Serikali inataka kutumia mbinu ya 'Sharpeville Massacre" kuifuta CHADEMA kama serikali ya Makaburu ilivyoifuta ANC

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Credit to Hilda Newton (X)

1960, polisi wa Makaburu katika kitongoji cha weusi cha Sharpville nchini Afrika Kusini walifyatua risasi kwa umati wa watu wasio na silaha waliokuwa wakiandamana kwa amani kupinga sheria kandamizi na kuua watu 69 na kujeruhi 186.

Serikali ya Makaburu ilidai kuwa wafuasi wa ANC na washirika wake walikuwa wakifanya vurugu na walipanga kupindua serikali. Viongozi wengi wa ANC walikamatwa na kufunguliwa kesi za uhaini.

Baada ya mauaji ya Sharpeville Kiongozi wa ANC Nelson Mandela akiwekwa kizuizini na chama cha ANC kilipigwa marufuku hadi 1990.

Mbinu hii ya Makaburu serikali ya Samia inataka kuitumia kuifuta Chadema.

Taarifa zinasema serikali ya Samia imepanga kuitumia ripoti ya Tume ya Jaji Othman Chande kuifutia usajili CHADEMA.

Baada ya mauaji ya Oktoba 29 (Tanzania Massacre), Serikali ilimuagiza msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi aifutie usajili CHADEMA ikidai ndo iliyoratibu Maandamano, Jaji Mutungi alikataa na kusema italeta shida zaidi maana nchi bado haijapoa. Kwahiyo Mama ameiagiza Tume ya Jaji Othuman Chande ifanye kila linalowezekana kwenye report yake iseme CHADEMA ndo chanzo cha Maandamano ya Oktoba 29.

Kuna Viongozi wengi wa CHADEMA wanakamatwa na kubambikwa kesi za Uhaini na Ugaidi na kulazimishwa kukiri kuwa wao ni viongozi wa Chadema na walikuwa na mpango wa kuipindua serikali ili waje kutoa ushahidi kwenye tume.

Mfano, huko Bunda wamemkamata aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa Yohana Kaunya wakimlazimisha aseme aliteuliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA kuratibu Maandamano ya Oktoba 29, Nchi mzima na kwamba yeye ndo alileta watu kutoka nchi jirani.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma Mzee Rajab Bujoro na Mwenyekiti wa CHADEMA Kasulu wamepewa kesi ya Ugaidi wamelazimishwa wakubali kwamba walipanga njama za kuingiza silaha kutoka nchi jirani.

Tume ya Othman Chande imeagizwa kupita kwa maRPC wote nchini na watapewa nakala za maelezo ya Viongozi na Wanachama wa CHADEMA waliokiri kuhusika na Maandamano ya Oktoba 29 ili wapate justification ya kuiangushia lawama zote CHADEMA then Tume itapendekeza CHADEMA ifutwe kwasababu inahatarisha Amani ya nchi.
 
Yana mwisho hata wakitaka kutumaliza watanzania wote,wakumbuke ukizoea damu za watu kuna siku watu watazoea hiyo damu kukufata na wewe.
 
Hicho chama kilikufa tangu 2015 sasa hivi kina watu wajinga ambao wanaeneza propaganda I was there
 
Chama kilichokufa ni CCM, hakina tena sera wala ushawishi. Kimepoteza mvuto, sasa sera yake ni kuteka na kuua watu. Kama maji tu yanawashinda mnachoweza ni nini. Mko madarakani sio kwa sababu wananchi wamewaweka hapo, ila kwa sababu mmetumia vyombo vya dola kuua watu na kujiapisha vichakani. CCM haina tofauti na Bhoko haram
 
Credit to Hilda Newton (X)

1960, polisi wa Makaburu katika kitongoji cha weusi cha Sharpville nchini Afrika Kusini walifyatua risasi kwa umati wa watu wasio na silaha waliokuwa wakiandamana kwa amani kupinga sheria kandamizi na kuua watu 69 na kujeruhi 186.

Serikali ya Makaburu ilidai kuwa wafuasi wa ANC na washirika wake walikuwa wakifanya vurugu na walipanga kupindua serikali. Viongozi wengi wa ANC walikamatwa na kufunguliwa kesi za uhaini.

Baada ya mauaji ya Sharpeville Kiongozi wa ANC Nelson Mandela akiwekwa kizuizini na chama cha ANC kilipigwa marufuku hadi 1990.

Mbinu hii ya Makaburu serikali ya Samia inataka kuitumia kuifuta Chadema.

Taarifa zinasema serikali ya Samia imepanga kuitumia ripoti ya Tume ya Jaji Othman Chande kuifutia usajili CHADEMA.

Baada ya mauaji ya Oktoba 29 (Tanzania Massacre), Serikali ilimuagiza msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi aifutie usajili CHADEMA ikidai ndo iliyoratibu Maandamano, Jaji Mutungi alikataa na kusema italeta shida zaidi maana nchi bado haijapoa. Kwahiyo Mama ameiagiza Tume ya Jaji Othuman Chande ifanye kila linalowezekana kwenye report yake iseme CHADEMA ndo chanzo cha Maandamano ya Oktoba 29.

Kuna Viongozi wengi wa CHADEMA wanakamatwa na kubambikwa kesi za Uhaini na Ugaidi na kulazimishwa kukiri kuwa wao ni viongozi wa Chadema na walikuwa na mpango wa kuipindua serikali ili waje kutoa ushahidi kwenye tume.

Mfano, huko Bunda wamemkamata aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Bavicha Taifa Yohana Kaunya wakimlazimisha aseme aliteuliwa na Kamati Kuu ya CHADEMA kuratibu Maandamano ya Oktoba 29, Nchi mzima na kwamba yeye ndo alileta watu kutoka nchi jirani.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma Mzee Rajab Bujoro na Mwenyekiti wa CHADEMA Kasulu wamepewa kesi ya Ugaidi wamelazimishwa wakubali kwamba walipanga njama za kuingiza silaha kutoka nchi jirani.

Tume ya Othman Chande imeagizwa kupita kwa maRPC wote nchini na watapewa nakala za maelezo ya Viongozi na Wanachama wa CHADEMA waliokiri kuhusika na Maandamano ya Oktoba 29 ili wapate justification ya kuiangushia lawama zote CHADEMA then Tume itapendekeza CHADEMA ifutwe kwasababu inahatarisha Amani ya nchi.
Sidhani maana ukweli unajulikanana wala chadema haikuhusika
 
Yani serikali ihangaike na Chama ambacho unaweza ukatembea mitaani siku mzima hata bendara Yao hauioni?
Chadema mmekaliwa na wananchi msiisingizie serikali
 
Kweli sikio la kufa halisikii dawa.
Hao wahuni watasababisha wananchi wengi sana waungane na GenZ halafu watajua hawajui
 
Yani serikali ihangaike na Chama ambacho unaweza ukatembea mitaani siku mzima hata bendara Yao hauioni?
Chadema mmekaliwa na wananchi msiisingizie serikali
Chama sio bendera, hivi bendera za CCM siku hizi unaziona.
 
CHADEMA iko kwenye mioyo ya wapenda mabadiliko wote nchini! Kuifuta kwa hila hakuwezi kuua upinzani kamwe. Huko ni kujidanganya tu.
 
Hili haliwezekani kwasababu ulimwengu wa miaka ya sharpvile massacre sio ulimwengu huu wa kidigitali ambapo sababu za maandamano ziko well documented watu wametekwa wengi mno na watu wamelalamika mnooo lakini amiri Jeshi mkuu hajawahi hata kukemea au kuwapa pole wafiwa au wahanga taasisi zimeongea mpaka za kiislamu (rejea waraka wa shura ya maimamu) Yani Kila sehemu kwenye nchi si mitaani si makanisani si misikitini kote watu wamelia kuhusu utekaji ccm walivyo wajinga bunge nalo ambapo ndio ingekuwa sehemu ya wananchi kupumulia (shorcup absorber) wakaipiga pini isijadili utekaji. Haya Mungu si athumani viongozi wa chadema kabla ya maandamano wote wakapigwa lockup akiwemo lissu ambae miezi tisa kabla ya maandamano alikuwa ndani. Sasa swali wataifuta chadema Kwa sababu zipi? Chadema inahusikaje na maandamano hayo? Chadema ndio waliowateka kina mdude polepole sativa kushambulia kina Kitima nk ? Wakijaribu kuifuta chadema maana yake wanatengeneza mlipuko wa volcano wa kuilipua Tanzania. Kama ndio lengo lao watafanikiwa kuitia kiberiti Tanzania ila kama sio lengo lao warudi chini hawatafanikiwa.
 
Halafu utakuta mtu anasema ati tufanye maandamano ya amani! Hata Mandela aliona kuwadai mafisadi na wanyonyaji uhuru kwa njia ya amani ni upuuzi! Akaamua kuanzisha umkotho we sizwe, na ilipelekea south africa kupata uhuru kwa njia hii!
 
Serikali hii haishindwi kitu kama imeweza kuua maelfu mchana kweupe still inakataa kuwa haijaua, itashindwaje kutunga sababu za uongo ili tu iweze kuifuta Chadema.
 
Halafu utakuta mtu anasema ati tufanye maandamano ya amani! Hata Mandela aliona kuwadai mafisadi na wanyonyaji uhuru kwa njia ya amani ni upuuzi! Akaamua kuanzisha umkotho we sizwe, na ilipelekea south africa kupata uhuru kwa njia hii!
Upo sahihi kabisa kuna wakati walikuja Morogoro wakapewa na majengo kupanga mbinu za kuikomboa SA.
 
Chama hakiwezi kufutwa kwa matakwa ya mtu mmoja mpumbavu amepanga kuharibu nchi yetu na sio kuleta maendeleo ameuwa na kupora haki za raia wengi.

Ndio maana amekimbia kijificha huko mapangoni. Hicho chama anachotaka kukifuta hatuta mskiliza muache ajitekenye alafu acheke mwenyewe hana mamlaka hayo alipatikana kwa wizi wa kura na uchaguzi usio halali.
 
Back
Top Bottom