Mohamedy cadinaly
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 2,449
- 2,245
Mods ondoeni huu uzi...maana unaudhi!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwendelezo wa mchongoo....Inaendelea basi kama ujuavyo Congo hasa vijiji vya kitchanga ni vita tu nikalala vile vile chini tuli mpaka wale waasi walivyo pita na asikuambie mtu waasi wananuka sana mana hawaogi.na sura zao zinamakovu ya kutisha basi baada ya kupita wale waasi nikamuita mama nyabadee nikakuta yuko kimya nikajua risasi zimempata basi wakati Huo milio ya risasi inalia kwa Mbali Mbali mimi nikatambaa chini chini ili nikamuone mama nyabadee kama yupo hai Au lah nikatambaa nikafika nikaita mama nyabadee BADO kimya ile nimeingia ndani ya chumba kwa kutambaa nikamkuta yupo chini ya kitanda basi haraka nikamwambia twende tukimbilie kijiji cha nyuma pale tulipo kuta wale wanajeshi wa Congo na mda ule mule chumbani mwa mama nyabadee mulikuwa na panga nikaona hawa waasi watazoea nikabeba lile panga aise ili nikiwakuta njiani ni kukata tu.
Japo najua panga mbele ya ak47 ni uongo lakini kwa ujasiri nilio kuwa nao na licha mule ndani mulikuwa na silaa hiyo hiyo nikaona nibebe hiyo hiyo. Basi tukaanza safari ya kurudi kile kijiji cha nyuma nikiwa na mama nyabadee nyuma nikiwa nimemshika mkono tukatembea wee mana ilikuwa ni BARA bara tu mana short cut way hamna congo ukipita short cut jiandae kukutana na nyoka koboko Au kukutana na kikundi cha waasi kukuteka.
Mana Congo Ina karibia vikundi VYA waasi 204. Basi wakati tupo barabarani na mama nyabadee kwa Mbali tukaona kigari Fulani kama jeep hivi Au wengine hupenda kuita kibanda wazi ile Gari ilikuwa inakuja kwa kasi sana basi tukaona bora tujifiche pembeni mana ile Gari inavyokuja utazani waliko toka wale watu si kwema basi wakati tumejificha ni bora mana tulifanya la maana nikasikia mlio mzito wa lisasi ile Gari ikayumba yumba baadae ikatulia kumbe ilikuwa taili imepigwa risasi nzito ya kivita ikawa imepasua lile taili na baada ya kutulia wale walio kuwepo mwenye Gari lile waliluka chini huku wakiwa na risasi wakaanza kupiga risasi na kumbe walikuwa ni waasi wa Joseph kony wanakimbizwa na wanajeshi wa monusco basi vita ile ilikuwa kali sana nilishuhudia Yule kamanda wa kikosi cha Joseph kony (LRA) akitoa bomu la mkono na kuwatupia wanajeshi wa monusco aise na kweli likawapiga pale pale wanajeshi wawili walipasuka pasuka sijawai ona damu inaruka vile ni hatari Wewe sikiza tu basi lakini wale wanajeshi wengine wa munusco hawa kukata tamaa wakaendelea kurusha risasi wakawapiga waasi watano pale pale wengine wakakimbilia polini na Yule mkubwa wao aise Congo Wewe isikie tu hasa huku Congo goma Au kivu ni hatari sana kifo nje nje waasi kukukata ulimi hawaoni shida.
Basi baada ya mapigano kuisha mimi Na mama nyabadee tukafika pale mpaka palipo kuwa NA Mapigano tukawakuta wanajeshi wa monusco wanasaidiana kuinua wanajeshi wenzao walio jeruhiwa na walio kufa wakatuuliza mmetoka Wapi tukawambia tumetoka kijiji cha nyuma hapo.
Basi ikabidi na sisi tuwasaidie mana pale palijaa damu na utumbo wa wanadamu.
Itaendelea Namaliza yote msihofu jamani huku vita sana hata muda huu nasikia risasi kwa Mbali sana.
Ndio nimefikaDah kulikoni raraa reree na Extrovert hawajatia timu humu hata like
hahahaaaaMwendelezo wa mchongoo....
Kapigwa risasi ya kichwa na m 24.We jamaa umepotea malizia story yetu aisee
.
Katika harakati zangu za kujikomboa na umasikini, niliamua kufanya ziara ya kusaka fursa Mpya nchini Congo. Nilikua tayari nimeshapata masimulizi mengi ya upatikanaji wa madini ya dhahabu na Rubi.
Ni mnamo mwaka Juzi mwanzoni nikiwa mji wa Uvira amabapo jilikutana najamaa Akiwa na jiwe alilo dai kuwa ni Rubi
Baada ya mazungumzo marefu jamaa alikubali kunipa jiwe Moja ambalo alisema kuwa alishawahi kulipeleka Kigali Rwanda lakini katika vipimo ilitoa majibu yanayo Changanya. Ilisoma upande Moja ni Rubi na wakati mwingine inasoma Spinel. Sasa akanionesha ndoo imekaa mawe ya Kila namna. Kazi yangu nilitakiwa kwanza kwenda Tanzania kupima jiwe hilo ili tujue ni aina Gani ya jiwe Kisha nitafute mteja wa Uhakika ambaye tutakuwa tunampa Mzigo.
Kazi hiyo nikaichukua na kuanza safari, sikuhiyo nililala Bujumbura na keshoyake nikalala Kigoma. Asubuhi nilianza safari mpaka Arusha. Pamoja na kuzongwa na matapale na kashkash nyingi nilifanikiwa kufanya vipimo na bahati mbaya jiwe lilikua feki.
Pale Arusha nilikutana na wadau wengi sana na kupewa michongo nankutiwa moyo sana. Nilianza kuiona Dunia ya dealers. Sasa kazi ilaanza kutafuta connection ili nikasake Mzigo. Hapo ndipo safari wa Kivu kaskazini ikaanza.
Kiukweli sikuwa najua mawazo yangu ni hatari kiasi gani lakini laiti ningelijua pengine ningeanza kuungama dhambi zangu kwanza kabla ya kuanza safari katika ukanda wa damu mbichi.
Wakati ukawadia na safari ikaanza, niliambiwa nitafute biashara ya kwenda mayo ili nizugie kuingia mayo maeneo ya ndani na machimboni. Kwanza nikawaza kupeleka Nguo za kiume Jeans za masela na Viatu moka za Bakulutu na Kisha nikafikiria kupeleka Mchele. Baada tathmini jikapeleka Jeans Viatu na Samaki. Nilidhamilia kukutana na kamii ya Kila namna nanjinsia zote nilidhamilia kufa au kurudi na Mali. Militia taarifa za AWALI kujua hata mavazi ninayotakiwa kuvaa nikiwa huko. Nilihakikisha ninachukua kilataarifa Kwa uzito unao stahili.
Nilijifunza kuhisabu na kutaja pesa Kwa kifaransa, ndani ya wiki Moja nilijua kuhesabu Moja mpaka Milioni na kutaja pesa na maneno muhim ya kibiashara. Mfano Congo neno Kuuza wao linamaana ya kununua kuuu. Nipatie, kombola, mbasela na maneno mengine kama kutaja rangi na kusalimia. Bahati ni kwamba Kiswahili Cha Kivu kinafanana sana na Kiswahili Cha Tanzania Bara tofauti na hawachanganyi sana french kama wale wa Lubumbashi na Kinshasa.
View attachment 2497368
Safari ilianza Kwa kupitia Burundi Kisha kuingia mji wa Uvira. Hapo nililala na kesho nikapanda Hiache kwenda Mji wa Bukavu. Nilikua na machaguo mawili aidha kupitia Barabara ya ndani ya Congo au kupitia Rusizi Kisha Rwanda na kurudi tena Congo. Barabara ya ndani ya Congo ni mbaya sana na hatari sana, wanapita watu wahalifu na wanao ogopa ukaguzi wa Rwanda na ukifika unafanyiwa sherehe yaani makorongo na magari kuanguka sio habari tena, kutekwa na kuuwawa ni kawaida kuliko kusaliklmiana. Hii inaitwa Barabara ya Ngomo(Kaburi wazi)
Changamoto ya kupitia Rwanda, ukiwa na Visa ya Dola 50 basi ukiingia Rwanda Visa ya Congo imeisha na ukitaka tena kuingia Congo Kwa kutokea Barabara mchepuko ya Rwanda basi utalazimika kulipia Visa tena, kwahiyo kupitia njia hiyo utalipa Dola 200 kwenda na kurudi. Suluhisho ni Visa ya Dolar100 ambayo unapewa miezi mitatu na unaweza kutoka Congo na kuingia kadili uwezavyo. Hilo nilisha lifuatilia mapemaa, nikawa na Visa ya Dola100 nikapita Rwanda. Kuna mengi hapa Rwanda lakini kwakua sio mada ya Leo itoshe kusema ni Dunia tofauti sana. Tuishi bongo tu, amani inatosha.
Sasa niliingia mjini Bukavu kupitia mpaka wa Rusizi. Pale Bukavu wakati nimeingia nikakuta watu wanafunga maduka na kukimbia kujificha, nilipojaribu kuuliza wakasema Kuna vita imetangazwa M23 wanaingia Leo. Hapo nilitetemeka sana, nikawaza nirudi Rwanda lakini ukaguzi na Mahojiano ya Rwanda yalinipa hofu, maana ilifika wakati nashuhswa kwenye gari nafanyiwa Mahojiano maalum . Nilishangaa Kila yulipopita nakuta askari wanajua Kuna Mtanzani Yuko kwenye gari. Nilikua nahojiwa Kwa muda mrefu mpaka abiria wanalalamika, abiria Wote walikua Wakongo na karoko mswahili Mimi, askari wa Rwanda hawamuelewi wanashangaa Mtanzani kupitia pale.
Sasa Hali Ile ilinipa hofu ya kurudi Rwanda na nikakumbuka adhima yangu Bado, safari yangu Bado na lazima nifike.
Hapo nilisajili lakini ya Simu na kuweka vocha niajiunga mitandao yote na kupata dakika 3 Kwa Buku...
Haraharaka nikapita mtu wa toroli wao wanapita shareti, nikapakia mizigo tukaelekea Bandarini. Kutoka Bukavu kwenda Guma Kuna ziwa Kivu hapo unapanda meli usiku Kucha unafika kesho Asubuhi. Lengo langu niondoka Bukavu na usiku niwe kwenye meli ili hata vita ikitokea Mimi nakua kwenye meli.
Bandarini nilikuta Meli nyingi ila nikaamua kupanda "Emanele04" waniita Emauele katre, hii Bei yake Iko juu na wanapanda watu wenye uwezo na mabishoo. Lengo langu nilitaka kuanza kukutana na watu ambao wanaweza kunipa michongo ya machimbo au kupata connection za dealer wazuri. Katika safari yangu nilikua mkimya sana kwani Kila nilipo jaribu kuongea watu waligeuka kunitazama, nikagindua Kiswahili changu kinaniumbu jambo ambalo sikulitaka hasa kulingana na treatment ya Wanyarwanda.
Usiku niliingia Club na kukaa Kwa muda Kisha nikarudi, mpaka wakati huo sikupata mtu wa kuanza mazungumzo naye. Tukiwa njiani upande Moja nchi kavu kulikuwa Giza huko ni Congo kisiwa kinaitwa Idjwi na upande mwingine Kuna mataa sana, huko ni Rwanda na mataa yale ni miji na vijiji.
Asubuhi tulifika Bandarini Goma. Hapo nilikuwa makini kuangalia watu wenye mizigo kama yangu hasa samaki ili nijue wanako wapeleka. Kuna dada Moja alikua na Samaki mwengi. Niliadhimia kujiweka karibu yake. Wakati anapakia kwenye gari kupeleka stoo ndipo nikasogea na kumuomba anipakilie Mzigo wangu nitachangia garama, dada yule alikubali na Alipo niuliza napeleka wapi nikamwambia Kuna mtu tutamkuta hapo mbele ndiye anajua stoo ilipo, lakini haikua kweli.
Tulienda mpaka nakoenda yeye, na tukiwa njiani nilikwambia ukweli kuwa sina stoo Bali nimekuja tujaribu biashara. Alipo niuliza Bei za Samaki Tanzania nilimdanganya nikamwambia Bei ya chini sana kiasi akawa anatamani nimpeleke huko chimbo. Leongo langu lilitimia na tulipo fika stoo kitu cha kwanza alimueleza mume wake kuhusu Bei za Samaki Tanzania na kuanzia hapo hao wakawa weneji wangu. Kesho yake nilizunguka mjini Goma mpaka sehem inaitwa Bireree hapo ni mjini na ndipo mpakani na Gisenyi Rwanda, yaani border Ile Iko kama ilivyoisha Tunduma na Nakonde Zambia. Nyumba zimeungana za Rwanda na Congo. Soko na mishe nyingi ziko upande wa Congo . Asubuhi Wanyarwanda wanavuka kufungua biashara zao huko Goma ni jioni kurejea kwao.
Muda ndio huu Sasa ebu simulia mzeeNadhan huyu jamaa akimaliza ntasimulia ya mgodin