Wana bodi salaam.
Uzi huu ni maalumu kwa ajili ya kuratibu safari za Mh Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ameapa kuwa rais kwa mujibu wa katiba kufuatia kifo cha hayati dKT John Pombe Joseph Magufuri march 17.03.2021. Kwa mujibu wa katibu makamu wa Rais anashika madaraka ya urais na ndipo hapo march 19, 2021 aliapa kuwa Rais wa Sitta wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
SAFARI ZA KIMATAIFA
01. Tarehe 11,04.2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda alipokutana na mwenyeji wake Jenerali Kaguta Msevin katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kusafirisha mafuta ghafi toka Hoima Uganda hadi mkoani Tanga.
02. Tarehe 04.05.2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya. Pamoja na kuktana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, pia atahutubia mabunge yote ya Kenya. Ziara yake inatarajiwa kutatua msuguano wa kidiplomasia ambao umekuwepo kwa muda mrefu.
03. Tarehe 22.06.2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassani, ametua nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC.
Picha rasmi za Mh Rais