Siku moja Isaac Newton akiwa amekaa chini ya mti wa passion alidondokewa na tunda la passion. Akajiuliza kwanini tunda lidondoke kwenda juu na sio kwenda au kwanini lisidondoke kiulalo ulalo.. Mwisho wa siku aligundua kitu kinaitwa " The Law of Gravity".. Ni wapi Newton alikusanya data za kimahesabu ili kuprove hypothesis yake?
My point is vitu vingine vinahithibitisha vyenyewe.. Uthibitisho upo kwenye vitu vyenyewe. So usikariri. Elewa.
😂😂 Imenibidi nicheke kwanza ulichoandika! Eti Newton alidondokewa na passion fruit? Newton aliishi Uingereza, huko hakuna miti ya passion, hadithi yake inasema ni toloo au epo, yani unavyouliza tu kuwa Newton alitoa wapi data za kimahesabu inadhihirisha hujui historia ya sayansi, ngoja nikueleweshe, iko hivi Newton alitumia data za miaka mingi za unajimu kutoka kwa Johannes Kepler na Tycho Brahe, na akalazimika kugundua hesabu mpya kabisa inayoitwa calculus ili kuthibitisha nadharia yake kwenye kitabu chake cha Principia Mathematica! Hakukaa tu chini ya mti akatunga stori kama unavyofanya wewe sasa hivi hapa.
Point yangu ni kwamba hizo ndoa zinavunjika kwa sababu hazijafuata taratibu za kimila jambo linalo fanya zisitambuliwe na mabibi na mababu.. Zinavunjika kwa sababu ya defects zao zenyewe na sio kwa sababu mabibi na mababu wamekasrika. Yani ni sawa na binti wa miaka 16 atoroke usiku nyumbani kwao aende club. Huko club abakwe. Atabakwa sio kwa sababu ametoroka kwao ila kutwa na madhara hayo kwa sababu ameenda sehemu ambayo sio sahihi kwake Owenda na baba yake hana taarifa.. Baba ake angekuwa na taarifa labda angemuwekea mabaunsa wakumlinda na wabakaji.
Narudia tena: Salimisha ndoa yako kwa mababu zako
Yaani unafananisha taasisi ya ndoa ya watu wazima wawili na mtoto mdogo aliyetoroka nyumbani?
Kisheria na kiuhalisia, hizo defects huwa zinatengenezwa na akili na tabia mbaya za hao wanandoa wenyewe wakiwa hai, sio kwa sababu ya roho za waliokufa zimegoma kuwalinda, umesoma kweli wewe, mbona ni mweupe hivi?
Unachokifanya hapa ni kuzunguka mbuyu tu, hauna hoja yoyote yenye mantiki.
Ground for divorce inajulikana, nayo ni moja tu 👇👇👇
The Marriage has broken down irreparably.. To prove the marriage has broken irreparably, mahakama huangalia vitu vikuu vitatu.
1. Adultery
2. Cruelty.
3. Dissertion.
Nilipo sema uende mahakamani sijamaanisha ukienda mahakamani utakutana na kesi zinazo zungumza kuhusu mkaja wa babu, Ila nimemaanisha uende mahakamani kuona rate ya divorce.
Nimefurahi umetaja vigezo vya mahakama vya adultery, cruelty, na desertion, sasa nikuulize hivi unajua maana ya hivyo vitu?
Hakuna mtu ambaye huwa anasaliti ndoa yake kwa sababu mababu hawamtambui, usaliti ni issue ya tamaa za mtu binafsi, hata ukienda mahakamani kuangalia rate ya divorce, utaenda kuishia kuona tu uharibifu wa tabia za binadamu wa sasa, sio uharibifu unaotokana na kukataa mila. You just proved my point using the law, Ahsante sana.