Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Hii inashangaza sana, nakaa eneo A

kuna siku niliamka saa 10 alfajiri kuwahi basi Ubungo, kituo cha daladala nakutana na wanafunzi (O-Level) wa Zanaki na Jangwani, ni mwendo wa 35 km mpaka uko Zanaki, ilihali eneo hilo kuna shule za sekondari kadhaa,

Kuna wazazi wengine wapuuzi sana...unakuta anakaa kimara na huko kuna shule nzuri tu lakini anampeleka mtoto shule tegeta au mikocheni.Unategemea nini hapo.
 
Hawa watoto wanapata muda kidogo wa kupumzika (kulala).

isitoshe wanapewa 'home work' nyingi sababu masomo wanasoma mengi na hata mabegi yao makubwa sababu ya kubebeshwa madaftari mengi...

Hii sio sawa.
Serikali iliangalie hili, tunatesa watoto wadogo bure. Wanahitaji kupumzika Sana Hawa ili ubongo wao ukue[emoji3525]
 
hii inashangaza sana, nakaa eneo A
kuna siku niliamka saa 10 alfajiri kuwahi basi Ubungo
kituo cha daladala nakutana na wanafunzi (O-Level) wa Zanaki na Jangwani, ni mwendo wa 35 km mpaka uko Zanaki
ilihali eneo hilo kuna shule za sekondari kadhaa,
Sijaelewa Hapa wazazi wanakua wamefanya nn Sana Kama sio kuwatesa hao watoto
 
Mimi mtu mzima tu kuniamsha saa 11 alfajiri mara mbili mfululizo ibidi ujipange.
Unless mchana niwe nalala tena.
Sasa Kama mtu mzima Ni kipengele, inakuaje kwa mwanafunz Tena mtoto wa miaka 4.

Kwanza nafikiria hata huu umri wa watoto kuanza kwenda shule nao urejerewe upya.

Naachoona sikuhz watu wanajipelekea TU watoto shule, Hakuna usimamizi wala Nini.

Tofauti na miaka ya zamani
 
Mkuu kupokea wanapokea but in a very low level,, kwenye elimu huuita "remembering",, but hawafikii the highest levels kama analysis au applying that's why tunalalamika elimu yetu ni ya kukaririshana
Mtoto wa Hivi hata alikua akili yake haitoweza kuchangia mambo kwa ufasaha zaidi,

Maana ubongo wake umetumikishwa mno kabla haujakomaa.

Tunakwenda kuzalishwa taifa la hovyo kabisa
 
Kuna mmoja alikuwa anarudi nyumbani na Manundu, wazazi wanashangaa. Kumbe mtoto anasinzia kwenye gari matokeo yake anajigonga kwenye machuma ya gari. Inasikitisha sana.
Ukatili kabisa huu
 
Imekaaje hii[emoji848]

Saa 11:20 alfajiri Unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni.

Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,

-Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?[emoji848]
-Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?[emoji848]
-Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?[emoji848]

Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote Ni wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA[emoji3525]

Unapoishi mji kama Dar es salaam Kuna vitu ambavyo maisha yatakuwa hayakupi uchaguzi...
 
Mtoto anatakiwa asome karibu na anapoishi, mtoto hatakiwi soma muda mrefu
Sidhan Kama wazazi wa kaliba Hii wanalitambua hili,

Went mamlaka wanapaswa kuingilia Kati, Elimu imefanywa biashara wameacha kuzingatia utu na Haki za watoto.
 
Nawaonaga jioni muda wa kurudi nyumbani, vimesinzia usingizi fofofo bus zima had huruma, sasa hapo ukute katoto kakike kamesukwa na dread za uzi kimevutwa nywele hatari, hapo unategemea mtoto atakua sawa kweli? Mtoto haogeshwi kichwa mwezi mzima kisa kimesukwa nywele halafu nywele zenyewe zinauma balaa, changanya na kukiamsha alfajiri hapo ni upuuzi mtupu
Huu wa kusuka Watoto na kuwakaza vichwa Ni unyanyasaji mwingine was watoto?

Kiukweli hawatendewi haki.

Tunakuja kutengeneza taifa la akili fyatu kwa mikono yetu wenyewe.

Inasikitisha Sana mkuu
 
Wazee wa kulialia kama kawaida yetu.

Usiwasahau wale wa kijijini wanaotembea umbali mrefu kwenda shule.

Solution umesahau kuweka.
 
Wee mkuu unaona liko sawa hili?
Unaweza kufanya hivi kwa wanao pia?

Hivi mtoto unaepishana nae saa 11, unahisi kaamshwa saa ngapi uyu?

Mtoto akiwa na miaka 3 lazima awe ameanza chochote, ukitegemea na location uliyipo kupata day care yaweza kuwa mbali...

School basi inaweza kuwa na route ndefu na inaanzia kwako, mtoto wako lazima aamke alfajiri au asiende Shule akae nyumbani.

Mimi siwezi kukubali ndo maana watoto wangu hawaishi dar. Ila watoto wakiishi Dar hauna uchaguzi, hayo mambo ni kawaida kabisa.
 
Hivi wewe na Mimi tunao comment kwenye huu Uzi si ni wahusika wa kuamsha watoto usiku?

Ambaye hahusiki ujue mtoto wake Yuko boarding au St Kayumba.
 
Sasa Kama mtu mzima Ni kipengele, inakuaje kwa mwanafunz Tena mtoto wa miaka 4.

Kwanza nafikiria hata huu umri wa watoto kuanza kwenda shule nao urejerewe upya.

Naachoona sikuhz watu wanajipelekea TU watoto shule, Hakuna usimamizi wala Nini.

Tofauti na miaka ya zamani
Tatizo kubwa show off na kufanya mambo kwa kushindana matokeo yake anaumizwa mtoto.

Kisa jirani au rafiki yako kampeleka mwanae shule fulani na wewe una mpeleka huko huko wakati eneo ulilopo au eneo jirani atleast 5 km kuna shule nzuri tu.

Kingine serikali iongeze masharti kwa hizi medium schools ziwe na magari mengi atleast magari 10 kuliko kutegemea gari 2 au 3 kwenda zaidi ya km 40 kubeba wanafunzi matokeo yake yanageuka mabweni asubuhi vilevile wanafunzi wanachoka mapokeo ya kile wanachojifunza yanakuwa ni hafifu.

Pia serikali iwape amri askari wakamate school buses zote zitakazo onekana zinabeba wanafunzi saa 10-11 asubuhi atleast zianzie saa 12 asubuhi hivyo watawahi masomo kwakuwa vipindi huanza saa 2 asubuhi tofauti na sasa licha ya kuwahi kubeba wanafunzi bado wanachelewa kufika shuleni sometimes hadi saa 3.30 asubuhi.
 
Kuna matatizo sehemu nyingi hapa.

Hata wazazi tuna matatizo pia.
  • Inakuaje mzazi unakaa 12 km kutoka shuleni kwa mtoto tena umepanga? kwa nini usipange karibu na shule ya watoto wako unaamua kupanga karibu na kazini kwako?
  • Kwa nini mzazi usimtafutie mtoto shule karibu na nyumbani. Kama kwa radius ya 5km na hapo unapokaa hakuna shule nzuri, basi umekosea mahali pa kupanga/kujenga.
  • Si lazima masomo yaanze saa 1 asubuhi kila shule. Ni kukariri tu. Shule zinaweza kuwa na masaa tofauti ya kuanza masomo.
  • Shule zibanwe ziwe na mabasi mengi ili route zisiwe za kuzunguka sana. Hii itasaidia kupunguza muda wa watoto kuwa njiani. Wenye shule wasipobanwa kwenye eneo hili hawawezi kujali maana ni mahali wanapobana matumizi.
  • kama kwenye eneo moja kuna watoto wa shule moja wengi wazazi wanaweza ku opt kutolipia basi la shule wakatafuta usafiri wao wenyewe. Kuna mahali wazazi wamekodi noah inachukua watoto asubuhi na kuwarudisha jioni, badala ya basi la shule. Wanatumia pesa nyingi zaidi lakini kwa manufaa ya watoto wao
Kama hamna namna basi walau mtoto alale mapema ili apate masaa mengi ya kupumzika. Usimwache akaangalia tamthilia mpaka saa 4 usiku.
 
Back
Top Bottom