Kwema Wakuu!
Serikali haitahusika Kwa namna yoyote Ile Ikiwa haikuandika barua Wala Kûtuma email kwenda Kampuni ya Tigo kutaka kuingilia faragha na tàarifa za LISU.
Mambo ya serikali Kwenda Kwa makampuni au mashirika hufanywa kiofisi na barua lazima ihusike.
Mawasiliano yoyote àmbayo hayatahusisha njia rasmi huweza kuleta mkingamo wq kisheria.
Hivyo itasemwa kwamba kulikuwa na genge la Watu weñye Maslahi binafsi nje ya serikali àmbalo ñdilo liliwasiliana na Kampuni ya Tigo kutaka tàarifa za LISU.
Hii inatoa Somo Kwa wafanyakazi na Wamiliki WA makampuni kuwa Makini Wakati wanapata oda au maigizo Kutoka kwèñye mamlaka za kiserikali. Kwamba maagizo hayo yawe Kwa njia Rasmi ikiwemo kuandikwa Kwa barua kama ushahidi.
Haya
Robert Heriel Mtibeli kumbuka hili...
## Msingi wa tatizo ni kesi ya "jaribio la mauji ya kisiasa na tendo la kigaidi" alilotendewa mwanasheria, mwanasiasa, mwanaharakati mkosoaji mkuu na mashuhuri Tanzania Mh. Tundu Lissu wa sera na mipango ya serikali chini ya CCM kwa miaka zaidi ya 20 sasa...
Maswali makubwa ambayo kila mtu hujiuliza ili kupata majibu yasiyo na shaka ni:
1. Ni kwanini walitaka kumuua mtu huyu...?
2. Nani alitoa amri ya kuuwawa mtu huyu..?
3. Kina nani walihusika kupanga na kutekeleza shambulio hilo...?
4. Kwanini Vyombo vya kisheria vya serikali ya Tanzania i.e Police, DCI, DPP nk vimeshindwa kutenda wajibu wao wa kisheria na kikatiba kuchunguza na kuchukua hatua? Nani anawazuia kutenda wajibu wao..?
##Kwa ushahidi ambao umeanza kuchomoza, TIGO kampuni ya mawasiliano ya simu chini ya mmiliki wake Millicon/Honora, kwa kutumia mifumo yao (hawa TIGO) ya mawasiliano ambayo victim Tundu Lissu ni mteja wao inaonesha walikuwa sehemu ya wawezeshaji wa unyama huu wa mauaji kwa njia moja au nyingine....
##It doesn't matter whether walikuwa na mawasiliano rasmi na mtuhumiwa namba 1 (serikali) au la. Hili litajulikana tu kwa taarifa ya uchunguzi mahususi uliofanywa na Mr. Michael Clifford anaoutumia kama ushahidi kudai yake haki yake toka kwa Millicon/Honora/TIGO (T) ambao anaendelea kuutoa mahakamani huko Uingereza....
NOTE:
√. Kwa maoni yangu, naweza kukubaliana na hisia zako kuwa, obvious serikali nzima haikuhusika isipokuwa watu wachache, wakubwa, wazito na wenye mamlaka na maamuzi makuu ndani ya serikali walioamua kuvunja sheria na katiba na kutumia vibaya mamlaka yao (abuse of power) kwa maslahi yao binafsi ya kisiasa kutenda tendo baya kabisa la kinyama (barbaric) la kumuua mtu huyu (Tundu Lissu) kwa sababu tu anahatarisha (jeopardize) mipango na maslahi yao hayo ya kisiasa....
√. Hawa ndio wanaotakiwa kujulikana ili hatua za kisheria dhidi yao ziwalalie na huyu mtu (Tundu Lissu) aweze kutendewa vyema na kupata haki yake. Na TIGO mpaka hapo wako kwenye position nzuri ya kufumbua fumbo hili kwa msaada wa Mr Michael Clifford....