Hapa kinachoongelewa ni juu ya Covid19 na sio malaria
Yote ni maradhi ndio maana nimetoa mfano huo kuwa sio mpaka mtu aumwe malaria ndio aweze kujua kuwa malaria ipo na inauwa,sawa na corona kama corona ipo basi sio mpaka mie niumwe ndio niweze kujua ipo.
 
Kabisa mkuu vyuoni kuna misongamano mikubwa mno isiyofuata tahadhari yoyote full kukumbatiana na kisses kibao kwa wapendanao
Achilia mbali makanisani kwenye vyombo vya usafiri, masokoni mbona watu wangeanguka sana kama kweli ingekuepo .
Acha kuongea kama fala nina uchungu sana hapa nlipo mmoja wa family members wangu kaipata hii nlikuwa sitaki kuamini kama Corona ipo but wanasema mdharau mwiba humchoma
 
Acha kuongea kama fala nina uchungu sana hapa nlipo mmoja wa family members wangu kaipata hii nlikuwa sitaki kuamini kama Corona ipo but wanasema mdharau mwiba humchoma
Pole kwa kupoteza mpendwa wako mkuu na siongei kama fala naandika ninachokiamini usitake niamini uaminivyo mkuu

Nawasilisha
 
Magufuli ameshamsifia balozi wa china kwa kutovaa barakoa.

Unaelewa hilo? Unaelewa ujumbe anaoutuma kwa wananchi hapo?

Magufuli na viongozi wake wanatoa maelekezo yanayotoa sera za serikali. Na kwa sasa, kiukweli,sera ya serikali ni kuficha ukweli, ndiyo maana hata haitangazi kuna wagonjwa wangapi Tanzania.

Uko na Magufuli katika sera hi ya kuficha ukweli?
 
Mwanzo ilikuwa vifo vya corona vinatangazwa na idadi ya wagonjwa hutangazwa, ila sasa hawafanyi tena hivyo sasa unategemea utapataje uthibitisho kuwa ipo au haipo?
Siishi dunia ya peke angu mkuu naishi na nachangamana na binadamu wenzangu likitokea jambo na mimi ni rahisi kuhusishwa na kujua kwa maana iyo sasa toka corona imetoweka nchini sijaskia kisa chochote kihusianacho na huo ugonjwa
 
Unataka kuambiwa na nani na mara mgapi kwamba ugonjwa upo, swala la kujilinda ni la mtu binafsi.
Chukua tahadhari kama ichukuliwayo katika magonjwa mengine, malaria, ukimwi, kuhara bila kuzua HOFU.

Inakisiwa vijirusi vinabadilikabadilika, inamaanisha hata maambukizi, dalili na hata ukali wake unatofautiana kutoka mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Pia haijatambuliwa madhara yake ya muda mrefu yatakua ni nini kwa aliyeugua katika mfumo wa mwili.
Ni ujinga kufikiri kuwa matokeo ya ugonjwa ni kifo. Kila ugonjwa una mlango wa kutokea ikiwa ni pamoja na kupona, kupata kilema na kifo kama tokeo. Kufikiri katika Hofu ya kifo tu ni matumizi mabaya ya akili.
 
Tatizo ni kufikiri serikali ni viongozi hata wewe na waandishi humu ndani ni sehemu ya serikali, kuna njia mbalimbali ya kutoa taarifa. Tahadhari ni muhimu kwa kila ugonjwa
 
Siishi dunia ya peke angu mkuu naishi na nachangamana na binadamu wenzangu likitokea jambo na mimi ni rahisi kuhusishwa na kujua kwa maana iyo sasa toka corona imetoweka nchini sijaskia kisa chochote kihusianacho na huo ugonjwa
Mkuu kilitumika kipimo gani kuweza kujua kuwa corona imetoweka? kwa sababu nachojua serikali iliacha kupima na kutoa takwimu katika kipindi ambacho corona ndio imepamba moto.
 
Rais kila mara anawatangazia watu kuwa Tanzania hakuna korona.
Mimi naweza kujihadhari lakini vipi kuhusu mamilioni ya wananchi wanaomsikiliza na kumuamini, huoni kuwa anawapa info zinazowamislead?
 
Tuache lawama zisizo na msingi kwa mtu au taasisi. Muda huu tukiambiwa hakuna Ukimwi na Malaria tutaacha kutofanya ngono zembe au kutumia chandarua?
Jilinde na walinde na ndugu zako.
Kila kitu kimeainishwa katika miongozo ya wizara ya Afya. Tuna vyombo vya habari. Kutokutimiza wajibu kwa kila mmoja wetu ndio kutatuletea majanga
Ukiangalia miji na nchi zinazoumia ni zile zenye miingiliano mikubwa ya wasafiri.
 
Hata katika ulimwengu tumepewa uhuru wa kuchagua jema na baya. Tushawaza kwa nini tunatenda mabaya kwa wingi?
Kwa sababu kila tutendapo baya kuna wa kumsingizia(nimedanganywa na shetani)
Ndivyo binadam tuangamiavyo.
 
Wasiotumia condom na chandarua wako wengi pamoja na kujua kuwa kuna ukimwi na malaria,ukiangaloa sasa hivi jinsi ukimwi unavyochukuliwa ni kama wanadharau ukimwi sasa wakiambiwa hakuna ukimwi ndio kabisa.
 
Corona ipo watu wanakufa chukua tahadhari husika. Usiamini Serikali iliyojaa waongo.
 

Huu ndiyo uazalendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…