Sakata la BANDARI ZETU na DPW linataka kuliingiza Taifa kwenye umwagaji wa damu!?

Samia kama alikuwa na nia njema na sio ovu angewapa Waarabu TTCL na kisiwa cha Pemba ambapo kuna umasikini wa hali juu. Samia hana nia njema na Bara nashangaa sana akina Kitenge na mkuu wa nyumba ya mbumbumbu kuona ni sahihi kuitoa Bandari zote kwa Waarabu huu ni ujinga wa hali ya juu.
 
Hakuna damu itakayomwagika kwenye nchi hii...tulieni muuzwe kwa step..
 
Boss Mshana,tupe mtizamo wako kuhusu ishu hii ya DP World,je,kuna manufaa kweli kwenye ule mkataba? (Naamini wewe ni mzalendo hivyo huwezi kuongopa).
 
Tuzidi kuliombea taifa na kuwaombea wote wenye mapenzi mema na Tanganyika yetu
SERIKALI imeagiza vyombo vishungulike kikamilifu na Wakili Boniface Mwabukusi kutokana na Wakili huyo kudaiwa kutoa matamshi yanayohatarisha amani nchini.

Agizo hilo la Serikali limetolewa leo tarehe 9.7.2023 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega, Japhari Kubecha ambapo pia amekiagiza Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS kuchunguza kwa kina uhalali wa muhuri wa wakili huyo.

Katika siku za karibuni Wakili Mwabukusi amekuwa akitoa matamshi mbalimbali kuhusu mkataba wa bandari na tayari ameshafikisha shauri hilo Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.

"Naomba chama cha Wanasheria Tanganyika TLC wachunguze kwa kina Uhalali wa Muhuri wake,Huyu wakili hakuna wakili wanamna hii... wapo wanasheria wabobezi wametoa maoni yao tena wakiwa Kintume na serikali lakini hawakufikia kiwango hiki cha Kuvunja Utu wa watu,Umoja wa Kitaifa,Amani na Mwenendo wa Nchi.

Vyombo vishughulike kikamilifu juu ya Mtu huyu" amesema Kiongozi huyo wa Serikali, Japhari Kubecha.
 
Wewe mtu wa Same unahoji kuhusu Bandari na wazaramo wahoji nini au yale mamilima yenu yasiyo na faida? Mshamba mmoja unahoji bandari ambayo hujawahi hata kuitumia. Hiki kimbelembele unakipata wapi hasa.
....Akili, Matope, ndugu yangu ? Wewe ni Mtanganyika au Muarabu ?
...Sasa wewe Mzaramo was Pwani una Uchungu Gani na Mlima Kilimanjaro ??
Kweli, Kuna Watu walembashwa Asali [emoji35]
 
we ndiyo umetishika, nani wa kumwaga damu? acheni stori za kitotot
...Kwani Vita ya Wenyewe Kwa Wenyewe inaanzaje Kwa Wengine ? Wanaenda ? Rwanda Walipenda ? SI Ujinga huu huu wa Watu kufanya Wenzako Wajinga, na Vyombo vya Habari vikapepea moto ? Sisi nani yasitukute ? [emoji35]
 
It is well with thee...Simama na haki na Mungu atakuwa pamoja na kila aliye upande wa HAKI
 
Swali langu ni dogo tu, ikawaje huu mkataba uka leak? Maana mikataba ya nchi hii inafichwaga kusiko julikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…