Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Kama wewe ulivyo tapeli. Tanzania Ina wachungaji wangapi?. Unawafahamu wachungaji wangapi?. Yani kisa Mwalimu mmoja kazaa na mwanafunzi, ninaconclude walimu wote wazinzi. Yani unashindwa kutofautisha Kati ya cult leader na mchungaji. Mitume na manabii wafanyeje uchafu wewe umekalia wachungaji wote matapeli.
Mimi naona wewe una conflict of interest dhidi za mfalme zumaridi..kwakuona makanisa haya ya watu binafsi yanapata waumini wengi na wewe ulio kwenye mfumo ya makanisa ya wazungu unakosa sadaka kili uchwao hali inakua ngumu kwa kukimbiwa na waumini..ndio mana una hasira dhini ya makanisa binafsi.

Watu wameona ni wale wale wapigaji tu ila mfumo unatofautinana..bora huku watapata miujiza kuliko kwenye matumaini hewa ya kuambiwa toa sadaka usali sana utafanikiwa huku ninyi mkineemeka na kuneemesha makanisa ya wazungu kupitia mifumo yao.

Acha waswahili wafungue makanisa mengi zaidi tutajirishane humu humu ndani..kama inakuuma sana join nao kama huwezi kaa kimya..mana na wewe ni zombi kwa namna yako.

Usimpige mawe mbwa aliyekuja kwenye sherehe huenda alichokifuata na wewe ndicho ulichokifuata.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhalifu hawi mhalifu hadi pale itakapothibitika!

Sakata la mfalme Zumaridi (Kiongozi wa kanisa la Zumaridi huko Mwanza) Linaacha midomo wazi kwa wapenda haki na utii wa sheria!

Sipo hapa kumtetea Mfalme Zumaridi, Bali nashangaa namna ya uharamu wa ukamtaji!

Taratibu za ukamataji kwa mujibu wa sheria ziko wazi kabisa lakini mamlaka zimekuwa zikionesha kufeli Mara kwa Mara kutekeleza sheria hiyo jambo ambalo limekuwa likitweza utu wa watu wasio na hatia.

MFANO! mambo kama haya yalitokea huko mtwara hadi kufedhehesha uongozi wa polisi ambayo yalianza hihivi kwa kufumbafumba mambo,

Mfano 2. Ni huko ARUSHA Kuna taarifa ya askali mzalendo kulalamika kutaka kuuwawa na polisi wenzake kwa mambo Yale Yale kama ya mtwara na serikali iko kimya.

SASA NI HILI SAKATA LA TATU LINALOTIA KICHEFCHEFU

Ni TUKIO LA zumalidi Siku ya kwanza inaripotiwa kwamba polisi waliruka ukuta/geti ili kuingia kwa Zumalidi! Kitendo hiki kilitakiwa kulaaniwa na kila mtu! (Waliruka kwa Zumalidi kesho wataruka kwako)

Kama kulikuwa na ulazima wa kufika pale kwanini hawakufuata utaratibu wa upekuzi unavyotaka? Kwanini hawa kumshirikisha mwenyekiti wa mtaa/mjumbe? Kwanini waliruka ukuta kama jambazi! (VIPI KAMA ZUMARIDI ANGEJIBU MASHAMBULIZI KWA KUFYATUA RISASI KWA POLISI ALIYEVAA KIRAIA ALIPORUKA UKUTA?) Ina maana wangejibu kwamba walikuwa kwenye mapambano na majambazi au?

Kwa utaratibu walio utumia polisi hauna tofauti na utarabu wa kijambazi! Na hili linachangia sana siku hizi RAIA kutokutofautisha kati ya jambazi na polisi.

Tukiachana na mbinu ya ukamataji!

Riport ya polisi ina ukakasi mkubwa juu ya mtuhumiwa Zumaridi!

Kosa walilo utaarifu Umma kwamba anasafilisha BINADAMU 149, kosa hilo Linatia aibu nyingine!

Hivi tangu lini watu wanaokusanyika kusali pamoja imekuwa kosa la jinai?

Mbona jumuiya na taasisi kibao tunawaona wanakusanyika na kukesha na haijawahi kutajwa kuwa ni kosa?

Zumalidi kasafirisha binadamu kutoka wapi kwenda wapi kwa lengo gani? Kuna jinai gani pale?

Hapo taifa juzi wakatoliki walikusanyika mbona haikutamkwa kuwa ni usafirishaji wa binadamu?

Kina mwingira na wachungaji kibao Tanzania kila kutwa wanakusanya watu na haisemwi ni usafirishaji,

INAKUWAJE JAMBO LILE LILE LIWE HALALI KWA MWAMPOSA LAKINI LIWE HARAMU KWA ZUMARIDI?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Nawashauri TAKUKURU WAINGILIE KATI!
Haiwezekani sheria zipo wazi, kwanini zisingefuatwa kama kweli ZUMALIDI anamakosa makubwa hivyo!

Mimi kwa utashi wangu nahisi sakata la Zumaridi lina maslahi binafisi!

TUKIRUHUSU HAYA YA UKIUKWAJI WA SHERIA HAKUNA ATAKAYEBAKI SALAMA!

Itakuwa mtu akikosana na polisi wanakuja kuluka ukuta! Na majambazi nao watatumia mwanya huohuo kufanya uharifu!
Ni Sawa tu, unaweza je kuwa mfalme kwenye nchi yenye Rais? Pumbavu kabisa
 
Kwani hao watu 149 walikuwa kwenye nyumba ya ibada? If not; hauwezi kuwalinganisha na Mwamposa au Wakatoliki wanaokuwa sehemu rasmi ya ibada.
Nyumba ya ibada ipoje.
Vipi wakatoliki wanaokusanyika nyumbani kwa muumini kusali ibada za jumuiya wanaomba wapi kibali.
 
Kinachotutesa watanzania ni chuki binafsi . Kama sheria zipo kwanini zisifuatwe katika ukamataji.
 
L & R ni matokeo ya elimu yetu na wengne ni matokea ya jamii na sehemu tumetoka
 
Nyumba ya ibada ipoje.
Vipi wakatoliki wanaokusanyika nyumbani kwa muumini kusali ibada za jumuiya wanaomba wapi kibali.
Kuna tofauti ya kukusanyika na kuishi. Kila Mkatoliki anaishi kwake, na hukutana kwa muda mchache.
 
Tatizo tunakimbilia kulaumu bila kufatilia kwa kina, nahili limekuwa Tatizo kwa vijana wengi.

Kamanda wa polisi ameeleze vyema kabisa, kwamba wao walienda kumfata mtoto kwa kibali cha mahakama nahuyu mtoto inasemekana alitoroshwa hali iliyopelekea asiendelee na masomo.

Walipofika kwa huyo mama hawakupewa ushirikiano, wakaongeza kikosi wakaingia kwa nguvu na kukuta mengine yanayoendelea humo ndani ni kinyume cha sheria.

Naweza kuwa nimeongeza au kupunuza maneno ila tafuta maelekezo ya kamanda wa polisi yatakusaidia
 
Zumalidi kasafirisha binadamu kutoka wapi kwenda wapi kwa lengo gani? Kuna jinai gani pale?
Eti usafirishaji wa binadamu!
 
Sukule jingine la zumaridi hili hao polisi hawakwenda kukagua bali kumkamata yule mama mtuhumiwa.
 
Kwa hiyo mfalme Zumaridi kakamatwa na polisi au kachezea kichapo cha Polisi?
Kama kuna lolote katika hilo naombeni mniwekee kavideo hapa.

Kwa jinsi wale mazombe walivyo wababaisha wale polisi na video kuonekana mtandaoni, ni lazima tu polisi wangekuja na kipigo kikali baadaye.
 
Angekuwa anakashifu dini ya kislamu huyu angekuwa marehemu ila kwavile amekashifu ukristo mmegeuka kuwa watetez wake
 
Back
Top Bottom