehitimu na kuelewa, sasa wamenibwaga humu nikisubiri wateja.”
“Pole sana Asi.”
“Asante sana kaka yangu, hata sijui nifanye nini?”
Inaendelea...
Kuwa wa Kwanza Kupokea mwendelezo wa Riwaya hii Kwa kujiunga katika Group la bure WhatsApp, Gusa Hapa Kujiunga
Tupate Wadhamini:
Kwa Mahitaji ya kuandikiwa CV, Barua ya Maombi ya Kazi na Masomo kwa Wanafunzi wanaorudia mitihani, Gusa Hapa Tuwasiliane Whatsapp.
walete waleteeeeeeeeeeeeeeeSehemu ya 22
“Suluhisho lipo, nimekuja kukuokoa!” nilisema kwa msisitizo.
“Umekuja kuniokoa mimi? Nakuona kama mtu ambaye umesafiri kuja India kwa mambo yako binafsi, na sasa unadhurura katika madanguro kutafuta kahaba wa kulala naye na kama bahati tu umeniona mimi unayenifahamu. Hata hivyo nafurahi kupata mteja kutoka nchi yangu.”
“Ni ngumu kunielewa Asi, lakini amini tangu niache kukuona, nimekuwa nikikutafuta na nimechunguza mengi mpaka leo nakupata hapa… unakumbuka uliwahi kuniuliza nafanya kazi gani?”
“Ndiyo… ukanijibu watu wengine kazi zenu huwa hazitajwi hovyohovyo! Kwa hivyo kazi yako ni kutafuta watu waliopotea, na kwa nini unafanya haya Mako, naona umejitoa kwa kiwango kikubwa.”
“Nafanya haya kwa sababu nakudai, nakudai pesa zangu, shilingi halali za Kitanzania, elfu kumi na tisa.”
Asi alicheka sana kisha akasema, “Muda wote nilikuona ukiandika katika kikaratasi, kumbe zilifika hela hizo,” alisema akiwa katikati ya kicheko na kuzungumza.
“Nisikilize Asi, unachotakiwa kufanya ni kuniamini, kunisikiliza ninachokuambia na kuwa mwepesi katika maamuzi, nisikilize, hustahili kufanyishwa unyama huu kwa maslahi ya watu wengine, wewe ni mtu unayestahili kuheshimiwa utu wako…” kabla sijamaliza kuzungumza, king’ora kikaanza kulia, nikatambua, muda wa saa moja niliopewa kulingana na malipo yangu ulikwisha hivyo nilitakiwa kutoka.
Akili yangu ilitafakari haraka kipi nifanye, sikuwa tayari kumuacha Asi eti nimfuate kesho. Kwa urembo wake, asingekosa bwana wa kumnajisi. King’ora kiliendelea kulia kikiniashiria nitoke, tukatazamana na Asi tusio jua la kufanya, lakini nikajikuta nikizungumza haraka, “Asi, vaa nguo kama suruali na koti ukiweza, nataka uonekane kama mwanaume japo watagundua, lakini tunatoka wote.
Msichana wa Kitanga hakuwa na namna isipokuwa kufuata maelekezo. Punde akawa kavalia mavazi niliyopendezwa nayo, suruali pana aina ya jinzi, na shati la mikono mirefu. Nilitembea nikiwa nimemshika mkono, tukatoka katika chumba kile na mara baada ya kuuachia mlango, ukajifunga na kuanza kuomba hela ili ufunguke. Mlango haukutambua kwamba, mhusika wa chumba aliibwa!
Usiku ulikwishaingia, lakini kwa sababu ya mataa tulionana. Muda wa usiku ilionekana ndiyo muda wa biashara haswa, kwani tulipishana na watu wengi waliokuwa wakikagua warembo wa kulala nao. Tuliendelea kutembea mpaka tulipofika getini, kwa jicho la kuibia, nyuma niligundua mambo yalikwisha haribika, watu waliovaa suruali na fulana nyeusi walikuja wakikimbia. Nikamkamata mkono kwa nguvu Asi kisha tukaanza kukimbia.
Tulikimbia tukijificha pembezoni mwa kuta ili tusionekane, waliotukimbiza niliwaona wakiteta jambo, kisha wawili wakarudi ndani, watatu wakaendelea kutufuata.
Tulikimbia muda mfupi mbele tukaona gari aina ya Toyota Pickup ikiwa imesimama kando ya barabara na mwanamke anafungua ili aingie ndani ya gari hiyo. Nilimkamata mkono mwanamke huyo wa Kihindi kisha nikamsukuma pembeni, akalalamika kwa kiingereza kwa nini namfanyia ukatili, nikamjibu, “Watu wabaya wanatukimbiza, natumia gari lako kujiokoa, tukifanikiwa tutaliacha mahali salama na utalipata.”
Tuliingia ndani ya gari mimi na Asi, yule mwanamke akabaki nje amesimama asiyeamini macho yake. Nikalitia moto gari lile lililokuwa na gia ‘automatic’, halafu nikagundua injini yake ilitumia ‘diesel’ nikafurahi sana.
Wakati naiwasha tu ile gari na kuweka gia iondoke, jamaa waliokuwa wakitukimbiza walifika, almanusura niwagonge lakini niliwakwepa. Nilipokunja kulia, ndipo nilipogundua kuwa, wale jamaa walijigawa makundi wawili, wengine waliendelea kutufuata kwa miguu na wengine walirudi kuchukua gari. Nilipoongeza mwendo tu, niliitambua gari yao, Ford Ranger, ambayo nayo ilikuwa ‘pickup’ kama gari yetu.
Inaendelea...
Kuwa wa Kwanza Kupokea mwendelezo wa Riwaya hii Kwa kujiunga katika Group la bure WhatsApp, Gusa Hapa Kujiunga
Tupate Wadhamini:
Kwa Mahitaji ya kuandikiwa CV, Barua ya Maombi ya Kazi na Masomo kwa Wanafunzi wanaorudia mitihani, Gusa Hapa Tuwasiliane Whatsapp.
Bure na itaendelea hivyo siku zote.Unaiuzaje hii yote.
Poa kaka nimeipenda sana.Bure na itaendelea hivyo siku zote.
Rudi ulete Mambo bosssSehemu ya 22