DPP anatishia kupeleka watu gerezani. lakini DPP hasemi kwanini amevunja CPA, kifungu cha 91, Sura ya 20. Shauri lipo mahakamani, hakimu/Jaji ndio wanaweza kumtoa mtuhumiwa gerezani kwa remove order sio DPP (mlalamikaji). Nolle Prosequi inakutaka ueleze mahakama. Hukufanya hivyo.
Sheria haikupi mamlaka ya kumpeleka na kumtoa mtuhumiwa gerezani bila kibali cha mahakama. Ulichofanya kwa Nusrat ni mwendelezo wa kukanyaga sheria kwa kiburi tu. Umeweka bila kosa la msingi na umewatoa gerezani bila kufuata utaratibu. Kifupi umewakomoa, Nusrat kahongwa ubunge
DPP, ukisoma chapter 20, Section 91, CPA, part IV "Power of the DPP to enter nolle prosequi" haikupi mamlaka ya kumtoa mahabusu gerezani bila amri ya mahakama. Sheria inakutaka uieleze mahakama au kujulisha mahakama kwa maandishi kwa niaba ya Jamhuri. Hujafanya hivyo kwa NUSRAT.
Kwa utaratibu wa magereza Tanzania, wafungwa wanahesabiwa saa nane mchana, wanajiandaa kuingia selo saa tisa hadi saa kumi. DPP hana mamlaka ya kwenda gerezani kumtoa mahabusu au mfungwa saa moja na nusu usiku bila kibali cha mahakama kwa amei ya hakimu au Jaji. DPP hana mamlaka hayo, kisheria.
Kuhusu hilo la Freeman Mbowe, kwamba pamoja na wenzake, Mlimani City aliongoza kwa kuimba "Mungu ibariki Chadema" sehemu ya "Mungu ibariki Tanzania", kwanini iwe kosa kwa Mbowe sasa (ukitishia kumkamata) na iwe sio kosa kwa Nusrat hadi kuachiwa huru na mashtaka yake kufutwa?
Kama ulimkamata Nusrat kwa kosa hilo na ukamuacha iwe vipi halali kudhani Freeman Mbowe alitenda kosa hilo ambalo umelifuta kwa Nusrat na wenzake? UHALALI huo unatoka wapi? Kama Nusrat aliachiwa na kufutiwa mashtaka maana yake sio kosa, kwanini ulete stori nyinginezo.
Sio wajibu wa DPP kukamata watuhumiwa. Sio wajibu au jukumu la DPP kuwatoa watuhumiwa gerezani. DPP ni mwendesha mashtaka. Kusema "au na yeye (Mbowe) nimkamate?) ni kutishia raia kwa mamlaka ya ofisi yako. Sheria hazifuatwi. Tumeamua kufuata watu sio sheria.
DPP ni mlalamikaji katika kesi za jinai akiwakilisha Jamhuri. Mfungwa/mahabusu akiwa gerezani ni mali ya Gereza. Hakimu/Jaji wanaweza kumtoa gerezani kwa amri ya mahakama sio DPP. Katika mashauri ya Jinai, Jamhuri ni mlalamikaji. Kesi inafutwa na mahakama. Baada ya DPP kujiondoa.
DPP anasimama mbele ya vyombo vya habari anatamba kwamba "mimi ndie nimemtoa gerezani kwa mamlaka yangu" hadhi na mamlaka ya mahakama inapokwa na DPP. Kuirejesha nchi yetu kwenye misingi, lazima tuwaeleze hawa watu ukweli, sio "semi god".
Mamlaka ya mahakama imeporwa.
#MMM, Martin Maranja Masese