Saa ya Rais Samia yadaiwa kuwa na thamani ya Tsh. Milioni 111,601,22/=

Failure kwa sababu hakuwa fisadi kama mlivyo nyie?
Kabishane na waliovaa suruali zenye viraka kwa sababu yake,
Kabishane na waliopanga folen masaa 10 ili kununua sukari nusu kg kwa ajiili yake
Kabishane na walionunua nguo kwa zamu
Kabishane na wananchi waliochelewa kuzijua TV Africa nzima kwa ajiili yake 😂
Kabishane na wananchi waliozuiwa kununua computer kisa uroho wake wa madaraka 😂😂

Sasa ndio rais mzuri huyo ?
 
Ukitawaliwa na roho ya kishetani hauwezi ku-feel guilty consciousness, roho inakuwa ngumu haswaa.
Hata mioyo iwe migumu kiasi gani lakini furaha moyoni huwa ni ndogo sana !
Ni sawa na furaha ya mlevi anapokuwa amelewa anahisi furaha,
Lakini akiamka anaamka na mning’inio bab kubwa 😂
 
Lakini serikali hiyo hiyo ya Nyerere enzi hizo ilikuwa inaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi maskini ikiwemo elimu, matibabu, maji nk.

Fikiria maelfu ya wanafunzi ndoto zao za kielimu zimekufa kwa kunyimwa ufadhili wa serikali, halafu eti nikanunue saa ya milioni mia.....hiiii bhagosha!​
 
Hata mioyo iwe migumu kiasi gani lakini furaha moyoni huwa ni ndogo sana !
Ni sawa na furaha ya mlevi anapokuwa amelewa anahisi furaha,
Lakini akiamka anaamka na mning’inio bab kubwa 😂
Amani ya moyoni ni utajiri mkubwa kuliko mali na anasa.
 
Kutazama muda tu milioni mia na ushee, hii ni kufuru na kejeli kwa watanzania maskini.
 
Cheki hiyo longines gold watch
Nchekie bei ikoje sshivi huko
Hii saa ina kama 20+ yrs

Ova
 
Hatununuliki kirahisi hivyo
Tumnange kwenye ishu za kimsingi, sasa huo mshahara wake anautumiaje kama tunaanza kumkagua mpaka mavao yake?
Sikutegemea kusoma hili kutoka kwako. Kiongozi mkuu anasomeka fikra zake kwa wananchi wake kwa hata muonekano wake na matumizi yake.
Hajafanya kosa lolote lakini katika nchi iliyoyopea umasikini wa kiwango cha watoto wanaenda shule kaptula zimetoboka na wanakaa chini, wakinamama wanajifungua sakafuni na kadhia za aibu chungu nzima Rais wao anavaa saa ya urembo ya zaidi ya milioni 100 na wanamtangaza kama mtu mwenye uchungu na watu wake.
 
Sikujua kama unaweza kuwa na low thinking kiasi hiki, kwani hivyo vitu vya umaalum haviwezi wekwa kwa saa ya million 5 na vikafanya kazi ile ile ya saa ya million 100? unapokuwa kiongozi hata mavazi yako yanatoa ujumbe kwa unaowaongoza..kwa mtu anayefahamu kusudi la aliyemuumba kumpa utajiri, uongozi au kitu chochote cha kufanyia watu wengine, hawezi kuwa na muda wa kuwaza anasa! hana nafasi au uwezo kufanya anasa..mara mia watoto wake wafanye fahari za aina hiyo lakini si yeye kama kiongozi.
 
Hatununuliki kirahisi hivyo
Tumnange kwenye ishu za kimsingi, sasa huo mshahara wake anautumiaje kama tunaanza kumkagua mpaka mavao yake?
Ni ujinga kiongozi wa nchi masikini tena anayelipwa mshahara kwa kodi za masikini kuvaa saa ya milioni 111 wakati wale unaowaongoza hawana uhakika wa milo motatu kwa siku! Kuna tofauti ya kiongozi na 'boss' Rais anapaswa kuwa kiongozi na sio boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…