Hili la safari za nje siwezi kulizingumzia lakini la kujiita Dr ni kutokana na ukweli kwamba amepewa hizo doctorate za heshima (Honoris Causa). Hivyo basi ana haki ya kuchagua kuzitumia katika kumu-adress. Kuna wengine wanaopata doctorate lakini hawapendi watambulike kama Dr. Umetoa mfano wa Mwl Nyerere. Huyu kweli hakupenda aitwe Dr, lakini kwenye miaka ya michache baada ya uhuru alikua akiitwa Dr. Baadae alikuja akaweka zuio la kuitwa Dr na akataka aitwe Mwalimu. Hivyo Kikwete ana haki kabisa ya kupenda aitwe Dr. Na kumbuka kwamba sio lazima mtu awe amesomea udaktari. Hata hizi doctorate za heshima zinaweza kutumika kumtambulisha mtu.
Nitakupa mifano ya viongozi wengine ndani na nje ya Tanzania ambao wanatambulika kwa hizo honorary doctorate zao:-
1. Dr. Salim Ahmed Salim - Tanzania
2. Dr. Kenneth Kaunda - Zambia
3. Dr. John Garang (R.I.P) - South Sudan
4. Dr. Jonas Savimbi (R.I.P) - Angola
5. Dr. Reginald Mengi - Tanzania
6. Dr. Henry Kissinger - USA
Hawa wote wanatumia utambulisho wa honorary doctorate zao. Lakini kuna viongozi wengine hawapendi kuzitumia. Umewataja Ally Hassan Mwinyi, John Malechela, Benjamim Mkapa. Lakini kuna wengine kama Getrude Mongela, Anna Mkapa, n.k. Hivyo ni suala la hiari na yule anayeamua kutumia honorary doctorate yake ni bora uamuzi wake uheshimiwe sawa sawa na uamuzi wa yule anayeamua asiutumie. Swali kwako Jason Bourne, endapo utapata bahati ya kutunukiwa doctorate, utaitumia katika utambulisho wa jina lako au vipi?