Daraja la busisi kigongo,limepewa jina linaitwa daraja la Magufuli!! Stand ya mkoa wa dsm imepewa jina inaitwa stand ya Magufuli!! uko dodoma kwa wagogo kuna mji umepewa jina unaitwa magufuli city!! Bado uwanja wa ndege wa chato nao utaitwa Magufuli international airport!!! Bado hamjalidhika mkaona mchonge na sanamu la marehemu lenye thamani ya tsh milioni 480!! Kweli?? Kweli??
Hii nchi inaitaji viongozi wanaopitisha matumizi ya pesa kufanya maujinga kama haya wachomwe moto hadharani kabisa,hizo pesa zinakarabati barabara ngapi za tarura? Hizo pesa zinajenga mashimo mangapi ya choo za shule? Hizo pesa zinajenga madarasa mangapi? Hizo pesa zinajenga nyumba ngapi za waalimu? Hizo pesa zinanunua vitabu vingapi mashuleni? Hizo zinajenga nyumba ngapi za waalimu? Hizo pesa zinajenga nyumba ngapi za madaktali wetu uko vijijini? Jameni!!
Wamepitisha bajeti wameongeza tozo kwenye kila muhamala utakaofanya kwenye simu,wameongeza tozo kwenye kila lita ya mafuta ya petrol!!,wameongeza tozo kwenye kila lita ya mafuta ya dizel!! Wameongeza tozo kwenye kila lita ya mafuta ya taa!!sawa tumekubali tufunge mkanda wanasema pesa ni za kujenga barabara za mjini na vijijini, ndio watumie pesa zote hizo kujenga sanamu kweli?!
Sanamu litasaidia nini wananchi kutatua kero zao?! pesa zetu wananchi sio za kujenga masanamu,pesa zetu ni za kujenga nchi yetu!! Viongozi wamekaa kwenye hizo nafasi wamevimbiwa mpaka wanaamua kujengeana masanamu! Tutakuja kumtia kiongozi kitu cha sanda mchana kweupe ili iwe fundisho kwa wajinga wenzake shwain.