Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Nafikiri umekurupuka, pia sio mbaya serikali ikiwapendelea hao, sioni ubaya wake.
Wewe una matatizo. Upendeleo wa aina yoyote ile ni ukiukwaji wa KATIBA waliyoapa kuilinda na kuitetea. Acha kushabikia ujinga mkuu. Watu wa sampuli yako ndio mnasababisha serikali isiboreshe shule za umma. Punguza ujinga kama huwezi kuacha.
 
Shule za bweni zipo aina nne
1. Vipaji maalum mf. Kilakala, ilboru n.k
2. Bweni ufundi mf. Moshi technical .nk
3. Bweni kitaifq mf. Moshi sekondari,
4. Bweni teule mf. Shule za jamii ya kifugaji kule monduli, ngorongoro na Longido ambapo wanafunzi wote wataingia bweni ili wasihame na wazazi wao hivyo kukosa masomo.

sasa hapa nitaongelea namba 1-3
Kwa nijuavyo kwenye selection wanaangalia ufaulu ila hawangalii idadi ya
Kwa maana kwamba wanaangalia jumla ya alama. kwa hiyo unaweza kuta mwanafunzi mwenye B ya 44 na A zingine 5 za 50 anakampita mwanafunzi mwenye A zote za 45 au 46 n.k

Pia kuna kigezo cha jinsia. kwamba kuna nafasi za wasichana na wavulana kwa uwiano sawa kama ni was 100 na wavulana 100. Wavulana kwa kawaida hufaulu sana kwa hiyo nafasi zao huishia kwa wenye alama nyingi lakin wasichana wanaweza wasipatikane wote wenye alama nyingi hivyo kupelekea wenye chache pia kupata

pia ili kuleta uwiano vizuri kila mkoa unagawiwa idadi ya wanafunzi wa kupeleka wanafunzi shule za bweni kwa kuzingatia wingi wa wanafunzi. Mfano. Dar wanaweza kupewa nafasi 300
Arusha 200 n.k
Sasa mkoa ukishapata unagawa pia kila wilaya kulingana na uwiano huo.

Sasa wilaya zikipokea wanaanza kuchagua wale wenye alama kuanzia 300 wanaenda vipaji
Nafasi za vipaji zikiisha wenye alama zinazofuatia wanaenda bweni ufund
N.k
Ukifuatilia mara nyingi unaweza kugundua kwamba kwa mwaka fulan mwanafunzi mwenye alama ya chini aliyechaguliwa bweni ni 285 kwa wavulana na 280 kwa wasichana.

Nadhan nmeeleweka.
N.b mimi ni mwalimu na sihusiki katika upangaji ila naelewa taratibu hizo
 
Hakuna aliyeshushwa. Tatizo wengi wenu mnaowapeleka watoto huko private mnajilazimisha wakati vipato vyenu ni vya kubangaiza. Na bado akienda chuo anaweza asipate mkopo au akapata kwa % chache.
Kwahiyo suluhisho ni kutujazia watoto wote wa darasa moja kwenye shule moja tena darasa moja?? Inaonyesha hujaelewa kabisa nini kinajadiliwa..!! Ishu ipo hivi, Mwenye C huko private aende hizo za kutwa na mwenye C huko primary za serikali naye aende huko sekondari za kutwa..!! Lakini kumchukua mwenye A wa private kumpeleka sekondari ya kutwa halafu mweye C toka kayumba aende shule maalumu ndo upendeleo ulipo..!! Na ndo kinacholalamikiwa..!! Hakujatajwa uwezo wa mzazi kulipa mamilioni au kushindwa kulipa mamilioni huko private..!!! Na kwa taarifa yako, si kila aliyeko Kayumba maana yake ameshindwa kulipa ada za mamilioni huko private. Ni maamuzi na mitazamo ya shule zipi kila mmoja anaona zinafaa kuwapeleka watoto wake.
 
NAOMBA TUCHUNGUZE

ZOEZI LA KWANZA
Nenda eneo lolote Tanganyika au Zanzibar,

Chukua makundi mawili ya watoto

Kila kundi watoto 40

Kundi moja peleka private primary school

Kundi moja peleka government primary school.

Chunguza matokeo yao ya mtihani wakiwa darasa la saba.

MASWALI
1. Je, watoto wa shule ipi wamefaulu zaidi?
2. Je, ufaulu wao unaleta tafsiri gani?

ZOEZI LA PILI
Nenda private primary school

Chukua vijana 20 darasa la Saba waliofaulu zaidi (bila shaka ufaulu Ni A,A,A)

Chukua vijana 20 darasa la Saba kutoka government primary school, waliofaulu zaidi, ( bila shaka ufaulu Ni B,B,B)

Vijana wote 40 wapeleke government secondary School
Chunguza matokeo yao kidato Cha Nne na sita

MASWALI
1, Je, ufaulu wao upoje? Unafanana au wale waliochukuliwa private wameshine zaidi ya wenzao?
2. Matokeo haya yanaleta tafakari gani?

ZOEZI LA TATU
Chukua vijana 40 waliofaulu zaidi shule za msingi wapeleke shule ya kata

Chukua vijana 40 waliofaulu kwa viwango vya chini, wapeleke Tabora boys, na Tabora girls

Chunguza matokeo yao baada ya kufanya NECTA

MASWALI
1. Je, shule ipi imefaulisha zaidi?
2. Je, matokeo hayo yanakupa tafsiri gani?

HITIMISHO
1. Jamii zetu zinabeba watu wasiotofautiana Sana kiakili!
Performance ya mtoto wa private haimpi uhalali wa yeye kuwa Genius zaidi ya wenzake wa government
Genius wa private atapimwa na wenzake huko private, na genius wa government atapimwa na wenzake huko government!

Uwepo wa private school haufuti uwepo wa vipaji vya akili huko government

Kwasababu special school za government ni kwa ajili ya watoto magenious wa Tanzania, then lazima tuende kila upande kuwachukuwa magenious hao

Kama tunataka magenious kadhaa, tunaweza kuamua kuwachukua baadhi upande huu na wengine upande ule

Ufaulu wa upande mmoja sio guarantee kuwa upande mwingine hauna magenious as long as maandalizi yao yalikuwa tofauti

2. Special school za government hazina miujiza!
Pale pana magenious, then wanafanya wonders
Shule za kata kwa Sasa Zina waalimu wa kutosha Kama kule special school, kinachowakosti Ni kubebeshwa wanafunzi waliofeli darasa la saba

NB
1. Kumbuka serikali haifanyi biashara ya Elimu
2. Lengo la serikali Ni kuleta Elimu kwa jamii, hivyo lazima izingatie tabaka zote, yaani jinsia, ulemavu, maskini na matajiri

Kama imepanga ziwepo shule za vipaji, lazime ihakikishe inazingatia vipaji kwenye kila tabaka, yaani jinsia zote, walemavu, maskini na tajiri, na hivyo haipaswi kupofushwa na matokeo ya mtihani tu!

3. Kwa sababu ya uchache wa special schools, wengi wenye vipaji hukosa nafasi.
Na Hawa wanaokosa Ni kutoka kwenye tabaka zote za jamii, ingawa hapa walalamishi Ni wa private school!

4, Kilicho muhimu Sasa Ni kugombana na serikali iboreshe shule zote, na si kugombana sisi kwa sisi kuwa mwanangu apate wako asipate, au kugombana na serikali kwamba kwanini umemteua mtoto wa mwenzangu Ila wangu umemuacha?
 
Dawa ya hii serekale pigana upate Hela huduma zote utapata bila bughudha lakini ukianza kutaka huduma yao only 20% is available out of 100%
 
Wewe una matatizo. Upendeleo wa aina yoyote ile ni ukiukwaji wa KATIBA waliyoapa kuilinda na kuitetea. Acha kushabikia ujinga mkuu. Watu wa sampuli yako ndio mnasababisha serikali isiboreshe shule za umma. Punguza ujinga kama huwezi kuacha.

Unaongelea ukiukwaji wa Katiba Tanzania? Endelea na huo mjadala.
 
Dawa ya hii serekale pigana upate Hela huduma zote utapata bila bughudha lakini ukianza kutaka huduma yao only 20% is available out of 100%
Hapa ndo unaharibu!
Kama rushwa inasaidia endelea ikusaidie sio kuifanyia promo

Rushwa Ni mbaya Sana, hujaitafakari tu!
Kukosesha watu haki
Kuharibia watu maisha ambavyo walistahili na wewe usiostahili kujinyakulia Ni laana zaidi ya kwenda kwa mpalange!

Mimi naamini wote tusingetoa rushwa, huduma zingetolewa tu
 
shule za gharama sio vipaji,kwanini sio vipaji? unaweza kujiuliza, jibu. shule za gharama Ina kila kitu cha kumfanya mwanafunzi apate alaama A.mfano nikupe chukua mwanafunzi ambaye amesoma shule za kawaida amepata alama A.je angesoma shule za gharama huyo mwanafunzi angepata alama gani? toa jibu mbona umekaa kimya
 
Hebu jiulize kama wote waliopata A wapelekwe kwenye shule Teule hao wa B na C nani atawapa changamoto.
 
K
Kwani Nani amezuia serikali usiweke mazingira mazuri ya watoto kupata elimu Bora Kama wanavyofanya shule binafsi?
Mbona Nyerere na Mwinyi waliweza ?
Enzi hizo shule za serikali ndiyo za kifahari na za binafsi wanaenda walikwama za serikali.
 
Kuna mdau aliandika humu, hakuna kitu hata kimoja ambacho serikali inafanya kwa ufasaha na usahihi. Ni kuunga unga tu mradi pakuche
Nimeshangaa sana hawa jamaa. Kuna dogo kijijini kwetu amepata wastani wa C mbovu kabisa eti amepangiwa korogwe girls alafu wale madogo waliopiga A wamepangiwa shule za kata. Duh
 
Unaongelea ukiukwaji wa Katiba Tanzania? Endelea na huo mjadala.
Katiba inatamka wazi kuhusu USAWA. Wewe unashabikia UPEBDELEO na UBAGUZI. Una akili timamu kweli?
 
we
we bwege endelea kuwasomesha shule binafsi, ulivyowapeleka shule binafsi shule ya msingi ulikuwa una malengo waende shule teule? Serikali iko makini, km hutaki waende hiyo shule ya kata warudishwe huko binafsi. Na ukae ukijua wataenda kusoma vyuo vya serikali na hawatakuwa na mikopo. Kupanga ni kuchagua. Mnaopeleka watoto hizo shule za gharama ni mabwege tu mnaoliwa hela na wajanja, walimu wanaowafundisha huko private ni watanzania wale wale waliosoma vyuo vya serikali, tofauti ni gharama na kiinglishi cha kuongea mtaani siyo kiinglishi cha kitaaluma. Watanzania wakiwa na vijihela kidogo ni malimbukeni.
 
Kwa kweli hii serikali ina mambo ya kipumbavu sana. Sijui wanafikiri kwa kutumia kiungo gani (Masaburi).
nyie ni mna mambo ya kipumbavu, msiipangie serikali namna ya kuendesha shughuli zake, pambananeni na watoto wetu mnavyotaka mabwege nyie
 
Hivi unajua unachokiongea kweli mkuu? Hesabu gani hizo ambazo hazifuati ufaulu? Ina maana hizi nafasi zinagawiwa kama njugu kwa matakwa ya watu kutoka juu? Ili iweje?
wakati mnapeleka watoto wenu private primary mlikuwa mna malengo gani, na kwanini leo mtake tena shule za serikali, kwanini msiendelee kuwasomesha huko private? Hata hivyo unatakiwa ujue vyuoni ataenda vyuo vya serikali tena akifaulu vizuri. Tatizo watanzania wanapenda sana social classes, elimu imekuwa km maonesho. Mwisho msitake serikali ifanye kazi kwa maslahi yenu, pambanneni na hali zenu.
 
kuna mitihani ya Cambridge wapeleke huko hao watoto wako we kenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…