Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Hivi wewe na Mimi tunao comment kwenye huu Uzi si ni wahusika wa kuamsha watoto usiku?

Ambaye hahusiki ujue mtoto wake Yuko boarding au St Kayumba.
Nahusika humu na mtoto wangu haamshwi saa10 hata siku moja, ni ujuha kumuamsha mtoto mda huo kisa aende shule, maeneo ya karibu hakuna shule yenye viwango vya kumpleka mtoto?

Unaishi Mbezi mwisho unampeleka dogo Mikocheni, are you for real? Hiki kizazi wazazi hatuna busara kabisa.
 
Upo sahihi, walau 5km distance! Sio mtoto anaenda 20km shule kila siku. Humtendei haki hata kidogo.
 
Boarding kwa umri huo ni kutelekeza mtoto, mbaya sana. Anadevelop tabia za ajabu, unamlaumu na kumpiga wakati ulimtupa akijifunzie huko.

Umeona athari za kuvuruga utamaduni? wanawake walipaswa wabaki na majukumu yao ya asili- kulea. Kula kwa jasho abaki nayo mhusika!
 
Upo sahihi, walau 5km distance! Sio mtoto anaenda 20km shule kila siku. Humtendei haki hata kidogo.
Wazazi wa familia 3 au 4 wanaweza kumrecruit mwalimu wa watoto wakamuandalia vifaa na mazingira biashara ya usumbufu ikaisha.
 
Toa nondo mama d mpaka waereweee😂😂😂

Mama mwenye busara zake

Ova
 
Hawa watoto wanapata muda kidogo wa kupumzika (kulala).

Isitoshe wanapewa 'home work' nyingi sababu masomo wanasoma mengi na hata mabegi yao makubwa sababu ya kubebeshwa madaftari mengi...

Hii sio sawa.
Hapa kwenye begi ndo panaponikera zaidi, utadhani mpagazi wa mt. Kilimanjaro

Kwani kuweka makabati huko mashuleni kila mtoto akapewa funguo yake ni /= kiasi gani?
Miundo mbinu mibovu ya shule, wamiliki njaanjaa akiona hana watoto anageuza mabanda ya kuku.
 
Tatizo ni uhaba wa mabasi kwenye hizo shule husika unakuta shule idadi kubwa ya wanafunzi lakini mabasi ya kukusanya wanafunzi yapo mawili au matatu.
Pia kuna haja ya kuelimisha wazazi ni kwa namna gani umbali wa shule na unapoishi vinavyo athiri afya ya akili na maendeleo ya taaluma ya mtoto.
 
Mpuuz uyo anaogopa wenzie watamuonaje, uku anahatarisha afya ya akili ya mwanae
 
Kiukweli hili halikubaliki mkuu[emoji3525]
 
Kiukweli umeongea hoja ya msingi Sana, enzi hizo tulifundishwa na Bibi zetu.

Ikitokea miaka ya 2000 kukawa na zile twishen ndogo ndogo za pale mtaani, mtoto anashinda pale anacheza uku anajisomea kdg kidg.
 
Uko sawa 100% Mama D. Mtoto wa miaka 4 unamwamsha kwa alarm? Huyu anatakiwa alale mpaka aamke mwenyewe usingizi unapomwisha.
Kuna haja ya waalimu kuanza kuspecialise kwenye private schooling kwa watoto. Watapata sana watu
Sahii kabisa,
Private home schooling inaweza saidia hili tatizo.
 
Kabisa,
Wazazi wanaitumikia pesa, na pesa inapelekea kuzitesa damu zao wenyewe.
 
Kwa nini tusiwe na hulka ya kuboresha shule zilizopo karibu na mazingira yetu, hii tabia ya kuamsha watoto saa 11 sio poa hata. Mtoto aamke 12, aandaliwe vizuri hadi saa moja aende shule akiwa fresh.
Sahii kabisa mzee mwenzangu
 
Huu upuuzi haufai hata kidogo
 
Sahii kabisa,
Kwa hili wazazi Ni kiungo muhimu kulikomesha, elimu itolewe
 
Ukisasa na umjini mjini umetupofusha kuhatarisha maisha ya wanetu.

Hii ya kua wote baba na mama wafanyakazi Ina athari zake Sana.
 
Sio kweli Mbezi, Kimara, Segerea kote hakuna shule nzuri mpaka umpeleke mtoto wako Mikocheni saa kumi usiku kila siku, ni ulimbukeni tu.

WA adopt basi hao watoto wewe maana una uchungu kuliko wazazi wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…