Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Ila kweli wanateseka aisee..wakifika nyumbani hakuna kucheza,ni kufanya homework na kula.Sasa wakicheza si watachoka sana jamani
Ni Uonevu usiomithilika kabisa huu mkuu
 
Na mabegi makubwa mgongoni kama wapanda mlima Kilimanjaro
 
Hawanunui magari ya kutosha,hapo watoto wapelekwe shuleni halafu wanafuatwa wengine kwa gari hilo hilo na unaweza kuta hiyo shule haipo mbali sana na makazi yao.
 
Unapoishi mji kama Dar es salaam Kuna vitu ambavyo maisha yatakuwa hayakupi uchaguzi...
Sio kweli Mbezi, Kimara, Segerea kote hakuna shule nzuri mpaka umpeleke mtoto wako Mikocheni saa kumi usiku kila siku, ni ulimbukeni tu.
 
Nimejikuta nacheka balaa,napenda kusuka ila mwanangu big no akikua ataamua mwenyewe yaani unakuta kitoto kimesukwa nywele mzigo kichwani kimevutwa hadi huruma jamani kwakweli wazazi tujitafakari watoto wanapitia mateso.
 
Hiyo ni kazi ya serikali kuboresha mashule ya kata wanayojenga siyo siasa tu. Kwani hela ya serikali kazi yake nini kila kitu tujenge wananchi?
 
Change begins with you! Asilimia kubwa ya wanaolalamika humu ndiyo hao hao waliotufikisha hapa kwa kutofanya sehemu yao kikamilifu mahali fulani!

Ndiyo makandarasi walioshindwa kukamilisha ujenzi wa mabarabara waliokabidhiwa kujenga na hivyo kutusababishia mifoleni inayofanya watu kuanza safari usiku usiku kama wachawi ili tu kuwahi wanapokwenda, ndiyo wajenzi wa mashule, ndiyo wanandaa sera, ndiyo walimu wakuu, ndiyo wabunge, ndiyo mawaziri, ndiyo hao hao!

Mmejificha kwenye ID fake na sasa mnajidai kulalamika! Nendeni mkatimize sehemu zenu!'
 
Kama muda wao wa kulala sio zaidi saa kumi na mbili jioni(18:00) hakuna tatizo. Zaidi ya hapo sio afya

Wahusika wa shule (waalimu, wamiliki n.k) wangejibu hii hoja tuwasike na wao wanasemaje.

Inawezekana wao wanajua muda wa hao watoto kulala ni saa 18:00 jioni na pengine walishakubaliana na wazazi kuhusu swala hilo.

Vikao vya wazazi, waalimu (parents day) ni muhimu sana, kazi yake ndio kushuhulikia maswala muhimu kama haya.
 
Sema dar ndo ipo hvyo kwasababu ya foleni ila mikoani saa moja ndo wanaamka dar kila kitu shida.
Siyo sababu ya foleni ni uchache wa magari ya shule. Unakuta shule ipo segerea mwisho na watoto wanaishi kinyerezi afu wanashukuliwa saa12 kasorobo, hapo kuna foleni kweli??
 
Watanzania hatuna maZoea ya kulala saa 12 jioni, labda jela kwa Lazima.

Kwenye hizi familia zetu Ni nadra sana hizo kitu, KWANZA Ni wazazi wachache Sana MDA huo unawakuta nyumbani[emoji4]
 
Tatizo kubwa Sana hili mkuu
Sana....mtoto mpaka arudi home ni usiku na kesho alfajiri anaamshwa tena.

Kuna dem mmoja alikua anakaa Sinza halafu mtoto wake alikua anasoma Goba tena yupo grade 3.

Sasa siku ananihadithia eti jinsi anavyomuonea huruma mtoto wake kumuamsha sa 10 nilitamani nimtie makofi aisee halafu shule yenyewe ya kawaida tu ambako kila sehemu zimejaa,eti kisa mwenzie anaefanya nae kazi alimwambia ni shule nzuri
 
Teh teh teh teh πŸ˜‚ πŸ˜‚πŸ˜‚...umeamua kuwapa makavu...teh πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Elimu Bora au Bora elimu.
Kuna mdau kasema kwa uchovu wanaofika nao watoto, kule shuleni wanakuepo Kama masanamu TU kufata formality.

Ila akili yote hata haiko shuleni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Elimu ya hii nchi imekaa katika mfumo wa kimagereza shule zimegeuka kuwa magereza ya watoto kibaya zaidi mzazi unalipia gharama za indirect imprisonment of your own fucking child...AMKENI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…