Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021

Mama Samia ana kazi sana. Wengi wanampima huku reference point ikiwa JPM. Ndiyo shida ya kukamata uongozi huku mtangulizi wako akiwa amefanya mambo makubwa makubwa.
Huyo Jpm kafanya kubwa gani zaidi ya kupora korosho za watu huko kusini??
 
Reactions: BAK
tayari nimeupdate
 
Huu uzi ni wa muhimu sana.

LAKINI, kama wapo washauri wa Rais wahakikishe wanamshauri kuwa makini sana na Wakenya.

Ninasema hivi kwakuwa ninawafahamu vizuri wakenya na jinsi wanavyotuchukulia kiuhalisia

Wakenya wanaipenda Tanzania kimaslahi na kidhulma tu na si vinginevyo, hawana ujirani au urafiki wanaouzungumza.

J.P Magufuli alikuwa na mabaya yake lakini alifanya vizuri kwa kuhakikisha Wakenya hawachukui fursa za watanzania katika nchi yetu, hawaimport bidhaa ambazo hata sisi tunaweza kuziunda nchini

Hawachukui ajira za watanzania ambao nao sana sifa katika hizo ajira kama ualimu wa English medium school, International school, Hotel managements etc. ambazo walikuwa wamezishikilia wa LAKINI kule kwao hawatuajiri Watanzania.
 
Mama anapaswa kuzunguka sanaaa sanaaaa tu kuziba magape yaliyotengenezwa na awamu iliyopita, tunaihitaji sana dunia.
 
Watanzania kwenye hizo industry tunajiroga wenyewe mjomba, customer care zetu ni mbooovu kupindukia hatuna hospitality na hatuko charming hata kidogo yani kiujumla ni hatujali kabisa full ubabaishaji wacha wakenya wa zitumie hizo nafasi maana mchawi siyo Kenya bali tabia zetu wenyewe.
 
Ila awe mwangalifu na manyang'au!! Mwanzoni sikujua kumbe unyang'au huko knya ni sifa ya kujivunia!!
 
Huu ndio uongozi unaenda kubadilishana mawazo na wenzio ,sio unakaa tu nchini kufanya vitimbi vya ajabuajabu kama mwendazake .
 
Safari ya tatu. Rais Samia Suluhu Hassan, amefika Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa mh Kaguta Museveni aliyemshinda Bob wine kwa asilia 58%.

Hii ni safari ya tatu tangu awe rais
 
Safari ya tatu. Rais Samia Suluhu Hassan, amefika Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa mh Kaguta Museveni aliyemshinda Bob wine kwa asilia 58%.

Hii ni safari ya tatu tangu awe Rais wa JMT
 
Safari ya tatu. 12.05.2021 Rais Samia Suluhu Hassan, amefika Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa mh Kaguta Museveni aliyemshinda Bob wine kwa asilia 58%.

Hii ni safari ya tatu tangu awe rais
 
Safari ya tatu. 12.05.2021 Rais Samia Suluhu Hassan, amefika Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa mh Kaguta Museveni aliyemshinda Bob wine kwa asilia 58%.

Hii ni safari ya tatu tangu awe rais
Huuu uzi utakuwa na Pages zaidi ya 1000 mpaka kufikia Oktoba, 2025 wakati wa Uchaguzi Mkuu. Naombea sana Nchi yangu asitokee VASCO da Gama mwingine baada ya Baba Riz
 
Huuu uzi utakuwa na Pages zaidi ya 1000 mpaka kufikia Oktoba, 2025 wakati wa Uchaguzi Mkuu. Naombea sana Nchi yangu asitokee VASCO da Gama mwingine baada ya Baba Riz
Huyu mama kama siyo masharti ya corona anaweza kuwa Vasco dagama
 

01. Tarehe 11,04.2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda alipokutana na mwenyeji wake Jenerali Kaguta Msevin katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kusafirisha mafuta ghafi toka Hoima Uganda hadi mkoani Tanga.

02. Tarehe 04.05.2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya. Pamoja na kuktana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, pia atahutubia mabunge yote ya Kenya. Ziara yake inatarajiwa kutatua msuguano wa kidiplomasia ambao umekuwepo kwa muda mrefu.

03. Tarehe 12.05.2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, afanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Uganda kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Kaguta Mseven ambaye ameapa kuwa rais kwa muhula wa sita mfululizo.

04. Tarehe 22.06.2021, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassani, ametua nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC.

 
Reactions: BAK
Ya tatu hii, ndani ya siku 90 tu.
 
Kwa hiyo tunaweza kusema ni wastani wa safari moja kila mwezi. Kama sikosei Uganda kishaenda mara mbili kwa hiyo jumla ya safari za nje zinatakiwa ziwe nne, labda zimekuwa chache kutokana na COVID-19 Viongozi wa nchi za nje wanahofia kualika Viongozi kutoka nchi nyingine.
Mkuu, update kwa kutaja namba. 1,2,3 etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…