Sababu za kiroho kwanini lazima ufunge Ramadhani hata kama sio muislamu

Kalenda zote ni feki. Ukitaka kujua jiulize zilianza lini, kwanini na nani alizianzisha. Hivyo, ukitetea moja na kuiponda nyingine, mbali ya kuwa dalili za kutojua na upendeleo, ni sawa na kuruka mkojo na ukakanyaga manonihino mwanangu.
Hawachelewi kusema ilishushwa,wana akili ndogo sana hawaamini katika miujiza huku kimoyo moyo wanaipenda unafiki huu!
 
Hizi ndo hadithi kama zile za juma na uledi..


Yaani utume askari 10000 kuvamia seemu yenye majeshi, alafu wasiue mtu hata mmoja..

Hao labda hawakua na jeshi kabisa, walivamia raia tuu
 
Izi lawama Sasa sio uthibitisho kua Hakuna Mungu
 
Unachangia vitu usivyo vijua kwaio funga unafikir ni kula tu?
 
Nimekuelewa kuhusu nature inakutaka ufanye kitu gani kwa wakati gani asante
 
Izi lawama Sasa sio uthibitisho kua Hakuna Mungu
Kuwepo kwa lawama ni uthibitisho Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Mungu huyo angekuwepo, kitu kinachoitwa lawama kisingekuwepo wala kujulikana.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Kuwepo kwa lawama ni uthibitisho Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Mungu huyo angekuwepo, kitu kinachoitwa lawama kisingekuwepo wala kujulikana.

Thibitisha Mungu yupo.
Mungu asinge kuwepo hata lawama zisinge kuwepo sababu ungekua unamlaum Nan??? Lawama pia ni ushaid wa Mungu kuwepo sababu yeye ndie mlaumiwa
 
Mungu asinge kuwepo hata lawama zisinge kuwepo sababu ungekua unamlaum Nan??? Lawama pia ni ushaid wa Mungu kuwepo sababu yeye ndie mlaumiwa
Hujathibitisha Mungu yupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, angeumba kila kitu kizuri hakina lawama, lawama isingekuwepo.

Kuwepo kwa lawama ni uthibitisho kwamba Mungu huyo hayupo.
 
Hivi unachokiandika huwa una kielewa ? Unaposema Mola ji muweza wa yote swali lolote dhidi yake katika uwezo wake ni la uongo. Yaani hayo unayoyadai yote ji katika uwezo wake yaani hakuna kinachotoka nje ya milki yake na ametaka iwe hivyo.

Sasa unachokiandika wewe ni kama kutokea kwa hayo mambo ni udhaifu na ni jambo lililo nje ya uwezo wa Mola,swali ambalo ni la uongo na haliwezekani. Jaribu uwe unafikiria unachokiandika.
Tunaambiwa amejaa upendo na huruma, lakini anaachia watoto wasio na hatia wanakufa kwa njaa na magonjwa na majanga mengi.
Hii ndiyo ile maana ya mjuzi wa yote mwenye huruma,na amejaalia katika kika jambo liwe na sababu. Maana yake anayajua sisi tusiyo yajua. Na wakifa wanarejea kwake sababu kifo ni haki ya kila kilicho hai.

Magonjwa na mitihani vyote vinatoka kwake.
Watu kuwa na fingerprint tofauti si ushahidi kwamba Mungu yupo, ukijua computer programming kidogo tu utajua kwamba unaweza kutengeneza dataset ya vitu bilioni nane kwa kutumia base 24 alphanumeric characters ambazo hazijirudii.
Hili halikai hapa,mfano huu ni mfu. Kisha angalia asili.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, angeumba kila kitu kizuri hakina lawama, lawama isingekuwepo.

Kuwepo kwa lawama ni uthibitisho kwamba Mungu huyo hayupo.
Ukisoma katika elimu ya logic (ambayo mimi siikubali,ila nyinyi ndiyo mnaishi katika mapito hayo) inasema anaye kanusha hutangulizwa dhidi ya yule anaye sadikisha,mimi nasadikisha ya kuwa Mola yupo na ushahidi upo,ila wewe unaye kanusha unatakiwa ututhibitishie ya kuwa umejuaje kama Mola hayupo,yaani ilikuwaje mpaka ukafikia hitimisho hilo.

Wewe umejuaje kama unavyodai ya kuwa angekuwepo angeumba kila kitu kizuri ? Unajichanganya sana,yaai hilo umelijuaje wakati unadai kwamba hayupo ?
 
Ni vizuri umekubali tujadiliane kwenye msingi wa logic (mantiki).

Maana nje ya mantiki, hakuna kujadiliana, ni kelele tu.

Kwa sababu misingi ya kujadiliana inatumia mantiki.

Ukisema Mungu ni mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote, kwa kufuata mantiki, hana tabia wala hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya kufanyika.

Ulimwengu huu unaruhusu mabaya kufanyika.

Hivyo, kimantiki, ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Na zaidi, Mungu huyo hayupo.

Kwa sababu, Mungu huyo kuwepo na kuruhusu ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo ni contradiction.

Ni sawa na kusema mama yake mzazi babu mwenye miaka sabini ni binti mdogo mwenye miaka mitano.

Hapa ni kama mimi nimekuambia hakuna binti wa miaka mitano ambaye ana mtoto wa kumzaa wa miaka sabini, kwa sababu hiyo nincontradiction ya kimantiki.

Halafu wewe unaniuliza, wewe ymejuaje huyo binti hayupo? Kama hayupo umejuaje kuwa hayupo?

Nimetumia mantiki. Mama anatakiwa kuwa mkubwa kuliko mtoto wake. Pia anatakiwa awe kafikia umri wa kuzaa. Binti wa miaka mitano hajafikia umri wa kuzaa. Pia, binti wa miaka mitano hata akizaa kwa miujiza keo, mtoti wake hawezi kuwa na miaka sabini. Hivyo hili jambo la binti wa miaka mitano kuwa na mtoto wa miaka sabini haliwezekani.

Nimetumia mantiki kujua hilo.

Hili jambo haliwezekani kufanyika, ni contradiction inayoonesha hili wazo ni kitu cha kufikirika tu.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote naye ni wazo la kufikirika tu, kiuhalisia hayupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Usiku na asubuhi Chief

Saa 2 usiku na Saa 10 asubuhi ya siku nyingine

Sasa Mtu ule daku Msosi wa nguvu saa 10 asubuhi utashindwa nini kuvumilia mpaka jioni saa 12?

Hakuna kufunga hapo
Kwani maana ya kufunga ninini? Na kwani mnataka tafsiri ya kufunga kwa mujibu ya Uislamu iwe sawa na ya kikafiri?.
Aliye waamrisha Waislamu kufunga ndie huyo huyo aliewaekea muda wa kuanza na kumaliza.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Aliyewaamrisha Waislamu kufunga ni nani?

Jibu kwa uthibitisho.
 
Mleta mada hii kalenda yako ni ya kiarabu naona.
Kufunga sio lazima iwe ramadhani ni wakati wowote.
Dini yako sio dini yangu na dini yangu sio yako ILA dini yangu ni bora kuliko yako na kinyume chake kwako.
 
Miaka yote huwa unajifichia hapo, Ila wewe kama wewe huna uwezo wa kuthibitisha hayupo, ni mpaka uvizie Uzi wa kusema yupo.
 
Wewe sema tu huna jibu, hayo mengine ni blah blah tu za kukwepa swali.

Sent from my TECNO BC1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…