Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021

Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021

Tumtieni moyo Rais ili afanye kazi vizuri bila wasiwasi wowote. Ana makinda yapatayo million 60 yote yakiwa yameachama midomo, na kila kinda inabidi alitemee chakula midomoni yeye mwenyewe ili liweze kula na kushiba.
 
Kwa hiyo tunaweza kusema ni wastani wa safari moja kila mwezi. Kama sikosei Uganda kishaenda mara mbili kwa hiyo jumla ya safari za nje zinatakiwa ziwe nne, labda zimekuwa chache kutokana na COVID-19 Viongozi wa nchi za nje wanahofia kualika Viongozi kutoka nchi nyingine.
Nikumbushe tarehe ya kwanza ya safari ya uganda
 
  • Thanks
Reactions: BAK
View attachment 1749075

Habari za Kazi wana JamiiForums,

Katika thread hii nategemea tutaangazia ziara mbalimbali(Za nje ya nchi) za Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na manufaa kwa taifa.

Leo tarehe 11 April 2021 Mhe Samia anafanya ziara yake ya kwanza nje ya Tanzania na ziara hii ina lengo la kusaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta.

Tarehe 4 mei2021 Mhe Samia amezuru nchi ya Kenya na kuwahitubia wananchi wa Kenya.
Ni ziara yenye tija kwa uchumi wa Nchi. Aidha ikumbukwe mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mpenzi wa ziara za nje ya nchi na mara nyingi alimtuma Mhe Samia Suluhu kumuwakilisha.

TUTAENDELEA KUTOA UPDATES YA ZIARA ZA NJE ZA MH RAIS SAMIA.
01. Tarehe 11,04.2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda alipokutana na mwenyeji wake Jenerali Kaguta Msevin katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kusafirisha mafuta ghafi toka Hoima Uganda hadi mkoani Tanga.

02. Tarehe 04.05.2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya. Pamoja na kuktana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, pia atahutubia mabunge yote ya Kenya. Ziara yake inatarajiwa kutatua msuguano wa kidiplomasia ambao umekuwepo kwa muda mrefu.

03. Tarehe 12.05.2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Kaguta Mseven ambaye ameapa kuwa rais kwa muhula wa sita mfululizo.

04. Tarehe 22.06.2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassani, ametua nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC.
 
View attachment 1749075

Habari za Kazi wana JamiiForums,

Katika thread hii nategemea tutaangazia ziara mbalimbali(Za nje ya nchi) za Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na manufaa kwa taifa.

Leo tarehe 11 April 2021 Mhe Samia anafanya ziara yake ya kwanza nje ya Tanzania na ziara hii ina lengo la kusaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta.

Tarehe 4 mei2021 Mhe Samia amezuru nchi ya Kenya na kuwahitubia wananchi wa Kenya.
Ni ziara yenye tija kwa uchumi wa Nchi. Aidha ikumbukwe mtangulizi wake Hayati Dr. John Pombe Magufuli hakuwa mpenzi wa ziara za nje ya nchi na mara nyingi alimtuma Mhe Samia Suluhu kumuwakilisha.

TUTAENDELEA KUTOA UPDATES YA ZIARA ZA NJE ZA MH RAIS SAMIA.
TEAM JIWE KAZINI
 
Karibuni kwenye mada.

Mtakumbuka tangu mheshimiwa rais MagufuliJP aingie madarakani ameniwekea record ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amesafiri mara chache mno tena ndani ya Africa tu. Hajawahi kutoka nje ya bara la Afrika kwa safari za kikazi tangu awe rais.

Mama Samia Suluhu Hassan tangu ameapishwa March 2021 ameanza safari ambazo hasa zina lengo la kukuza mahusiano na nchi yetu. Naomba sasa tuanze kuweka records za safari zake tangu awe Rais.

1. Alisafiri kwenda nchini Uganda kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni kwaajili ya kusign mkataba wa bomba la mafuta
2. Safari ya pili ilikuwa nchini Kenya ambapo alialikwa na Rais Uhuru Kenyatta
3. Safari ya tatu nchini Uganda kwa uapisho wa Rais Museveni
4. Msumbiji kwa safari ya kikao cha wakuu wa nchi za SADC
5. Nchini Burundi kwaajili mwaliko wa Rais wa Burundi.

6. Tuendelee hapa kuandika record sawa
 
Cha muhimu ni kuwa Safari zinatija?
Yule jamaa hakusafiri kwa sababu mbili
1.Afya mgogoro
2.Lugha gongana
3.Uoga wa maswali ya wanahabari
 
Mama anajaribu kurudisha marafiki waliotukimbia kipindi cha yule mzee,hii ni nzuri kwa maendeleo yetu
 
Tanzania ni nchi ya watu walalamishi na ndio maana viongozi wasio na uvumilivu wanaweza kuishia kuburuza sana watu.
Bahati mbaya pamoja na kipawa hicho cha ulalamishi, watu wake wengi hawana uwezo wa kuchukua hatua yoyote dhidi ya lile wasilolipenda!
Hii mada ni mfano wa ulalamishi.
 
Cha muhimu ni kuwa Safari zinatija?
Yule jamaa hakusafiri kwa sababu mbili
1.Afya mgogoro
2.Lugha gongana
3.Uoga wa maswali ya wanahabari
Na alimtumia huyu huyu SSH kama msaidizi wake. Alikuwa akimuandaa pengine pasipo yeye mwenyewe kujua.

JK alisafiri zaidi ya safari 400 kwa miaka yake kumi ikulu, faida ya safari ni kubwa, MOI ikiwa mojawapo, mwendo kasi pia.
 
Watanzania katika ubora wao,kulalama kwenye social networks!!!President Samia kwangu ur doing good job and keep it up
 
Ndugu zangu kwa wale waliokuwepo humu kwa miaka mingi, kulikuwa na uzi uliokuwa unafuatilia safari za rais Kikwete na gharama za safari zake.

Natoa wito wa menejimenti ya JamiiForums kufuatilia ziara zote, gharama na faida tunazopata kama nchi.

Ahsanteni
 
Nashauri huwe huu umodify kidogo maana bado safari hazijawa nyingi
 
Ndugu zangu kwa wale waliokuwepo humu kwa miaka mingi, kulikuwa na uzi uliokuwa unafuatilia safari za rais Kikwete na gharama za safari zake.
Natoa wito wa menejimenti ya JamiiForums kufuatilia ziara zote, gharama na faida tunazopata kama nchi.

Ahsanteni
Ili?
 
Back
Top Bottom