#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Utathibitisha vipi kuhusu vifo vya COVID19 wakati serikali iliyojaa wasema uongo imeamua kuendelea na uongo wao kwamba Tanzania hakuna COVID19?
Hakuna vifo vilivyothibitishwa kua vimetokana na corona hata mimi na watu walionizunguka hakuna hata dalili ya corona miongoni mwetu sijui
 
Corona ipo watu wanakufa chukua tahadhari husika. Usiamini Serikali iliyojaa waongo.
Kabla hata serikali kutangaza hakuna corona watanzania wenyewe toka mwanzo hawakuwa serious na kujikinga corona,kipindi kile ni level seat walikuwa wanakaa chini kwenye daladala ili wasionekane na traffic hawakuwa wakijali kuhusu corona,huko kariakoo watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,huko mitaani kulikuwa hakuna kilichobadilika walikuwa wanaweka ndoo za maji ya kunawa kwa sababu ni matakwa ya serikali.
 
Corona ipo watu wanakufa chukua tahadhari husika. Usiamini Serikali iliyojaa waongo.

Kuna mwamba wa ubalozi wa marekani kakata kamba...Mwache aendelee kujidanganya.

USE.jpg
 
  • Masikitiko
Reactions: BAK
Serikali hii pamoja na kuwa ni Serikali haramu kwa kuwa haikupata ridhaa kutoka kwa Watanzania bali walipora uchaguzi iache kusema uongo eti Mungu katunusuru! Hata kule Saudi Arabia na Vatican pia wanamjua sana Mungu na si ajabu wanafanya ibada na kuomba sana kuhusu COVID19 lakini Serikali hazifichi ukweli kwamba ugonjwa uko na raia wa huko wanakufa.

Huu uongo kwamba Tanzania hakuna COVID19 ni hatari sana kwani unawafanya Watanzania wengi kuamini uongo huo na hivyo kutochukua tahadhari husika matokeo yake ugonjwa kusambaa kwa kasi kubwa na kusababisha vifo vingi vya Watanzania ambavyo vingeweza kuzuilika kama wengi wangechukua tahadhari ya kujikinga na COVID19.,

Kabla hata serikali kutangaza hakuna corona watanzania wenyewe toka mwanzo hawakuwa serious na kujikinga corona,kipindi kile ni level seat walikuwa wanakaa chini kwenye daladala ili wasionekane na traffic hawakuwa wakijali kuhusu corona,huko kariakoo watu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,huko mitaani kulikuwa hakuna kilichobadilika walikuwa wanaweka ndoo za maji ya kunawa kwa sababu ni matakwa ya serikali.
 
inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.
Kondoo walikuwa wanaishi kwa ustawi na kwa uhuru kwenye nyika za dunia kabla ya kuanza domestication of animals by humans. Hawahitaji mchungaji wa kuwaonyesha wapi pa kula na jinsi ya ku survive kwa kamba na viboko.
 
Hii kitu ipo sana sana na inakata watu kwelikweli.

Sasa inaitwa Penumia
 
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa.

Serikali zilizo responsible duniani zinaendelea kutekeleza sera za kupambana na Covid na kamwe hazitangazi kuwa zimeshashinda vita tayari, bali zinakuwa cautious na zinaendelea na jitihada za kupambana na huu ugonjwa.

Siyo siri, sisi Tanzania kwa kiwango kikubwa tulinusurika na wimbi la kwanza la maambukizi yale. Mungu wetu alitusaidia na kwa kweli watanzania walijitahidi pia kuchukua hatua, kila sehemu kulikuwa na ndoo za kunawa mikono etc

Pamoja na mafanikio yale haikuwa sahihi na haiendelei kuwa sahihi serikali kukaa kimya na kuacha kila mtu aamini Korona haipo nchini, au kuuaminisha umma kuwa korona haipo kabisa. kufanya hivyo siyo sahihi hata kidogo

Lakini cha kushangaza zaidi ni pale serikali na vingozi wake walipoanza kudiscourage wananchi kuchukua hatua za kujikinga. Barakoa zilianza kufanyiwa mizaha etc

Serikali ilipaswa iendelee kuhimiza watu waendelee kuchukua hatua, na kuencourage watu kujilinda lakini siyo kudiscourage measures zote ambazo wananchi wanafanya.

Labda kitu kimoja ambacho serikali lazima ielewe ni kuwa sasa wananchi wameanza kuwa na wasiwasi kuwa Korona ipo nchini, lakini wanakosa uhakika wa kimamlaka kulichukulia kwa uzito stahili maana serikali imeamua kupiga kimya!

Mimi ningependa kuieleza serikali yetu kuwa ni higly irresponsible katika kipindi hiki dunia imeingia katika vita ya pili juu ya huu ugonjwa lakini yenyewe imekaa kimya tu inawaacha wananchi peke yao utafikiri kondoo wasio na mchungaji.

Tunataka kusikia kauli ya serikali, Je Corona ipo Tanzania?, Je serikali ina mpango gani au imeamua wenye kuugua waugue, wenye kufa wafe lakini yenyewe itakaa kimya tu?

Nchi jirani zetu baadhi zimeanza kuchukua hatua kali mipakani mwao kuhusu wanaoingia, je sisi mambo shwari tu hakuna ishu?

Sisi tukimuona rais wetu amekwenda tena Chato kipindi hiki tukiambiwa kuwa Corona imechachamaa huko duniani tunapata wasiwasi kuwa huenda yasemwayo mitaani kuwa ni kweli maana tunakumbuka kipindi kule rais alipokwenda kukaa huko Chato kwa zaidi ya miezi miwili kipindi Corona imechachamaa mwaka jana!. Je ngoma imerudi kama mwaka jana?

Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata

Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
ukishaona meko kajichimbia chato weka mstari kuhusu covid-19 lile jamaa halina mpango na watanzania kuhusu hili janga yeye anachoangalia asiwapoteze watalii kuja nchini
 
Serikali hii pamoja na kuwa ni Serikali haramu kwa kuwa haikupata ridhaa kutoka kwa Watanzania bali walipora uchaguzi iache kusema uongo eti Mungu katunusuru! Hata kule Saudi Arabia na Vatican pia wanamjua sana Mungu na si ajabu wanafanya ibada na kuomba sana kuhusu COVID19 lakini Serikali hazifichi ukweli kwamba ugonjwa uko na raia wa huko wanakufa.

Huu uongo kwamba Tanzania hakuna COVID19 ni hatari sana kwani unawafanya Watanzania wengi kuamini uongo huo na hivyo kutochukua tahadhari husika matokeo yake ugonjwa kusambaa kwa kasi kubwa na kusababisha vifo vingi vya Watanzania ambavyo vingeweza kuzuilika kama wengi wangechukua tahadhari ya kujikinga na COVID19.,
Ndio nakwambia kwamba hata kipindi cha mwanzoni ambapo serikali inatangaza kuwepo corona na kuhimiza watu kuchukua tahadhari na hadi ikafunga mashule na mambo mengine,bado ilikuwa watanzania wenyewe hawakuwa serious kuchukua tahadhari kwenye corona. Kwahiyo asilimia kubwa ya watanzania toka tunatangaziwa kuwa kuna corona wao walikuwa wanaishi kama hakuna corona na ndio maana hata walipokuja kuambiwa hakuna tena corona haikuwa shida kwao kukubali hilo jambo.
 
Hatuwezi kuondoa tatizo kwa Kujidanganya na kujifariji halipoo...!! Corona balaa sanaaa...
Unajua wakati mwengine issue sio tu kwamba tatizo lipo au halipo,je uhalisia wa hilo tatizo ukoje?
 
Ugonjwa wa corona kupuuzwa si jambo geni kwa nchi maskin i kama ya kwetu. UKIMWI ulipuuzwa hadi wazungu wakaingilia kati kwa kutoa misaada ya vipimo na dawa, umaskini umepuuzwa tangu uhuru hadi sasa. Corona tusubiri wazungu wakimaliza kutoa chanjo kwa watu wao na kuitokomeza kabisa ndipo watahamia huku kwetu.
Kuzaliwa kwenye taifa maskini nadhani hata akili zinakuwa maskini maana mtu mmoja tu alivyoupuuza kila mtu sasa amepuuza kuanzia viongozi, wasoni na jamii kwa ujumla.
Kazi ipo kwelikweli.

Landson Tz
 
1. Nyungu zirudi (Mh. Jafo ongoza hili kamanda wangu).
2. Gari za abiria zipakie level seat inclusive mwendokasi.
3. Barakoa iwe lazima kwenye maeneo ya mikusanyiko na vyombo vya usafiri.
4. Zingatia kusimama futi 6(1.5M) kutoka alipo mtu wa karibu yako.
5. Ukipatwa na homa usipaniki, endelea na maisha mengine lakini hakikisha unavaa barakoa ili kuwakinga wengine.
6. Maombi ya kitaifa yarudi tena ikiwezekana yawe nonstop(Viongozi wa dini tusaidieni kwa hili).

Naomba ieleweke corona virus anasababisha pneumonia. Pneumonia ni pneumonia, haijalishi imesababishwa na kirusi ama vumbi ama kupaliwa. Pneumonia inaweza kumpata mtu yoyote yule wa umri wowote ila makali yake yatayegemeana na nguvu za kinga za muhusika. Ndio maana watoto wachanga huwa wanapata chanjo ya pneumonia sababu kinga zao bado hazina nguvu.

Hata hii pneumonia inayosababishwa na corona ni pneumonia kama pneumonia zingine. Lkn tofauti inakuja kwenye namna huyu kirusi anavyosambaa kwa kasi. Na huyu kirusi anakula mapafu, kitu kinachofanya awe hatari kushinda visababishi vingine vya pneumonia.

Mama Gwajima, fieldmarshal wa sekta ya afya, rudisheni zile measures mlizochukua mwaka jana, hatutaki data zenu bali hatua madhubuti ili kuepusha usambaaji wa huyu mdudu. Watu wamerelax mnoo mtaani. Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba, tena iwe ya mapema kabla haijawa too late.

Nimeongea haya baada ya kumshuhudia jamaa yangu leo akihemea juu juu. Kwa kweli huwezi elewa ubaya wa hii kitu mpaka ikupate au umshuhudie nduguyo au jirani yako akiteseka nayo. Its very terrible bandugu, usiombe kabisa.


 
Tanzania hakuna corona. Tuongeze uzalishaji wa mazao ili tuwauzie hao wenye kuteseka na nafaka kwa sasa maana hawatakuwa na chakula mwakani
 
Hii kitu kwa kweli ipo sana tu, juzi Kuna mtu wangu wa karibu amepoteza Dada yake kama masihara, ndani siku kama 3 alikuwa analalamika kifua na koo juzi akazidiwa kupelekwa hospitali doctor akasema ana shida ya upumuaji,akashauru awekewe mtungi wa oxygen ndani ya masaa 4 akavuta.

Majibu ya Daktari ni pneumonia ndiyo imemchukua 🙄🙄🙄🙄. Muuguzaji akaambiwa na wewe ukirudi nyumbani kunywa vitamin C na Zinc 😳😳😳😳.

Waungwana hebu mwenye uwelewa atufafanulie hili
 
Back
Top Bottom