Sababu za kiroho kwanini ndoa za kanisani (kikristu) na msikitini (kiislamu) huwa hazidumu

Wewe pumzi ya hoja imekukatikia katikati ya uwanja, umeishiwa spana umeamua kukimbilia kwenye kunisalimisha kwa mababu. Ndoa yangu ipo salama sana kwa sababu inaongozwa na akili, heshima, na tabia njema, sio porojo za kusadikika za porini.
Unatumia vigezo gani kusema ndoa yako IPO salama mkuu? Huo utafiti uliufanyia wapi?
 
Enzi za mababu zetu ndoa kuvunjika sio rahisi. Huu utamaduni wa kizungu na kiarabu haueleweki kwani sio jadi yetu. Tulipokea tu bila kuhoji, ukihoji ni dhambi..
 
USIKLIZWE
 
Mbona unahamisha magoli homeboyπŸ˜‚πŸ˜‚ ni dalili za kushindwa hoja
Kama hujafunga ndoa ya kimila, uwezekano wa kulea watoto wa nje ya ndoa ni 45%. Ndoa za kanisani na msikitini hazina adabu
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ Imenibidi nicheke kwanza ulichoandika! Eti Newton alidondokewa na passion fruit? Newton aliishi Uingereza, huko hakuna miti ya passion, hadithi yake inasema ni toloo au epo, yani unavyouliza tu kuwa Newton alitoa wapi data za kimahesabu inadhihirisha hujui historia ya sayansi, ngoja nikueleweshe, iko hivi Newton alitumia data za miaka mingi za unajimu kutoka kwa Johannes Kepler na Tycho Brahe, na akalazimika kugundua hesabu mpya kabisa inayoitwa calculus ili kuthibitisha nadharia yake kwenye kitabu chake cha Principia Mathematica! Hakukaa tu chini ya mti akatunga stori kama unavyofanya wewe sasa hivi hapa.
Yaani unafananisha taasisi ya ndoa ya watu wazima wawili na mtoto mdogo aliyetoroka nyumbani?

Kisheria na kiuhalisia, hizo defects huwa zinatengenezwa na akili na tabia mbaya za hao wanandoa wenyewe wakiwa hai, sio kwa sababu ya roho za waliokufa zimegoma kuwalinda, umesoma kweli wewe, mbona ni mweupe hivi?

Unachokifanya hapa ni kuzunguka mbuyu tu, hauna hoja yoyote yenye mantiki.
Nimefurahi umetaja vigezo vya mahakama vya adultery, cruelty, na desertion, sasa nikuulize hivi unajua maana ya hivyo vitu?

Hakuna mtu ambaye huwa anasaliti ndoa yake kwa sababu mababu hawamtambui, usaliti ni issue ya tamaa za mtu binafsi, hata ukienda mahakamani kuangalia rate ya divorce, utaenda kuishia kuona tu uharibifu wa tabia za binadamu wa sasa, sio uharibifu unaotokana na kukataa mila. You just proved my point using the law, Ahsante sana.
 
Enzi za mababu zetu ndoa kuvunjika sio rahisi. Huu utamaduni wa kizungu na kiarabu haueleweki kwani sio jadi yetu. Tulipokea tu bila kuhoji, ukihoji ni dhambi..
Kasome vizuri mila za makabila yetu. Kwenye makabila mengi tu ya Kitanzania, mwanamke alikuwa akishindwa kuzaa tu au akizaa watoto wa kike tupu, alikuwa anafukuzwa na ndoa inavunjika kienyeji kabisa mbele ya wazee wa kimila! Mbona hiyo huioni kama ni talaka ya kikatili? Utamaduni wetu ulikuwa na mapungufu makubwa sana kuliko unavyotaka kuusafisha hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…