Rostam Aziz: Dkt. Slaa alihongwa 2015 kuisaliti CHADEMA, akapewa Ubalozi

Rostam Aziz: Dkt. Slaa alihongwa 2015 kuisaliti CHADEMA, akapewa Ubalozi

Haya ndio madhara ya kumpa mjinga akufanyie kazi, anaharibu kwa kiwango cha juu zaidi, matokeo yake unajikuta wewe uliyemtuma una kazi mbili za kusawazisha tofauti na mwanzo.
 
Angekuwa Aliyesema Hayo Maneno Mazito Siyo Mtu Anayekijua Chama Cha Mambuzi
Ungesikia UVCCM Wangemtaka Aombe Radhi Ila SasA Huyo Ni Mfanyabiashara Wa Ujanjaujanja Muda Wote


Ukiona Kaja Hadharani Kasema Hivyo Ujue Ccm Yote Imetepeta Keshakanyaga Pipe Ya Oxygen
Chama Chake Hakipumua, Na Wote Wamefyata Mkia
wanasonya Tu, Ccm Inanuka Kila Eneo
 
Kwa hiyo hoja ya Rostam Aziz ni kwamba kwa vile hafanyi biashara ya moja kwa moja na Serikali, basi hastahili kukosolewa au kushutumiwa kwa lolote sababu yeye ni Mfanya Biashara Binafsi anayefanya biashara na Sekta Binafsi hata kama anatembeza rushwa kwa vyombo vya Serikali ili kufanikisha biashara zake?
 
Hili ni swali tu ndugu zangu , maana kwa kauli yake kwamba ccm na serikali yake inanunua wapinzani na kuwahonga vyeo akiwemo Dr Slaa , ni sawa na ngumi ya Kidevu kwa chama kinachojinasibu kwa kufuata misingi ya haki .

Ikiwa Serikali ya ccm itashindwa kumchukulia hatua ndugu Rostam kwa kauli yake hii kabambe dhidi ya serikali ya ccm basi bila shaka itakuwa uthibitisho wa wazi kwamba kumbe ule uvumi wa miaka mingi kwamba ccm inanunua wapinzani ni kweli na ni dhahiri shahiri !

Jambo hili likiachwa lipite hivi hivi itakuwa aibu na dhalilisho kuu kwa serikali ya Tanzania .
 
Leo mtu mkubwa sana ambaye kapata kushika vyeo vingi CCM na kuwa Mbunge na pia ni mfanyabiashara mjanja mjanja ametamka kwenye press kuwa walimhonga Dr Slaa kwa vile alikuwa anawapelekesha na sasa wamemtosa.
Kumbe CCM inayopinga rushwa (kama ahadi ya chama ya sipokei wala kutoa rushwa) ndiyo kinara wa rushwa na inagawa mpaka vyeo, jee hawa watu wanastahili hata kuwasikiliza?
Tupewe ishara gani kutambua kuwa umasikini wa watu wetu chanzo ni hawa watu? Tumelogwa?
View attachment 2669613
Hii ipo Dk ya ngapi, nimeskiliza press yake sikuskia haya maneno.
 
Leo mtu mkubwa sana ambaye kapata kushika vyeo vingi CCM na kuwa Mbunge na pia ni mfanyabiashara mjanja mjanja ametamka kwenye press kuwa walimhonga Dr Slaa kwa vile alikuwa anawapelekesha na sasa wamemtosa.
Kumbe CCM inayopinga rushwa (kama ahadi ya chama ya sipokei wala kutoa rushwa) ndiyo kinara wa rushwa na inagawa mpaka vyeo, jee hawa watu wanastahili hata kuwasikiliza?
Tupewe ishara gani kutambua kuwa umasikini wa watu wetu chanzo ni hawa watu? Tumelogwa?
View attachment 2669613
Ni vigumu kuitenga Ccm na rushwa, hili linafahamika kitambo tu.
 
Wameanza kuumbuana wenyewe kwa wenyewe. Yaani watoa rushwa na wapokea rushwa.
Mbaya zaidi, huyo Rostam ametoa tuhuma nyingine nzito sana Kwa watawala wa CCM!

Akiongelea suala la DP World amesema kuwa hao wawekezaji hawawezi kuwa na Imani na mahakama zetu Kwa kuwa mahakama zetu, zinaongozwa Kwa "remote control" za watawala wetu!😎
 
sasa RA ndio kasema Dr Slaa alipewa hela, mimi nani nibishe....

huyu RA anamuendesha EL anampeleka EL lumumba na EL anasema nimerudi nyumbani, huyu RA anasafiri na President mpaka USA anasign mamikataba yakutosha.. mimi nani nimbishie..
 
kama aliweza kuwaambia uchwara aka anaachana na siasa uchwara na wote waliufyata mkia nani wakumgusa huyu.
 
Makamanda wote nyie mna Bei zenu huko Ndio maana kazi yenu huwa Ni kuropoka tu Kama makasuku,kwa ajili ya kutetea matumbo yenu wakati CCM inawatetea watanzania wanyonge,Nyie machadema Ni mavinyonga , wababaishaji,wasaka tonge na watu msiojitambua
 
Bilionea Rostam Aziz angejibu hoja za Slaa objectively badala ya kuelekeza mashambulizi binafsi kwa mtoa hoja, kwa lugha ya kisomi inajulikana kama ad hominem. Ishu ni hoja, siyo mtoa hoja. Alitegemea nani asiye na mapungufu binafsi kama binadamu amkosoe? Mtume Muhammad au Allah? Kwa hiyo tatizo ni nani anamkosoa, na siyo hoja ya mkosoaji?
 
Back
Top Bottom