Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Kero zenu ni ngumu mno kutatuliwa na serikali ya Tanzania..kwanza watoto wanaosoma nje ya shule za umma wamekuwa as if sio priority.hawanaga msemaji, hata NGO's kama HAKI ELIMU au TWAWEZA wanamulika sana dosari wanaziona kwny shule za serikali kuliko za private..solution nyie wazazi wa watoto husika undeni umoja wenu.
kwamba serikali hua inapeleka ruzuku shule private ?
 
Kwakweli hili ni janga mtoto wa dada yangu ana miaka 10 yupo class 4 anatoka nyumbani saa 11:15 Asubuhi kila siku na darasan anatakiwa kuingia saa 12:30 Asubuhi eti kisa yupo darasa la 4 wanaandaliwa na mitihani ya necta darasa la nne
Na hapo kurudi 11:30 jioni
 
Hii maadaa nimeitupia kwenye group langu la WhatsApp la Wazazi na Walimu shuleni kwa wanangu,na mchezo huo nao wanao maana shule yao inaanzia hizo age za 4 na 6! Bado nasikilizia majibu kutoka huko!!
Usisahau kuleta mrejesho mkuu
 
Aisee...
Kuna kabila ninalifahamu ni la wapenda elimu, wakijua shule nzuri iko Magomeni na yeye amejenga ghorofa Makongo, atatafuta chumba Magomeni na watoto na mama wataishi pale J3-Ijumaa. Atasamehe ndoa wiki nzima mradi watoto wanapata elimu bora na Ijumaa anakwenda mwenyewe kuwachukua warudi nyumbani.
Aisee!
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Nadhani kuna haja labda ya Serikali kushauriwa ili iweze kuja na muongozo wa muda wa masomo wa shule hizi za awali. Pengine labda inabidi wazipangie muda wa watoto hawa kusoma, possibly wawe wanaanza hata saa 3 na kumaliza saa blaa blaa. Hii holela ya muda kila mwenye shule kujiamuria muda wake wa masomo kwa watoto hawa inavuruga, na itakuja kutuletea madhara kwa watoto. Kwa watoto wa rika hili, muda huu wa kuamka kwenda shule unakuwa ni adhabu kubwa mno kwao, na hivyo shule inakuwa adhabu kwao kwa ujumla wake. Mtoto wa rika hili anatakiwa aende shule akiwa amefurahia, na siyo kwenda analia kwa sababu ya kulazimishwa.
Mungu akubariki sana kwa kuguswa na jambo hili la msingi mno
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Ni zaidi ya ukatili Kwa watoto

Mtoto wa 4-9 years hata some wapi, kama ni smart atakua tu

Hakuna haha ya kumtesa kwenda kusomea mbali
 
Halafu kurudi nyumbani mara nyingi ni saa 10 mpaka 12 jioni! Unakuta katoto kamechoka na kusinzia tu kwenye hayo magari yao!

Haya ni zaidi ya mateso aisee kwa watoto.
Watoto wanateseka sana kwa kweli. Wanapata adhabu kubwa ambayo watu wazima wote waliopo muda huu hawakuwahi kuipata.
 
Mimi mtu mzima tu kuniamsha saa 11 alfajiri mara mbili mfululizo ibidi ujipange.
Unless mchana niwe nalala tena.
Kuna mtoto mimi niliwahi kumshuhudia mahali fulani kwa jamaa zangu alikuwa anapenda sana kwenda shule. Walipoamua kumpeleka, baada ya siku kadhaa akawa hataki tena shule. Mimi nilikuwa naishi na kaka yangu mahali nikampa taarifa za mtoto huyu baada ya kuwa nimezisikia wakilalamika kuwa hataki shule wakati mwanzoni alikuwa napenda sana. Nikwamweleza kuwa ANA alikuwa analilia kwenda shule lakini sasa wanalalamika kuwa hataki tena shule. Jamaa hapo hapo akaniuliza swali "wanamwamsha saa ngapi asubuhi"?, nikamjibu. Jamaa akatulia kidogo halafu akaniambia, SIYO SHULE ILIYOMSHINDA. KILICHOMSHINDA NI ULE MUDA WA KUAMKA KWENDA SHULE
Hawa watoto bora hata wawe wanachelewa kurudi jioni, ila wawe wanaondoka katika muda ulio sahihi asubuhi
 
mimi wanangu nilipoona ratiba ya school bus ndo kama hiyo nikasitisha mara moja maana mtoto anaamka usiku na anarudi jioni kachoka hata kula hawezi ni kulala tu ikabidi nifute hayo mambo ya school bus anaondoka asubuhi saa moja namshusha shule ndo naenda job walau imesaidia naona hata darasani anaimprove na anaipenda shule siyo kwa kipindi kile cha school bus mtoto anasoma kama adhabu
 
Kuna kabila ninalifahamu ni la wapenda elimu, wakijua shule nzuri iko Magomeni na yeye amejenga ghorofa Makongo, atatafuta chumba Magomeni na watoto na mama wataishi pale J3-Ijumaa. Atasamehe ndoa wiki nzima mradi watoto wanapata elimu bora na Ijumaa anakwenda mwenyewe kuwachukua warudi nyumbani.
Hii iko safi sana yaan, ndo inavyotakiwa sasa.
 
Kuna jamaa mmoja watoto wake kuanzia darasa la kwanza hadi form six wamesoma bweni[emoji2][emoji2]
 
Mtu yupo kigamboni au Mbagala alafu mtoto wa miaka minne anampeleka shule Upanga haiingii akilini kabisa yaani kuungisha majirani zako wenye day care unaona wanafaidi utasema kwa umri huo kuna vitu vya msingi sana mtoto anavyofundishwa huko shuleni
 
Twende mbele turudi nyuma jamani!

Hivi mtoto wako wa miaka mitatu/minne (chekechea )unashindwa kumfundisha mwenyewe nyumbani?!

Mimi nilifundishwa nyumbani na mama tena huko kijijini nilipoanza la kwanza na waliosoma chekechea nikaongozea mbona?!!

Ujinga ni wa wazazi wa leo, acha waliwe mipesa na kutesa watoto wao kwa pesa zao wenyewe[emoji3525]
Mimi kabla sijaanza darasa la kwanza nilikuwa najua kusoma na kuandika vizuri kabisa

Kaz hii aliifanya mjomba wangu nilikuwa nakupa mbata ile mbaya mpera hadi nkajua kusoma gazeti at age of six tu.

Shuleni nilienda fanya marejeo

Na darasa la 7 nilifaulu safi kabisa enzi zile ukifualu la saba bonge ujiko tena hapo dar es salaam.

Matokeo tulikuwa tunacheki pale kinondoni manispaa au gazetini.

Shule zetu ilikuwa

Azania
Dar sec
Benja
Zanaki
Kisutu
Jangwani
Kibasila
Kambabgwa
Kiluvya
Forodhani

Dar nzima hizo ndip zilikuwa shule za serikali enzi zile kabla ya ujio wa shule za kata
 
Yaani kati ya vitu ambavyo huwa naishanga Wizara ya Elimu ni suala la kuthibiti shule binafsi, yaani kweli mtoto wa miaka 4 anaamka saa 10 alfajiri anarudi saa 12 , afu tunaona sawa tu , duuh,
kweli sisi elimu zetu za kakariri. Mbona zamani tulikuwa tunaingia shuleni saa 4 asubuni tunatoka saa 7 na tumefika mbali !!
ukiangalia sababu ni kwamba mmiliki wa shule anabania gharama ya petroli ili tripu ziwe chache hivyo wanaoumia ni watoto , Wizara ipo kimya,
 
Back
Top Bottom