muuaji
watu waneokotwa kwenye viroba pwani ya bahari, wengine wamepotea, watu wamepigwa risasi, watu wamedhulumiwa biashara na pesa zao, korisho zao nk, wengine wamefukuzwa kazi kinyume cha sheria, mifuko ya hifadhi ya jamii imefurugwa na kuhujumiwa, mara kuanzishwe vitambulisho vya wamachinga kinyume cha sheria na taratibu, hadi mahakama zimeingiliwa, polisi wamefurugwa...anataman kuingilia mpaka jeshi na TISS kuwavuruga..mashekhe wapo magerezani kinyume cha sheria, maaskofu wanaambiwa si raia sababu wanadai demokrasia, wananchi wanawindwa kila mahali kama ngedere, hata tukicomment tu kwenye mtandao wa kijamii tunawindwa kama swala....huyo ndiyo useme analinda uhai wa watu? anyway...yana mwisho.
Inajulikana vyema kwamba ninyi ni watu kutunga na kutengeneza matukio daima. Juzikati hapa mlisingizia ambulance za serikali zinasafirisha kuwazika baharini maiti wa korona na ushahidi wenu ukiwa ni “video clips za Irani” za kubumba na kuediti. Mlidai maiti zingeokotwa barabarani watu wakiwa wamekufa kama kuku!
Ninyi ni mafundi-ulanzi wa kuchonganisha raia dhidi ya serikali yao. Hamtakaa mkubali kwamba ngoma hii imewashinda! Hamwezi kuicheza tena! Ndiyo maana mnaishia kusema “watu wame…,” “watu wame…,” hizo ni ngonjera mpya mlizojitungia.
Hakuna mfanyabiashara hata mmoja aliyedhulumiwa pesa yake; labda unazungumzia zile milioni 300 kila mwezi za ruzuku ya Chama cha Demoghasia & Maombolezo ambazo mwenyekiti wenu kaziingiza kwenye biashara zake. Wakulima wa korosho wamelipwa wote. Tozo na kodi zimefutwa zaidi ya 168!
Bima ya afya inafanya kazi vizuri, na inaendelea kuboreshwa deile! Utaratibu wa kuwapatia machinga vitambulisho umekuwa na ufanisi mkubwa sana, tofauti na vile walivyokuwa wananyanyaswa zamani. Wahujumu uchumi na wapiga-dili na wauza-madawa ya kulevya na walarushwa na wazembe wamewajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Na JPM azidi kuwakazia uzi kabisa hawa jamaa, bila kuwatazama usoni, maana wamelimaskinisha taifa muda mrefu! Mahakama zenu sasa ni bora na zinafanya kazi yake kwa weledi na haraka na kwa mujibu wa taratibu na sheria; idadi kubwa ya wafungwa imesamehewa na kuachiwa huru katika kipindi cha JPM, kuliko wakati mwingine wowote.
Jeshi letu limekuwa na nidhamu na mafanikio katika kazi zao. Rais wanaheshimu vyombo vya dola. Nchi imetulia. Maendeleo yanaonekana. Watu wanapiga kazi. Kuna nidhamu serikalini. Kodi inakusanywa. Nchi inaheshimika ndani na nje. Maisha yanasonga mbele. Miradi inachipuka: barabara & miundombinu mingine, umeme, maji, huduma za afya na elimu.
Aidha, ndege zipo kama zote, zingine zinakuja za kutosha tu. Watalii wanamiminika Tanzania. Amani na usalama Tanzania imerejea, isipokuwa tu kwa wahalifu na maadui na wachochezi, watu wabaya ndio wanaona hali siyo hali. Tanzania hivi karibuni inakuwa zaidi kuliko Ulaya na Marekani! Serikali imehamia Dodoma. Tanzania ya viwanda hiyo! “Mwenye macho haambiwi tazama!”