Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Umeandika upumbavu mtupu. Serikali iko sahihi 100% kufanya hivyo. Tena wamechelewa mno kuanza huo utaratibu. Kama ulisomesha mtoto private peleka mtoto private. Acha hao watoto wa St Kayumba waliofanya vizuri na wao wakasome shule bora zinazoitwa teule. Ila ninaisihi sana serikali kuendelea kupambana kuboresha shule za serikali. Anayesoma Kigogo Sec awe na mazingira mazuri kama wa Tanga tech au Ilboru sec.
Alafu the likes of huyu ndo washauri wa Mama...
Wapumbavu...
 
Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.

Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.

Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.

Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392

Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!

Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?

Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Wangekuwa wanawachukua hata nusu yao ya wanafunzi waliofanya vizuri, kwa kuwa wametokea kwenye shule zenye mazingira bora kwa baada Taifa lingekuja kupata wataalamu walio bora zaidi. Lakini wao watakuwa wanawaza kuwa kwa kuwa hawa wanafunzi wametokea kwenye shule zenye mazingira bora hivyo basi mategemeo yao wanawataka waje kuzipandisha hadhi shule za kata.
 
Sio kwamba waliopata A wote wanaenda shule za bweni, wewe una uhakika gan kama A zao zilikua Kali zaid, kinachowapeleka shule Nzuri ni marks walizopata,
Ina maana zile A zote za kumwaga kutoka shule binafsi ni A feki mkuu? Mbona unatetea ujinga?
 
Hao wa Private si waende shule za Private.. mbona Unalilia shule teule za Serikali..? Huwezi kumpangia Mmiliki
Mkuu umetokea wapi mbona unakuja kwa kukurupuka kama panya? Hapa hatuongelei UMILIKI bali tunaongelea UCHAGUZI WA WANAFUNZI. Umeelewa?
 
Kwani hizo shule teule zinafundishwa na walimu kutoka wp? Si ni walimu hao hao wanaofundisha shule za kata?

Ulitaka mwanao apelekwe shule teule ili utambishie wenzako au sio, mpeleke huko mwandege mwanao akasome kama hujaridhika mpeleke fedha, tusiime au St.francis....hela yako tu.
 
Mtoto aliepata B ya akisoma kayumba
Uwezi mfananisha na mtoto aliepata A akisoma Private school

Ni watoto wawili wenye uwezo tofauti ukizingatia vema mazingira ya usomaji

Kingine, Watoto wengi toka private wanaochaguliwa shule teule, hawaendi

Wanaenda zao feza, Marian, n.k

Nadhan serikali pia imezingatia hilo
Asante kwa ushauri mkuu. Maoni yako yamezingatiwa. Lakini ukweli ni kwamba shule nzuri Marian Feza, St Francis et al hazitoshi kuwameza wanafunzi wote wa shule za private.

Suluhisho ni serikali ifanya selection isiyokuwa biased ili mzazi mwenye uhitaji wa kumpeleka mtoto wake special school afanye hivyo. Wasichukulie hasira kwamba wazazi hawapeleki watoto. Na ndio maana kunakuwa na seond selection ili kuziba nafasi za wale watakaokacha.
 
Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.

Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.

Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.

Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392

Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!

Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Kwaiyo mlitaka shule nzuri za awali wasome watoto zenu?

Shule za bora za secondary wasome watoto zenu?

Na vyuo vikuu bora wasome watoto zenu tena hao hao wapewe priority ya kupewa mikopo?

Na kazi pia nzuri watoto zenu ndo wapewe watoto zenu kwanza?

Kwa ulichoandika hapa endapo kama ungenambia kwa mdomo ningekutukana
 
Na mimi nitaelezea uzoefu wangu katika swala hili la selection kwa kidato cha kwanza. Jambo hili naweza kusema kwamba halijaanza leo, linaweza kuwa limeanzia tangu miaka ya 2008 na litaendelea. Kwanini nasema hivi? Sababu ni hii mimi mwenyewe nilikumbwa na kadhia hii hii japo nilisoma shule ya serikali. Matokeo yetu ya shule ya msingi yalikuwa mazuri mno kwani shule yetu ilikuwa inafahamika kwa kufaulisha vizuri. Lakini lilipokuja swala la selection za kidato cha kwanza hadi waalimu pale shuleni walibaki kushangaa. Kwani kwa ufaulu nilioupata na kupelekwa shule ya kata nilipofika kule nilishangaa. Nilitegemea kupelekwa shule ya mkoa kama si wilaya. Kwani kuna wanafunzi waliokuwa na ufaulu kama wangu wa shule nyingine na walipelekwa shule za mkoa au wilaya. Na kibaya zaidi aliyefaulu kwa ufaulu wa juu zaidi pale shuleni kwetu aliishia kupelekwa Azania wakati mdada aliyemfuata ndiye aliyepelekwa Shule ya Vipaji yaani Kilakala. Kwa kweli ilikuwa ni sintofahamu sanaa. Kwahiyo nataka kusema hili swala kwa sasa hv ndo linaanza kuonekana ukubwa wake. Lakini lilianzia miaka ya nyuma kabisa. Kuwa na amani, muhimize kijana wako asome kwa bidii katika shule aliyochaguliwa atafaulu, au laa ukiona haujaridhika baadae umuhamishie shule nyingine ya serikali utakayoona ina uhafadhali kuliko hiyo. Shule za Kata zimekuwa zikitazamika vibaya katika jamii zetu kutokana na miundombino pamoja na vitendea kazi vya kufundishia lakini pia na aina ya wanafunzi wapelekwao huko. Wengi wao wanakuwa ni wale wasindikizaji hili linazidi kuzifanya shule hizi kuzidi kudharaulika lakini, wewe kama mzazi lisikuvunje moyo mpambanie mwanao na atafanikiwa. Mimi nilifaulu vizuri kuliko hata baadhi ya waliopelekwaga shule za mkoa na wilaya sijisifii lakini natoa ushuhuda.
Ulisoma Private!?
Ndo mjadala uliopo....
 
Kwaiyo mlitaka shule nzuri za awali wasome watoto zenu?

Shule za bora za secondary wasome watoto zenu?

Na vyuo vikuu bora wasome watoto zenu tena hao hao wapewe priority ya kupewa mikopo?

Na kazi pia nzuri watoto zenu ndo wapewe watoto zenu kwanza?

Kwa ulichoandika hapa endapo kama ungenambia kwa mdomo ningekutukana
Kwani we watoto zako wako wapi!?
 
Mkuu unapaswa kuzingatia pia mazingira ya usomaji Kati ya private na kayumba
Kama ni hivyo basi serikali iwe inatunga mitihani miwili tofauti:
1. Mitihani rahisi ya kubet kwa ajili ya wanafunzi wa shule za kata.
2. Mitihani migumu ya kujaza na kukokotoa mwenyewe kwa ajili ya shule binafsi.
 
Serikali inajua kabisa gap lililopo kwenye jamii kati ya wenye nacho na wasio nacho hivyo ikienda na hizi akili zenu za kishenzi watoto wa walalahoi watazaidi kuwa walalahoi. Angalau hao wanaojitahidi wakipelekwa shule nzuri sekondari itasaidia. Na wengi wao wakitoka Kayumba kwenda shule teule huwa breki ni University. Nyie mliojaliwa kipato pelekeni watoto sekondari za private mkuze uchumi. Tatizo wengi wenu pia mna hela za papatu papatu ndo maana mnataka ahueni mtoto aende shule nzuri za serikali. Hii SERIKALI YA CCM iko makini na wajinga wajinga kama wewe.
Umeongea point,
Mwenye maskio na asikie
 
Selection ipo Sawa

Nakupa mfano

John kapata math 41 "A" English 42 " A" wastan hapo ni 42

ISSA kapata Math 48 "A" English 38 "B" wastan hapo ni "43"

Hapo John na ISSA nan kamzid mwenzake ufaulu?
Mkuu hii mifano yako sio hai. Hebu rejea kusoma andiko langu kwenye uzi utanielewa ninachomaanisha.
 
Huwa inatokea mwanafunz A akawa na "C" 4 na "D" mbili lakin wastan "D"

Mwingine akawa na "C" 2 na "D" 4 lakin wastan "C"

Haya mambo mwanzisha mada umekurupuka
Toa mifano hai acha kukurupuka mkuu.
 
Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.

Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.

Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.

Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392

Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!

Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?

Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024

Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Alivyomuondoa Dr.Msonde pale NECTA nikajua hapa hadhi ya NECTA lazima ishuke tu!
Shida Wanzanzibar wabaguzi na wadini sana!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo ndio maana serikali inaamua KUBORESHA mazingira ya shule zake kwa kufanya upendeleo kwenye selection?
Jambo la ajabu sana hili.Sijui kama watafanikiwa kwa mkakati huo mbovu.Serikali lazima ione ni kwa namna gani itacope na strategies zinatumika private mpaka watoto wao wanainyanyasa mitihani ya baraza vile

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom