Hakuna vifo vilivyothibitishwa kua vimetokana na corona hata mimi na watu walionizunguka hakuna hata dalili ya corona miongoni mwetu sijui
Kabla hata serikali kutangaza hakuna corona watanzania wenyewe toka mwanzo hawakuwa serious na kujikinga corona,kipindi kile ni level seat walikuwa wanakaa chini kwenye daladala ili wasionekane na traffic hawakuwa wakijali kuhusu corona,huko kariakoo watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,huko mitaani kulikuwa hakuna kilichobadilika walikuwa wanaweka ndoo za maji ya kunawa kwa sababu ni matakwa ya serikali.Corona ipo watu wanakufa chukua tahadhari husika. Usiamini Serikali iliyojaa waongo.
Corona ipo watu wanakufa chukua tahadhari husika. Usiamini Serikali iliyojaa waongo.
Kabla hata serikali kutangaza hakuna corona watanzania wenyewe toka mwanzo hawakuwa serious na kujikinga corona,kipindi kile ni level seat walikuwa wanakaa chini kwenye daladala ili wasionekane na traffic hawakuwa wakijali kuhusu corona,huko kariakoo watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,huko mitaani kulikuwa hakuna kilichobadilika walikuwa wanaweka ndoo za maji ya kunawa kwa sababu ni matakwa ya serikali.
Kwa hili la Corona na mengineyo ni punguani peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa Tanzania kuna serekali!
Kondoo walikuwa wanaishi kwa ustawi na kwa uhuru kwenye nyika za dunia kabla ya kuanza domestication of animals by humans. Hawahitaji mchungaji wa kuwaonyesha wapi pa kula na jinsi ya ku survive kwa kamba na viboko.inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.
ukishaona meko kajichimbia chato weka mstari kuhusu covid-19 lile jamaa halina mpango na watanzania kuhusu hili janga yeye anachoangalia asiwapoteze watalii kuja nchiniCorona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.
Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.
Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.
Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc
Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo
Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc
Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.
Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!
Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.
Tunataka kusikia kauli ya serikali, Je Corona ipo Tanzania?, Je serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?
Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?
Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana!. Je ngoma imerudi kama mwaka jana?
Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata
Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
Ndio nakwambia kwamba hata kipindi cha mwanzoni ambapo serikali inatangaza kuwepo corona na kuhimiza watu kuchukua tahadhari na hadi ikafunga mashule na mambo mengine,bado ilikuwa watanzania wenyewe hawakuwa serious kuchukua tahadhari kwenye corona. Kwahiyo asilimia kubwa ya watanzania toka tunatangaziwa kuwa kuna corona wao walikuwa wanaishi kama hakuna corona na ndio maana hata walipokuja kuambiwa hakuna tena corona haikuwa shida kwao kukubali hilo jambo.Serikali hii pamoja na kuwa ni Serikali haramu kwa kuwa haikupata ridhaa kutoka kwa Watanzania bali walipora uchaguzi iache kusema uongo eti Mungu katunusuru! Hata kule Saudi Arabia na Vatican pia wanamjua sana Mungu na si ajabu wanafanya ibada na kuomba sana kuhusu COVID19 lakini Serikali hazifichi ukweli kwamba ugonjwa uko na raia wa huko wanakufa.
Huu uongo kwamba Tanzania hakuna COVID19 ni hatari sana kwani unawafanya Watanzania wengi kuamini uongo huo na hivyo kutochukua tahadhari husika matokeo yake ugonjwa kusambaa kwa kasi kubwa na kusababisha vifo vingi vya Watanzania ambavyo vingeweza kuzuilika kama wengi wangechukua tahadhari ya kujikinga na COVID19.,
Unajua wakati mwengine issue sio tu kwamba tatizo lipo au halipo,je uhalisia wa hilo tatizo ukoje?Hatuwezi kuondoa tatizo kwa Kujidanganya na kujifariji halipoo...!! Corona balaa sanaaa...
Kuchukua tahadhari peke yako hakukusaidii kitu.Tumeshasahau CORONA....We chukua tahadhari na ujilinde hiyo ni Rai ya Serikali ..hatutaki taharuki...! Taharuki mpelekee DJ.