Safari yangu "Kitchanga" mji uliotekwa M23

Inaendelea basi kama ujuavyo Congo hasa vijiji vya kitchanga ni vita tu nikalala vile vile chini tuli mpaka wale waasi walivyo pita na asikuambie mtu waasi wananuka sana mana hawaogi.na sura zao zinamakovu ya kutisha basi baada ya kupita wale waasi nikamuita mama nyabadee nikakuta yuko kimya nikajua risasi zimempata basi wakati Huo milio ya risasi inalia kwa Mbali Mbali mimi nikatambaa chini chini ili nikamuone mama nyabadee kama yupo hai Au lah nikatambaa nikafika nikaita mama nyabadee BADO kimya ile nimeingia ndani ya chumba kwa kutambaa nikamkuta yupo chini ya kitanda basi haraka nikamwambia twende tukimbilie kijiji cha nyuma pale tulipo kuta wale wanajeshi wa Congo na mda ule mule chumbani mwa mama nyabadee mulikuwa na panga nikaona hawa waasi watazoea nikabeba lile panga aise ili nikiwakuta njiani ni kukata tu.

Japo najua panga mbele ya ak47 ni uongo lakini kwa ujasiri nilio kuwa nao na licha mule ndani mulikuwa na silaa hiyo hiyo nikaona nibebe hiyo hiyo. Basi tukaanza safari ya kurudi kile kijiji cha nyuma nikiwa na mama nyabadee nyuma nikiwa nimemshika mkono tukatembea wee mana ilikuwa ni BARA bara tu mana short cut way hamna congo ukipita short cut jiandae kukutana na nyoka koboko Au kukutana na kikundi cha waasi kukuteka.

Mana Congo Ina karibia vikundi VYA waasi 204. Basi wakati tupo barabarani na mama nyabadee kwa Mbali tukaona kigari Fulani kama jeep hivi Au wengine hupenda kuita kibanda wazi ile Gari ilikuwa inakuja kwa kasi sana basi tukaona bora tujifiche pembeni mana ile Gari inavyokuja utazani waliko toka wale watu si kwema basi wakati tumejificha ni bora mana tulifanya la maana nikasikia mlio mzito wa lisasi ile Gari ikayumba yumba baadae ikatulia kumbe ilikuwa taili imepigwa risasi nzito ya kivita ikawa imepasua lile taili na baada ya kutulia wale walio kuwepo mwenye Gari lile waliluka chini huku wakiwa na risasi wakaanza kupiga risasi na kumbe walikuwa ni waasi wa Joseph kony wanakimbizwa na wanajeshi wa monusco basi vita ile ilikuwa kali sana nilishuhudia Yule kamanda wa kikosi cha Joseph kony (LRA) akitoa bomu la mkono na kuwatupia wanajeshi wa monusco aise na kweli likawapiga pale pale wanajeshi wawili walipasuka pasuka sijawai ona damu inaruka vile ni hatari Wewe sikiza tu basi lakini wale wanajeshi wengine wa munusco hawa kukata tamaa wakaendelea kurusha risasi wakawapiga waasi watano pale pale wengine wakakimbilia polini na Yule mkubwa wao aise Congo Wewe isikie tu hasa huku Congo goma Au kivu ni hatari sana kifo nje nje waasi kukukata ulimi hawaoni shida.

Basi baada ya mapigano kuisha mimi Na mama nyabadee tukafika pale mpaka palipo kuwa NA Mapigano tukawakuta wanajeshi wa monusco wanasaidiana kuinua wanajeshi wenzao walio jeruhiwa na walio kufa wakatuuliza mmetoka Wapi tukawambia tumetoka kijiji cha nyuma hapo.

Basi ikabidi na sisi tuwasaidie mana pale palijaa damu na utumbo wa wanadamu.

Itaendelea Namaliza yote msihofu jamani huku vita sana hata muda huu nasikia risasi kwa Mbali sana.
 
Justine Marack umeamua kuacha kumalizia ulipoanzia kama ulipitia changamoto za congo kama ulivyotuadithia vipi maneno ya wanaJF yaondoe utimamu wa kijana mwanaume na aliepitia mazito makubwa kwe taifa lenye vita lisilo lako?

Mzee lete muendelezo amini kesho mwanao au mtoto wa dada Yako kama sio mjukuu wako atakuja kusoma hapa na atajifunza kitu na utakuwa umemsaidia bila kudhan yaleo kuwa Kuna kesho hii simulizi inaweza kusaidia Moja ya damu Yako hapa Dunian.

N ombi tuu mzee
 
Mwendelezo wa mchongoo....
 
Mzeiya malizia stori basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…